Monday, April 22, 2013

MR. NICE AFUNGUKA KUHUSU BEEF LAKE NA WATANZANIA NA NIA YAKE YA KUOA MKENYA


Msanii mkongwe aliyekuwa amepotea kwenye chart nchini, Nice Lucas Mkenda ameendelea kutengeneza vichwa vya habari nchini Kenya baada ya jana kuhojiwa kwenye vituo vikubwa vya runinga nchini humo, Citizen TV na NTV.

Katika kituo cha Citizen, Mr Nice ambaye amesainishwa kwenye label ya Grandpa Records, alikuwa akihojiwa live kwenye muda wa taarifa ya habari ya jioni kwa lugha ya Kiswahili inayotazamwa na watu wengi nchini humo na hata Tanzania huku kwenye NTV akionekana kwenye kipindi cha comedy cha The Churchill Show. Haya ni miongoni mwa yale aliyoyaongea Citizen TV.

Kuhusu sababu za kwenda Kenya
Nilikuwa nimesimama muziki muda mrefu kama miaka minne hivi na baadaye nikakutana na kampuni ya GrandPa Records. 


Kwakweli walinifuata Dar es Salaam tukaongea maneno mengi ya busara sana kwasababu wao naona wanaona mbele zaidi. Wakaniambia Mzee ‘we umekaa kimya muda huenda ni sababu ya hasira lakini bado watu wanakuhitaji sana kwahiyo kuna vitu vingine hata kama vilikukwazwa vinaweza vikatatulika kwasababu unangojewa tu haujawa wa zamani, bado wewe ni mpya’. 


Nimekaa nyumbani 4 years lakini kaja mkenya, kanifuata kwa gharama nyingi sana na kunishawishi you must come back again! kwahiyo nasema wakenya asanteni sana kwa yote mliyonifanyia .

Kuhusu kama ana beef na watanzania

Hapana mimi sina beef na watanzania wenzangu kwasababu kwanza kazi ya muziki ni yangu sio ya watanzania na kila mtanzania ana kazi yake, kila mkenya ana kazi yake. 


Kwasababu hata kuna wakenya wanafanya kazi Tanzania wapo Tanzania na walifuatwa hapa Kenya kwenda kufanya kazi Tanzania. Nimekumbana na maswali mengi kwenye interview ‘kwanini usifanye na kampuni za Tanzania? 


Nikasema walioniona na wakaona kwamba nahitajika, ni mkenya ndio alikuja kunifuata so ningeacha kufanya naye kazi? Na akanipa faida zake.

Kuhusu wimbo wa Mack Muga wa Ali Kiba

Ali kiba ni mdogo wangu, rafiki yangu na hatujawahi kukorofishana hatujawahi kuwa na beef ya aina yoyote hata sijawahi kumsikia akinizingumzia mahali kwa ubaya. 


Haya ninayoyasema hapa , hizo ni story kichaa kwasababu nimeizunguka sana dunia kwakweli, passport yangu inatisha, unaifungua kama gazeti lakini bahati nzuri ama mbaya mimi sijawahi kufika South Africa hata siku moja na wala sijawahi kufanya hata interview na kituo chochote. 


Na hiyo nimeisikia hapa Kenya hata Tanzania sijawahi kusikia kitu kama hicho.
  
Kuhusu kuoa
Nadhani ni moja kati ya mambo yaliyonileta hapa nimekuja pia kuoa Kenya, short and clear , atapatikana na nitawaambia hayo ni mambo ya kumwachia Mungu.

BUNGE FILAMU PRODUCTION IKO MBIONI KUZINDUA FILAMU YA " WAZIRI BOYA"




BAADA ya Bendi ya Bunge Modern Taarabu kufanya uzinduzi wao wa albamu yao ya nyimbo tano iliyokuwa na jina la 'FU*K YOU'! jijini Dodoma, taasisi nyingine ya sanaa Bungeni ya Bunge Filamu Production nayo iko mbioni kuzindua filamu yao mpya ya'Waziri boya'.

Filamu hiyo iliyosheheni wasanii na watunzi mbalimbali na mahiri katika ya uigizaji inaongozwa na msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva) Joseph Mbilinyi maarufu kwa majina ya Mr II ama Sugu.

Yafuatayo ni majina ya washiriki katika filamu hiyo ....vikundi vyao vya sanaa katika mabano na utunzi wa kazi zao mbele 

-(SUGU:- Mbunge Mbeya mjini Chadema). "Mambo mengine nchi hii hayaendi kutokana na serikali pumbavu, hatuwez kuwa nawazir wa elim boya.

-(LIVINGSTONE LUSINDE:- Mbunge Mtera CCM). "Kuna wabunge ambao wana mimba zisizotarajiwa bungeni.

(JUMA NKAMIA:- Mbunge Kondoa kskz CCM). "Siongei na Mbwa bali naongea na mwenye Mbwa.

-(PETER MSIGWA:-Mbunge Iringa Mjini Chadema). "Serikali ina tatizo kwa kuwa kuna akili ndogo inatawala vichwa vikubwa.

(ANNA ABDALA:- Viti maalum CCM). "Sikufurahishwa na kauli ya Lusinde kwamba tunamimba zisizotarajiwa.

-(LETICIA NYERERE:- Viti maalum Chadema). "Kwa kuwa wanaume wengi wanabaka, kifunguliwe kituo wafundishwe kutongoza.  

