Sunday, March 31, 2013

MIILI YA WATU ILIYOPATIKANA KWENYE GHOROFA LILILOANGUKA DAR IMEFIKIA 21 MPAKA SASA



Miili ya watu iliyoopolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo lenye ghorofa 16 lililoanguka jana katikati ya jiji la Dar es Salaam, imefikia 21. 
BGkNxjCCQAEyljV
Shughuli za uokoaji zilizoanza jana bado zinaendelea kwa siku ya pili huku kukiwa na taarifa za kuwepo miili zaidi kwenye vifusi hivyo.

Jana Rais Jakaya Mrisho Kikwete alitembelea katika eneo la jengo hilo lililoporomoka lililopo Mtaaa wa Indira Gandhi/Morogoro.
BGhTCALCEAA5EUX
BGhxvZyCAAACKUS
BGj2L20CcAAk2Qh
BGk_iPYCMAA0JzE
BGkGOFQCAAAxCuR
BGkHMJ2CYAAqKHE
BGkhNw7CAAA6hR1
BGkOUrrCIAAEF5U
BGlcQBeCUAA_li0
BGlhHCDCAAEk1YB
BGlHo3LCAAEzet7
BGlKKpQCEAAD_Nd
BGlNk-ACMAIQnCd
BGlTF1nCQAEJ5Sx
BGlTUDmCAAAtzar
BGlvUhpCEAAbSNA

MAHAKAMA YASEMA Uchaguzi Kenya ulikuwa huru na wa haki





Willy Mutunga rais wa mahakama ya juu zaidi Kenya
Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya, imeamua kuwa rais mteule Uhuru Kenyatta atasalia kuwa rais mpya wa Kenya baada ya kusema kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia huru na ya haki.
Uchaguzi wenyewe ulifanyika tarehe nne mwezi Machi, ambapo hesabu ya kura ilimpa ushindi Kenyatta kwa zaidi ya laki nane.

Rais wa mahakama hiyo jaji mkuu Willy Mutunga alisema kuwa mahakama imekubali kwa kauli moja kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia ya huru na wazi na kuwa Kenyatta na mgombea mwenza wake walichaguliwa kihalali.

Uamuzi huu una maana kuwa Uhuru Kenyatta ndiye ataapishwa kama rais mpya wa Kenya tarehe tisa mwezi ujao
Kesi hiyo iliwasilishwa katika mahakama ya juu zaidi na mpinzani mkuu wa Kenyatta, Raila Odinga baada ya uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu.


Matokeo rasmi yalionyesha kuwa Uhuru alishinda uchaguzi kwa kumpiku Raila kwa asilimia 50.07 huku Raila akipata asilimia 43.28. Matokeo haya yalizuia kufanyika kwa duuru ya pili ya uchaguzi kwa kura 8,100.


Bwana Odinga aliishutumu tume huru ya uchaguzi na mipaka kwa kuhujumu matokeo ya uchaguzi ili kumpa ushindi Uhuru Kenyatta.


Uchaguzi wa urais, wabunge na wajumbe wengine wa serikali, ulifanyika tarehe nne mwezi Machi, ukiwa wa kwanza tangu uchaguzi uliokumbwa na ghasia mwaka 2007 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya elfu moja.


Bwana Kenyatta na mgombea mwenza wake ,William Ruto,wanakabiliwa na kesi katika mahakama ya jinai kwa kuchochea ghasia za mwaka 2007. Hata hivyo wamekanusha vikali mashtaka.


Mahakama ya juu zaidi inaweza kuthibitisha ushindi wa Kenyatta au kuubatilisha uamuzi wa wakenya na hivyo kuitisha uchaguzi mpya.Vyovyote matokeo yatakavyokuwa kuna wale watakaoghadhabika mno.


Rais anayeondoka mamlakani, Mwai Kibaki amewataka wakenya kuwa watulivu na kukubali uamuzi wa mahakama lakini wengi wanatagemea sana idara ya mahakama ambayo imekuwa na mageuzi makubwa na ambayo sasa watu watu imani nayo.


Mawakili wa Odinga wanasema kuwa kesi yao ilihusisha madai ya kuhujumu hesabu ya kura pamoja na matatizo ya usajili wa wapiga kura na vile vile matatizo ya mitambo ya usajili wa wapiga kura.


