Friday, April 5, 2013

MPENZI WANGU AKITONGOZWA HUNIAMBIA NA KU "FOWARD" MESSAGE KWANGU...JE HII NI SAWA?




 -Wadau  Naomba mnipe mwongozo kwa hili la mpenzi wangu.

 -Kuna mambo mawili yamejitokeza hv karibuni:

 - kwanza, juzi alinipigia simu[hatuko mkoa mmoja, anasoma] na katika maongezi akasema kuwa X-boy wake kampigia simu nanukuu.."eti kanipigia simu, nikamuuliza leo umekumbuka nini?....akaniambia eti anakuja huku[alipo huyu demu] mm nikamwambia nasafiri, sitakuwepo"

  -Pili, jana kaniambia "mpenzi kuna sms zinachekesha...ngoja nikuforwadie...sms 1 ilisomeka "nakuhitaji"....


Sms ya Pili ipo hivi.."leo umependezaa, nataka nije kwako"..hizi sms anadai katumiwa na mshikaji anayeonyesha kumtaka kimapenzi

MPENZI WANGU AKITONGOZWA HUNIAMBIA NA KU "FOWARD" MESSAGE KWANGU...JE HII NI SAWA?




 -Wadau  Naomba mnipe mwongozo kwa hili la mpenzi wangu.

 -Kuna mambo mawili yamejitokeza hv karibuni:

 - kwanza, juzi alinipigia simu[hatuko mkoa mmoja, anasoma] na katika maongezi akasema kuwa X-boy wake kampigia simu nanukuu.."eti kanipigia simu, nikamuuliza leo umekumbuka nini?....akaniambia eti anakuja huku[alipo huyu demu] mm nikamwambia nasafiri, sitakuwepo"

  -Pili, jana kaniambia "mpenzi kuna sms zinachekesha...ngoja nikuforwadie...sms 1 ilisomeka "nakuhitaji"....


Sms ya Pili ipo hivi.."leo umependezaa, nataka nije kwako"..hizi sms anadai katumiwa na mshikaji anayeonyesha kumtaka kimapenzi

RAY ASALIMU AMRI BAADA YA KUKUBALI KUACHANA NA FILAMU YAKE ILIYODAIWA KUWA INA UDHALILISHAJI MKUBWA




HATIMA ya filamu ya mwigizaji, Vincent Kigosi ‘Ray’, Sister Mary iliyokuwa imezuiwa kwa kudaiwa kudhalilisha ukatoliki, imefahamika kuwa mwigizaji huyo amesalimu amri ya viongozi wa kanisa hilo.

Cover la filamu hiyo ya Sister Marry.
Kanisa Katoliki nchini linaloongozwa na Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, liliizuia filamu hiyo kwa kile kilichodaiwa kuwa ilikuwa ikionesha udhalilishaji kwa namna ambavyo watawa wamevaa mavazi mafupi.
Baadhi ya vipande vilivyomo katika filamu hiyo.
Akipiga stori na mwandishi wetu, Ray amebainisha kuwa baada ya kuambiwa achomoe vipande vingi kwenye filamu hiyo, ameona ni bora kuachana nayo kwani hata akitoa haitaleta maana hivyo atakujairudia upya wakati mwingine. 

“Asilimia 85 ya filamu niliigizia kanisani na ndivyo walivyosema niviondoe, sina ujanja kwa sasa nimeanza kushuti filamu nyingine kabisa ile labda nije kuirudia upya hapo baadaye,” alisema Ray.

SHILOLE NA Q-CHILLAH WAFANYA "MAMBO YA KIKUBWA" NDANI YA NDEGE



MWANAMUZIKI wa miondoko ya mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na muimba Bongo Fleva, Abubakar Katwila ‘Q-Chillah’  hivi karibuni waliawaacha midomo wazi wasafiri ndani ya ndege kufuatia tukio lao la kufanya ‘malavidavi’ bila kujali.

 
Aibu hiyo ilitokea Machi 29, mwaka huu ambayo ilikuwa Ijumaa Kuu ambapo wasanii hao walikuwa wakitoka Dar kwenda Mwanza kwa ajili ya kufanya shoo siku ya Pasaka.

Akimsimulia mwandishi wetu, shuhuda wetu aliyekuwemo ndani ya ndege hiyo  alisema aliwaona Shilole na Q-Chillah wakiwa katika ‘mahaba’ ambapo mara kwa mara walikuwa wakipigana mabusu kitendo kilichowafanya abiria wengine kuwakodolea macho yenye kuwashangaa.
“Tunakubaliana na kazi zao, lakini kusema ule ukweli, sisi abiria wenzao tulishangaa sana, unajua kuonesha vitendo vya mahaba ndani ya ndege si utamaduni wetu Wabongo,” alisema abiria huyo aliyekuwa akienda Mwanza kikazi.

Aliongeza kuwa, ilifika mahali baadhi ya abiria walitaka kuwafungukia ukweli kwamba wanachokifanya si adabu hasa ikizingatiwa kuwa wao wana majina makubwa katika burudani za Bongo.

Kufuatia taarifa hizo na kudakwa kwa picha zao, Amani liliwasaka watuhumiwa hao kila mmoja kwa wakati wake ili kusikia kutoka kwao juu ya kufanya madudu ndani ya ‘pipa’.

 
Kwa upande wake, Shilole alisema kuwa mabusu ni vitu vya kawaida kwake ikizingatiwa Q-Chillah ni mwanamuziki mwenzake kwa hiyo hakuna tatizo.

“Jamani kwani mabusu yana shida gani, yule (Q-Chillah)  ni mwanamuziki mwenzangu na tumezoeana. Yale yalikuwa ni mambo ya kawaida tu na utani, si vinginevyo,” alisema  Shilole.

Q-Chillah simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita muda mwingi bila kupokelewa, lakini baadhi ya watu wake wa karibu walisema mwanamuziki huyo hana kawaida ya kupokea simu kama namba hazijui. 

"NALALIA PESA NA NACHAMBIA PESA"......HILI NI DONGO LA MANGE KIMAMBI AKIWA AMETAWANYA MIHELA KITANDANI


"NALALIA PESA NA NACHAMBIA PESA"......HILI NI DONGO LA MANGE KIMAMBI AKIWA AMETAWANYA MIHELA KITANDANI


Mjasiriamali na blogger maarufu nchini, Mange Kimambi amegeuka Beyonce na kuwaambia wasichana wanaohate mafanikio yake ‘Bowdown bit**es I got lots of money.’
  

Kupitia blog yake yenye wasomaji wengi hasa wanawake, Mange ambaye kwa muda mrefu anaishi nje ya nchi na kurejea hivi karibuni akiuza aina ya nguo yaitwayo Bongolicious, amepost picha hizi na kuandika:

Finally, nimemaliza mahesabu ya leo…..Ngoja niingie kulala sasa… Arusha mmetishaaaaaa, nimewapendajeeeeeeeeee. “BOW DOWN BITCHES”…SHIKAMOO DADA MANGE WILL DO…….LOL. Ps: Nimewazidishiaje hasira????? Hehehehehehe.
Mange 2
And rumor has it that this boss lady is beefing with Sintah.
Katika Moja ya comments zinasema;

“Hahaha ki bibi sintah kimenunaje sasa hahah kusema kweli sintah anajishaua tena sana kama mdogo wake sabra yan wana midomo ya kinafki sana na hawana kitu kaz kujiona matawi na wakat no money in their pocket..

khaaa hiyo mipesa yeye anaipata kwa mwaka..mxxiii..na ndo maana aliolewa Uganda na pia ana mtoto tena mkubwa kamuacha hukohuko..

hv hamjiulizi kwa nin kila xaa yuko huko…anajishaua kwa kipi sasa hicho ki gar chake kimoja hhahha watu wana magar wana change kila siku…kha eti ana kaa sinza ptyuuuu,” ameandika msomaji mmoja.
mange 3
Hata hivyo si kila mmoja aliyekifurajia kitendo hicho.

“I love you so much, I always feel like I am your big sister. Please stop this, this is not classy at all. You are not ignoring them, just leave it alone and do you. I beggo Please. Please let go and let’s just talk about bongolious. Showing off the money and matusi is so unnecessary my sister. Please let’s focus on becoming billionaires,”ameandika mwingine.

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRI MUSHI AFUTIWA MASHITAKA...DPP -ZANZIBAR ADAI KUWA HANA KOSA





Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Zanzibar, Ibrahim Mzee Ibrahim, ametupilia mbali uchunguzi wa mauaji ya Padri Evarist Mushi uliofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) na kusema mtuhumiwa hana kesi ya kujibu mahakamani.