Mnamo Ijumaa mahakama ya juu zaidi ilidurusu matokeo ya kura katika vituo 22 vya kupigia kura. Na pande zote mbili zilisema matokeo yalithibitisha misimamo yao.


Kenyatta ameutaja uchaguzi huo kama ishara ya kukuwa kwa demokrasia Kenya na ulifanywa kwa njia ya amani.


Tume ya uchaguzi, pia imesisitiza kuwa uchaguzi ulikuwa huru licha ya hitilafu za kimitambo....


Wachunguzi wa kimataifa nao walisema kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na kuwa tume huru ya uchaguzi uliendesha uchaguzi huo kwa uwazi.

HIZI NDO PICHA ZA MTUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRI- ZANZIBAR




 Hapo ndio tujue kuwa wenzetu hawabahatishi na hawana siasa kwenye kazi zao proffessional....kazi kweli kweli!!wamehadithiwa tu wamemchora mtu yule yule!!Angalia Mchoro wa Polisi Hapo chini na Ufananishe na mtu Huyu..


KIJANA AAMUA KUCHOMA MOTO KITAMBULISHO CHA TAIFA CHA KENYA MARA BAADA MAHAKAMA KUHALALISHA USHINDI WA KENYATTA HAPO JANA




Kijana ROBERT STEPHENE OKELLO mwenye asili ya Luo ameingia matatani mara baada ya kuamua kuchoma kitambulisho chake cha Utaifa mara baaada ya mahakama kutengua Pingamizi la Mgombea kupitia Tiketi ya  ODM bwana RAILA ODINGA kupinga Uchaguzi huo.

Kijana huyo aliamua kufanya hivyo kutokana na kile alichokiita kuwa ni Uonevu wa kisiasa na hivyo kupelekea kukichoma kitambulisho hicho ambacho kikatiba ni mali ya Jamhuri ya watu wa Kenya.

Hata hivyo Mahakama Nchini humo haijazungumza kitu chochote mpaka sasa na kuna wasi wasi mkubwa kuwa huenda pakatokea hali ya hatari zaidi kama mahakama itachukua Uamuzi wa kumtia mbaroni kiajana huyo

TASWIRA YA UOKOAJI UKIENDELEA KATIKA AJALI YA JENGO LA GHOROFA 14 LILILOPOROMOKA DAR NA KUUWA WATU KADHAA



Jengo la Ghorofa 14 lililokuwa likiendelea kujengwa pembeni kabisa mwa Msikiti wa SHIA Mtaa wa INDRA GHAND na Zanaki, limeporomoka na kusambaratika na kusababisha vifo vya watu kadhaa ambao hadi sasa idadi haijaweza kupatikana kutokana na waokoaji kukosa vifaa vya kutosha katika zoezi hilo la uokoaji. Imeelezwa kuwa ghorofa hilo limeporomoka leo asubuhi majira ya saa moja na nusu ambapo ulianza kusikika mlio kama 'Tetemeko la ardhi'.
Aidha imeelezwa kuwa katika Jengo hilo walikuwepo mafundi ambao walikuwa wakiendelea na ujenzi na chini alikuwepo Mama Lishe, aliyekuwa akiuza chai na eneo hilo pia walikuwapo watoto wadogo ambao haikuweza kufahamika idadi yao waliokuwa wakicheza eneo hilo, ambao wote inasemekana wamefukiwa na kifusi cha ghorofa hilo, huku waokoaji wakifanikiwa kumpata mtoto mmoja tu ambaye hata hivyo imeelezwa hali yake ilikuwa ni mbaya na kuwahishwa hospitali.
Ni moja ya Kifaa pekee kilichokuwepo eneo hilo Trekta, likifukua kifusi ili kuokoa watu wanaodaiwa kufukiwa na kifusi hicho.
Baadhi ya watu waliwahi kufika kujaribu kutoa msaada bila mafanikio hapa wakiwa wamekwama baada ya kukosa vifaa vya kutosha.
Wahindi nao walikuwapo kutoa msaada hapa wakilielekeza Trekta kusogea mahala walipo wao wakihisi kuwa kuna mtu mahala hapo.
Waokoaji wakijitahidi kutumia mikono kuondoa kifusi hicho ili kuweza kuwaokoa watu waliofukiwa.
Trekta likiendelea kuondoa kifusi hicho.
Waokoaji wakiwa hoi......
Juhudi zinaelekea kulala.........
Moja kati ya magari yaliyokuwa eneo hilo likiwa limeangukiwa na mabaki ya jengo hilo.
Trekta likiendelea kuondosha kifusi......../
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik, akihojiwa na wanahabari kuhusu tukio hilo.
Moja ya ghorofa lililo karibu kabisa na jengo hilo lililoanguka nalo likiendelea kujenga nalo pia likiwa na ghorofa 14.....
Sehemu ya wananchi wakishuhudia tukio hilo.
Vijana wakishusha mitungi ya gesi ili kuwasaidia kukata nondo.... baada ya kuona vimekosekana vifaa vya haraka

TASWIRA YA UOKOAJI UKIENDELEA KATIKA AJALI YA JENGO LA GHOROFA 14 LILILOPOROMOKA DAR NA KUUWA WATU KADHAA



 


Jengo la Ghorofa 14 lililokuwa likiendelea kujengwa pembeni kabisa mwa Msikiti wa SHIA Mtaa wa INDRA GHAND na Zanaki, limeporomoka na kusambaratika na kusababisha vifo vya watu kadhaa ambao hadi sasa idadi haijaweza kupatikana kutokana na waokoaji kukosa vifaa vya kutosha katika zoezi hilo la uokoaji. Imeelezwa kuwa ghorofa hilo limeporomoka leo asubuhi majira ya saa moja na nusu ambapo ulianza kusikika mlio kama 'Tetemeko la ardhi'.
Aidha imeelezwa kuwa katika Jengo hilo walikuwepo mafundi ambao walikuwa wakiendelea na ujenzi na chini alikuwepo Mama Lishe, aliyekuwa akiuza chai na eneo hilo pia walikuwapo watoto wadogo ambao haikuweza kufahamika idadi yao waliokuwa wakicheza eneo hilo, ambao wote inasemekana wamefukiwa na kifusi cha ghorofa hilo, huku waokoaji wakifanikiwa kumpata mtoto mmoja tu ambaye hata hivyo imeelezwa hali yake ilikuwa ni mbaya na kuwahishwa hospitali.
Ni moja ya Kifaa pekee kilichokuwepo eneo hilo Trekta, likifukua kifusi ili kuokoa watu wanaodaiwa kufukiwa na kifusi hicho.
Baadhi ya watu waliwahi kufika kujaribu kutoa msaada bila mafanikio hapa wakiwa wamekwama baada ya kukosa vifaa vya kutosha

BREAKING NEWSSSS!! RAIS KIKWETE AMFUTA KAZI MKUU WA MKO WA DAR ES SALAAM BAADA YA JENGO LA GOROFA KUMI NA SITA KUANGUKA.



Rais Jakaya Kikwete

Habari zilizotufikia hivi punde kutoka vyanzo vyetu vya habari, Rais Kikwete amemfukuza kazi Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar es salaam Said Meck Sadick kutokana na uzembe wa kutosimamia kikamilifu ujenzi holela ambao unafanywa na wakandarasi ambao hawana sifa jijini Dar es salaam. Uamuzi huo Rais ameutangaza usiku huu muda wa saa 6.15 leo tarehe 1/04/2013 na kuiacha nafasi yake ya ukuu wa mkoa ikikaimiwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi mpaka hapo atakapo mtangaza Mkuu wa mkoa mwingine.

Sambamba na Mkuu wa Mkoa, Rais amemsimamisha kazi Msimamizi wa Mkoa katika Idara ya Ujenzi sanifu, pamoja na maafisa wawili ambao ni wakaguzi wa majengo wakati yanapokuwa yanajengwa.

Hatua hiyo ya Rais imekuja kutokana na Jengo lenye Gorofa 16 kuanguka na kuonekana uongozi wa juu kuto kuwa na taarifa zozote juu ya ujenzi wa jengo hilo ambalo halikuzingatia vigezo ambavyo vimewekwa kwa ajili ya ujenzi huo, kimoja wapo ni kile ambacho kilitaka ujenzi huo kuishia gorofa 12 na mkandarasi kujenga mpaka gorofa 16. Mheshimiwa Rais ameagiza wale wote ambao wamehusika katika kufanya uzembe wa ujenzi huu wachukuliwe hatua stahiki kulingana na kosa husika. Mpaka hivi sasa ni maafisa kadhaa wameshakamatwa akiwemo mkandarasi ambaye alikuwa analijenga jengo hili.