Padri Mushi ambaye alikuwa Paroko wa Kanisa Katoliki Minara Miwili aliuawa kwa kupigwa risasi Febuari 17, mwaka huu katika eneo la Beitrasi mjini hapa akiwa ndani ya gari alipokuwa akielekea kuongoza misa ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Theresia, mjini Zanzibar.
Baada ya mauaji hayo, Rais Jakaya Kikwete alitoa kibali cha kukaribisha maafisa wa FBI kushirikiana na Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa mauaji hayo na Machi 17, mwaka huu Jeshi la Polisi lilimkamata Omar Mussa Makame kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.
Uchunguzi wa NIPASHE umebaini kuwa DPP baada ya kulipitia jalada la uchunguzi wa mauaji hayo, juzi alitoa mwongozo kwa Jeshi la Polisi kuendelea kumtafuta muuaji wa Padri Mushi.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, DPP aliliandikia barua Jeshi la Polisi na kukabidhiwa juzi ikieleza sababu za ofisi yake kutofungua hati ya mashtaka hadi sasa dhidi ya mtuhumiwa wa mauaji hayo.
Jeshi la Polisi limethibitisha kuipokea barua ya DPP ambayo inaeleza kuwa ushahidi uliokusanywa katika jalada la kesi hiyo hauna mashiko na kwamba mtuhumiwa hahusiki na mauaji hayo.
Chanzo cha habari kutoka Jeshi la Polisi kilieleza kuwa DPP hajaridhishwa na uchunguzi wote uliokusanywa dhidi ya mtuhumiwa pamoja na watuhumiwa watatu wanaotuhumiwa kwa mauaji ya askari polisi, Said Abdulrahman aliyeuawa kwa kupigwa mapanga na watu wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar Oktoba 17, mwaka jana.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, alithibitisha hatua ya DPP kutupa uchunguzi wote wa jalada la mauaji ya Padri Mushi na kuwataka waandishi wa habari kumtafuta DPP azungumzie sababu za uamuzi wake wa kutokubaliana na uchunguzi wa Polisi.
Hata hivyo, alisema kwamba Jeshi la Polisi bado linaamini uchunguzi walioufanya kwa kushirikiana na FBI hauna shaka na kwamba mtuhumiwa huyo ana kesi ya kujibu mahakamani na wataendelea kumshikilia.
Alisema kwamba kwa mujibu wa sheria, Jeshi la Polisi jukumu lake ni kuchunguza kesi na ofisi ya DPP jukumu lake ni kufungua hati ya mashtaka na kutetea kesi mahakamani.
Hata hivyo, NIPASHE ilipofika katika ofisi ya DPP, Katibu muhtasi wake alisema amepokea maagizo kutoka kwa bosi wake kuwa waandishi wote wa habari wanaofuatilia suala hilo, wamuone Kamishna wa Polisi kwa vile kazi aliyopewa ya kupitia jalada la uchunguzi kabla ya kufungua kesi ameikamilisha.
“Kamishna ndiye aliyeitisha mkutano na waandishi wa habari kuelezea hatua iliyofikiwa pamoja na kukamatwa kwa mtuhumiwa, sasa awaite tena amalizie kazi yake ya kuwaeleza hatua iliyofikiwa baada ya Mkurugenzi kurejesha jalada la mauaji,” alisema Katibu muhtasi huyo.
Katika hatua nyingine, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, Yusuph Ilembo, jana alifika katika Mahakama Kuu ya Zanzibar, kufuatia ombi lililofunguliwa mahakamani na wakili anayemtetea mtuhumiwa wa mauaji, Abdallah Juma Mohamed.
Abdallah Juma amefungua ombi katika Mahakama Kuu kwa kutumia kifungu cha sheria 390 cha sheria namba 7 ya mwenendo wa makosa ya jinai ya mwaka 2004, akitaka Jeshi la Polisi litoe maelezo kwa nini mteja wake hajafikishwa mahakamani ndani ya saa 24 tangu alipokamatwa Machi 17, mwaka huu.
Wakili Abdallah Juma akisaidiwa na mawakili Shaban Juma Bakari na Shaibu Ibrahim Shaibu waliitaka Mahakama Kuu itoe amri ya kuachiwa kwa mteja wao kutoka mikononi mwa Jeshi la Polisi. Hata hivyo, Ilembo alisema kuwa kutokana na uzito wa kesi hiyo, anaomba kupewa muda wa kutayarisha majibu ya hati ya kiapo kwa maandishi na kuuwasilisha kwa upande wa utetezi na mbele ya mahakama hiyo kabla ya ombi hilo kuanza kusikilizwa na kutolewa uamuzi.
“Tunaomba mtuhumiwa aendelee kushikiliwa na Polisi, wakati tukifanya matayarisho ya kujibu hati ya kiapo,” alisema Ilembo.
Kwa upande wake Jaji wa Mahakama Kuu, Mkusa Isaack Sepetu, alisema baada ya kusikiliza pande zote mbili, alimtaka Ilembo awe amejibu kwa maandishi hati ya kiapo ya maombi hayo kabla ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo Aprili 8, mwaka huu.
Aidha, Jaji alisema wakati wa kusikilizwa kwa shauri hilo, ametaka mtuhumiwa huyo afikishwe mahakamani, baada ya hoja za upande wa mawakili wanaomtetea kutaka dhamana kwa mteja wao, kwa vile bado hajafikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji.
Kutupwa kwa uchunguzi wa jalada la mauaji hayo pamoja na jalada la uchunguzi wa mauaji ya Polisi kunadhihirisha kuwapo kwa mvutano mkubwa baina ya Jeshi la Polisi Zanzibar na ofisi ya DPP.