Kwa kutambua leo ni Tarehe 1 mwezi wa nne tunaamini unaweza ukatambua Rais amechukua maamuzi ambayo ni sahihi ili kuweza kujenga heshima kwa watendaki wake na iwe mfano kwa wengine.
Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

1/04/ 2013

RAPPER CYRILL KID KAMIKAZI AMEFIWA NA MAMA YAKE MZAZI


Top Talent


RAPPER CYRILL KID KAMIKAZE AMEFIWA NA MAMA YAKE MZAZI MAMA JANE KITAINDA. MSIBA UPO TEGETA NYUMBANI KWAO CYRIL. TOP TALENT INATOA POLE KWA FAMILIA ,NDUGU NA MARAFIKI KWA UJUMLA.

Friday, March 29, 2013

Diamond Platinum akiwa na judges katika music video audition ya kumtafuta model ambaye ataweza kufanya video mpya ya Diamond Platinum.Zoezi ili lilifanyika katika maeneo ya Nyumbani lounge Jijini Dar es Salaam

.

Diamond hapo akielezea sababu na dhumuni zilizomfanya mpaka afanye hivyo huyu hapa anafunguka kwa dzain hii "kusema kweli nimeona umuhimu kwasababu unakuta pale msanii anapoamua labda kufanya video mpaka aanze kutafuta watu lakini mimi nikaona kwanini ni si ajili watu wa kunifanyia video zangu kama models na ndiyo maana leo hii ni siku maalum ya kumtafuta yule ambaye ataweza kufanya video mpya ya kwangu na pia kumuajili katika kazi zangu za muziki kwa hiyo pale ninapoamua kufanya video ninakuwa ninajua kabisa nina watu kadhaa wa kufanya nao video".Hayo ndiyo maneno ya Diamond wa wasafi akielezea sababu na dhumuni la kufanya Music Video Audition leo maeneo ya Nyumbani lounge jijini Dar es Salaam.
 

Rihanna - Diamonds (acoustic cover)

Mandela arudishwa hospitalini Pretoria



Mandela apelekwa hospitalini tena
Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela amepelekwa hospitalini kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.
Taarifa kutoka kwa afisa ya Rais wa Afrika Kusini zimesema kuwa uchunguzi huo ni wa kawaida tu.
Kwa muujibu wa tovuti ya Urais, Madaktari wanaomfanyia uchunguzi Mzee Mandela wamesema hakuna haja ya kuwa na taharuki yeyote.
Kwa muda mrefu sasa hali ya kiafya ya rais huyo mstaafu imekuwa ni swala la kutia wasiwasi.
Mandela mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini kwa siku 18 mwezi wa Desemba mwaka jana kutokana na kutatizwa na mapafu pamoja na vijiwe ndani ya kibofu chake cha mikojo.
Taarifa iliyoandikwa kwenye mtandao wa Ofisi ya Rais Jacob Zuma zimeeleza kuwa Mzee Mandela alipelekwa katika Hospitali ya Mjini Pretoria kwa uchunguzi wa kawaida wa ki-afya.
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na matatizo yanayoambatana na umri wake mpevu.
Mzee Mandela alihudumu kama rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 1994 hadi 1999 na ndiye rais wa kwanza mweusi kuwahi kuitawala nchi hiyo.
Kutokana na juhudi zake za kupigania demokraisa na kupambana na sera za ubaguzi wa rangi nchini humo, Mzee Mandela anatambulika kama Baba wa Taifa nchini Afrika Kusini.
Tangu mwaka 2004 Mzee Nelson Mandela amekuwa hajitokeza hadharani au kushiriki katika shughuli zozote za umma.

Rais mstaafu Mandela hospitalini tena


Rais wa zamanai wa Aafrika Kusini, Nelson Mandela amelazwa tena hospitalini baada ya kuugua tena ugonjwa wa mapafu.

BINTI ABAKWA MPAKA KUFA...ALIKUWA ANATOKA NACHINGWEA RESORT


BINTI ABAKWA MPAKA KUFA...ALIKUWA ANATOKA NACHINGWEA RESORT


Bint aliyejulikana Mariam amekutwa na mauti  baada ya kubakwa mpaka kufa....
 
Vijana hao waliokosa utu na kushindwa kumuogopa Mungu walifanya kitendo hicho mbele ya eneo la kanisa(Voda st)Nachingwea Lindi.
 
Marehemu alikuwa  na  mkasa   huo wakati akitoka Nachingwea Resort(NR) katika muziki siku ya ijumaa.Inasadikika marehemu amelewa  na wabakaji  alitoka nao muziki.

Thursday, March 28, 2013

HONGERA DINA KWA KUPATA TUZO YA WOMEN OF THE YEAR



Leo hii kupitia tuzo za Tanzania Women Of Achievement Award (TWAA), mtangazaji wa Clouds Fm, kupitia kipindi cha Leo tena, Dina Marios, amejichukulia tuzo ya "Women of the year" , katika sherehe zilizofanyika katika hoteli ya Serena, iliyoko jijini Dar es salaam.
"sikutegemea kama nitapata tuzo hii, maana kila mmoja aliekuwa karibu yangu nilimuona kama mtu mzima sana, nikasema hawa ni watu wazima sana mimi hapa sidhani kama kuna changu, ila nikajipa moyo nikasema, hawa akina mama waliopata tuzo wamefanya kazi nzuri sana mpaka kufikia hapa, lakini kabla sijamaliza nikasikia wanataja jina langu ikiwa ni tuzo ya mwisho kutolewa. huwezi kuamini hata sikumbuki nilitoa speech gani pale ila kila mtu alisifia, nimeshukuru sana" amesema Dina
all the best to you, na mungu akuzidishie


HII NDIO COVER MPYA YA SINGLE INAYOFATA YA KANYE WEST


HII NDIO COVER MPYA YA SINGLE INAYOFATA YA KANYE WEST

Top Talent
Wakati wote Kanye anapotaka kutoa album yake inakuwa kama ni event, matokeo yake vyombo vya habari na ,mashabiki wanashindwa kusubiri kujua kuhusu ujio wake mapema iwezekanavyo.
kwa bahati mbaya, matarajio yao yanapelekea kuwepo kwa nyepesi nyepesi na ripoti ambazo saa nyingine zinakuwa sio za kweli, kwanfano kumekuwa na ripoti kadhaa kuwa album ya 6 ya West itakuwa inaitwa black American physcho, mara Rich Black American, na sasa kuwa ni Iam God
kutokana na post ya The Huffington, mtu wa karibu sana na Kanye kuwa "Iam God" sio jina la tittle ya album, lakini haliko mbali na tittle ya single yake inayofata.
msanii chini ya G.O.O.D. Music,Malik Yusef amethibitisha tittle kupitia mtandao wa twitter
@teamkanyechi its “I am(A) GOD” FAMO #psalms 82
— Malik Yusef (@malikyusef) March 26, 2013
inasemekana title hiyo imetokana na passage kwenye biblia Psalms 82:6-7 ambayo inasema “I have said, Ye are Gods and all of you are children of the Most High. But ye shall die like men, and fall like one of the princes.”
tofauti ndogo ya kuongeza “a” kuifanya iwe “I Am A God” ni kutofautisha kuwa wimbo hau suggest kuwa Kanye mwenyewe ndio the Creator lakini mtu huyo huyo ananguvu ya kuwa greater being.
West amekuwa na historia ya kuhusisha idea na picha za kidini katika kazi zake. moja kati ngoma zake zilizofanya vizuri ni “Jesus Walks” kutoka kwenye album ya off The College Dropout, alitokea kwenye cover ya Rolling Stone akiwa na taji la miba ambalo huwa linaonekana kwenye picha ya yesu, cheni kubwa yenye miungu ya Egymp Horus katika video ya "Power" na "Watch the throne", No church in the wild" amegusia theme ya morality versus decadence.
mpaka sasa haijatangazwa single wala album hiyo itatoka lin

28 March 2013 0 Comments 28 March 2013 By Admin Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP Suleiman Kova akiwa maeshikilia baadhi ya vipande vya meno ya Tembo vilivyokamatwa hivi karibuni katika eneo la Kimara Wilaya ya Kinondoni. Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP Suleiman Kova akifafanua kuwa Jeshi la polisi limeweka mikakati ya mpango kazi ikiwa ni pamoja na kushirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama pamoja na kikosi cha zimamoto ili kuhakikisha kuna udhibiti wa matukio ya uhalifu au fujo. Aidha amesema jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata bunduki mbili aina tofauti, moja ikiwa ni Shotgun yenye namba AB 44736 na ya pili ni Greener yenye namba 10883 pamoja na risasi 17. Na.INaMoTO Blog Team Jeshi la polisi kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kukamata vipande vya meno ya Tembo vipatavyo 13 ambavyo thamani yake haikufahamika mara moja. Tukio hilo limetokea katika eneo la Kimara wilaya ya Kinondoni ambapo askari walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema. Pamoja na kukamatwa kwa vipande hivyo pia amekamatwa mtuhumiwa Christopher Julius mwenye umri wa miaka 18, mwanafunzi wa Kidato cha Nne – Kibaha sekondari. Katika hatua nyingine kupitia misako mikali inayoendelea Jeshi la polisi limefanikiwa kukamata noti bandia 32 za shilingi elfu 10,000/= zenye thamani ya shilingi 320,000/= za kitanzania. Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP Suleiman Kova ametoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini hasa katika kuelekea siku kuu ambapo watu wasio na nia njema wanapenyeza pesa bandia kwa nia ya kujiongezea kipato binafsi.