"NATONGOZWA SANA FACEBOOK" ...CHUCHU HANS




Msanii wa filamu Bongo ambaye ni mke wa mtu, Chuchu Hans amefunguka kuwa  anatongozwa sana na wanaume kupitia Mtandao wa Kijamii wa Facebook, kitendo kinachomkosesha amani.

Akizungumza na mwandishi wetu, Chuchu alisema kuwa, anachojua yeye mtandao huo ni sehemu ya kukutana na marafiki na kubadilisha mawazo lakini cha ajabu kila akiingia, wanaume kibao wamekuwa wakimtaka.

“Mimi kwa kweli kila nikiingia Facebook nakutana na wanaume ambao wananitongoza, mtu anajua kabisa una mtu wako lakini bila haya anatangaza dau na kueleza kuwa, anakutaka, mijitu hii naichukia kweli,” 
alisema Chuchu

HABARI KUBWA ZA MAGAZETI APRIL 5 2013 NDIO HIZI.



.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

YUSUPH MANJI ATAJWA KWENYE ORODHA YA WATU WANAOFICHA FEDHA NJE YA NCHI




Muungano wa kimataifa wa uandishi wa habari za uchunguzi, ICIJ, umemtaja mfanyabiashara maarufu wa Tanzania, Mehbub Yusufali Manji maarufu kama Yusuf Manji kuwa ni miongoni mwa watu wanaoficha fedha nje ya nchi.
Katika ripoti hiyo, ICIJ umeandika:

Details: The Manji family is one of the richest in Tanzania. It started Quality Group Limited, the country’s major conglomerate with interests ranging from automotive to food processing.

Offshore business: Director and shareholder of Intertrade Commercial Services Inc. (2007-2009) in the British Virgin Islands.

Comment: Yusuf Manji, chairman and CEO of the company, did not reply to ICIJ’s emailed request for comment. The contact address in the records is that of the company in Dar es Salaam.

MKE WA MTU AFUMANIWA GEST AKITOA PENZI KWA RAFIKI WA MUMEWE.....




TIMBWILI la aina yake  liliibuka  hivi  karibuni   katika  nyumba  ya  kulala  wageni  maeneo  ya  Chalinze Bagamoyo kufuatia mumewe aliyefahamika  kwa  jina  la  Abuu  kumnasa  mkewe  akiliwa  uroda  na  rafiki  yake  wa  karibu  aliyefahamika  kwa  jina  la  Benard Celestin....

Tukio hilo  la  aibu  lilitokea saa 11:00 alfajiri  ya   tarehe  27  march   mwaka  huu baada  ya  mumewe  kuweka  mitego  mikali  iliyopelekea  kumnasa  live  mkewe  akipewa  mambo  na  rafiki  ya  mumewe.....

Kabla ya fumanizi hilo, mumewe  aliaga  anaenda Dar.Mkewe  alimsindikiza  mpaka  stendi  huku  akiwa  na  furaha  tele.....

Jamaa  alishukia  njiani  na  kurudi  kinyemela.....Za  mwizi  arobaini, mida ya  saa  saba  usiku,Gari  lenye rangi  nyeupe   lilitua  nyumbani  kwa  jamaa  na  kushuhudia  mkewe  akitoka  nje  na  kupanda  ndani  ya  gari  hilo.........

Mumewe  pamoja  na  kundi  zima  la  waandishi  wa Udaku-GPL walianza  kulifuatilia  mpaka  walipofanikiwa  kumnasa mwanamke  huyo  na  rafiki  wa  mumewe.....