  • 28 March 2013
  • By 
Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP Suleiman Kova akiwa maeshikilia baadhi ya vipande vya meno ya Tembo vilivyokamatwa hivi karibuni katika eneo la Kimara Wilaya ya Kinondoni.
Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP Suleiman Kova akifafanua kuwa Jeshi la polisi limeweka mikakati ya mpango kazi ikiwa ni pamoja na kushirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama pamoja na kikosi cha zimamoto ili kuhakikisha kuna udhibiti wa matukio ya uhalifu au fujo.
Aidha amesema jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata bunduki mbili aina tofauti, moja ikiwa ni Shotgun yenye namba AB 44736 na ya pili ni Greener yenye namba 10883 pamoja na risasi 17.
Na.INaMoTO Blog Team
Jeshi la polisi kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kukamata vipande vya meno ya Tembo vipatavyo 13 ambavyo thamani yake haikufahamika mara moja. Tukio hilo limetokea katika eneo la Kimara wilaya ya Kinondoni ambapo askari walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.
Pamoja na kukamatwa kwa vipande hivyo pia amekamatwa mtuhumiwa Christopher Julius mwenye umri wa miaka 18, mwanafunzi wa Kidato cha Nne – Kibaha sekondari.
Katika hatua nyingine kupitia misako mikali inayoendelea Jeshi la polisi limefanikiwa kukamata noti bandia 32 za shilingi elfu 10,000/= zenye thamani ya shilingi 320,000/= za kitanzania.
Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP Suleiman Kova ametoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini hasa katika kuelekea siku kuu ambapo watu wasio na nia njema wanapenyeza pesa bandia kwa nia ya kujiongezea kipato binafsi.

JACK WOLPER ATWAA TAJI LA IJUMAA SEXIEST GIRL




Jacqueline Wolper (kulia), akipokea cheti cha ushindi kutoka kwa DK. Cheni aliyekuwa jaji mkuu wa shindano hilo.  Wolper akiwa ameshikiria cheti chake muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi. Dok. Cheni akiwa kwenye pozi na Wolper juu ya jukwaa. Msanii wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz akiwajibika jukwaani na mnenguaji wake.
Chidy Benz akikamua jukwaani hapo.
Omm Dipoz akizungumza na mashabiki zake jukwaani.
Dogo Asley akiwajibika.
Awali jana mchana hawa ni baadhi ya watoto wakichezeshwa ukumbini hapo.
Watoto hawa wakijiandaa kushindanishwa moja ya mchezo wa kuzungucha rigi kiunoni jana mchana ukumbini hapo.
Mmoja wa watoto waliofika Dar Live mchana akikabidhiwa baiskeli baada ya kuibuka mshindi katika mchezo wa kuruka kamba.
Mchekeshaji maarufu Mtanga, akizungumza na mmoja wa watoto ndani ya Dar Live.
Sehemu ya umati uliyojitokeza ukumbini hapo.

MSANII wa chimbo la filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe, usiku wa kuamkia leo ameibuka kidedea kwenye shindano lililokuwa likiwashirikisha mastaa wa kike Bongo la Ijumaa Sexiest Girl ndani ya Ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.

Wolper amejizolea heshima lukuki na kitita cha sh. milioni 2 ikiwemo na ofa ya kulipiwa saluni kujiremba kwa mwaka mzima. Usiku wa leo pia ndani ya ukumbi huo kulikuwa na burudani kibao kutoka kwa Ommy Dimpoz, Chidy Benz, Dogo Asley, TOT Taarab na michezo kibao ya watoto iliyosindikizwa na shindano la Mkali wa Mic.