-(ALLY KESI:- Mbunge Nkasi CCM). "Serikali iruhusu raia walime bangi wapate fedha za kigeni.

-(DIDAS MASABURI, Meya wa Jiji la Dar es Salaam CCM) "Baadhi ya wabunge wanafikiri kwa makalio.

LADY JAYDEE: MNAFIKI WA MIAKA 10, SHUJAA WA SIKU 30



Imeandikwa na Saleh Ally via wavuti.com

MGOGORO wa kimuziki kati ya msanii Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ na kituo kimoja cha redio umezidi kuchukua kasi huku makundi mawili, kila moja likitengeneza ngome yake na kuamini linachoamini.

Kundi ambalo linamuunga mkono Jaydee na kumuona ni mkombozi, anazungumza kwa niaba yake na wasanii wengine, la pili ni lile linalobaki upande unaoshambuliwa, linatetea ngome yake.

Jaydee anashutumu kubaniwa nyimbo zake na kituo hicho ambacho kupitia mitandao kadhaa ya kijamii ameeleza wazi kuwa wanambania, wanaziponda lakini hata watangazaji wake wamekuwa wakionyesha chuki binafsi dhidi yake.

Jaydee pia aliwaponda wasanii Ben Pol na Linah anayetokea THT kwamba walishindwa kutokea kwenye uzinduzi wa video ya wimbo wake wa Joto Hasira, kwa madai walizuiwa na bosi wao.


Ujasiri huu wa Jaydee ndiyo kitu bora ambacho kimekuwa kikitakiwa kufanyika kutoka kwa wasanii, yaani wapigane kutetea muziki wa Tanzania hasa kama kuna watu au kundi la watu limejikita katika kuuangamiza.

Lakini ni tofauti kidogo, kwani wasanii wengi wamekuwa imara na kuwa tayari kujitetea wenyewe tu na si vingine. Nasisitiza mara nyingi, wao ndiyo wahusika wa kwanza na wanapaswa kuanzisha mapinduzi kuanzia kwao, mfano kusema naonewa si kitu kibaya lakini je, umewahi kupigania wanaoonewa?

Kujitetea pekee unaweza kufanya, lakini vipi utafanikiwa kama asilimia kubwa ya kundi la wanamuziki linaendelea kuonewa. Ukibaki hauonewi pekee na asilimia kubwa ya wasanii au wanamuziki inaonewa, kunaweza kuwa na 
mapinduzi sahihi?

Ndiyo maana nashangazwa kusikia Jaydee leo anaona ubovu wa kituo hicho, anathubutu kusema hadharani akionyesha wazi ameumia.Lakini miaka 10 au zaidi iliyopita, Jaydee alikuwa kimya na hakuwaza kusema kwamba kituo hicho kinawabania wasanii wengine na ‘kumtukuza’ yeye hata kama muziki wake haukuwa wa kiwango kilichokuwa kinazungumzwa.
Siwezi kusema muziki wa Jaydee ni mbaya, nimekuwa kati ya mashabiki wake. Lakini yoyote atanichekesha akisema nyimbo albamu zake zote alizotoa zilikuwa katika kiwango cha juu sana na ndiyo maana leo ni maarufu.

Hakuna asiyejua kwamba miaka nenda rudi, wasanii wamekuwa wanaongoza kwa unafiki, kutopendana wenyewe, kugeukana na hata kujenga makundi lukuki, ndiyo maana kila kukicha wamekuwa wakishambuliwa maana katika maisha yao hawana umoja.

Jaydee alianza kuwa mtangazaji katika kituo hicho baada ya kuacha kurap, akaamua kuachana na kurap na mwisho kuwa msanii wa nyimbo za kubembeleza, mara ya kwanza akianza kutikisa na albamu ya Machozi, Solo Thang anaweza kuhadithia vizuri kuhusu hili.

Kuanzia albamu ya Machozi, kituo hicho ndicho kilisimama kuhakikisha anakuwa bora hata kama muziki wake haukuwa ukimzidi kila mwanadada wakati huo.

 Angalia, kulikuwa wasanii kama Stara Thomas, Carola Kinasha ambao kiuwezo walikuwa juu kuliko Jaydee, lakini hawakupewa nafasi ya kutosha, badala yake Jaydee ambaye hakuthubutu kuwatetea hata kidogo akaendelea ‘kubebwa’ na watu wakaamini ni bora kuliko yeyote kwa upande wa akina dada au kina mama katika kuimba, haikuwa hivyo.

Angalia albamu ya Binti, karibu nyimbo zote zilikuwa na ujumbe mmoja, ulikuwa ukimshambulia mwanaume mmoja ambaye alikuwa amemuumiza Jaydee. Takribani ujumbe wa nyimbo karibu zote ulikuwa ni mmoja, lakini ilibebwa na kuonekana ni moja ya albamu bora kabisa kuwahi kuwepo katika muziki wa Tanzania, kitu ambacho hakikuwa sahihi.

Wakati huo wasanii lukuki walilia kubaniwa, mmoja wao alikuwa ni Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye ndiye alimtambulisha mwanadada huyo alipomshirikisha katika wimbo wa Mambo ya Fedha, kabla ya hapo hakuwa na jina. 
 
Jaydee hakuwahi kuungana naye hata kidogo hata kwa mstari mmoja wa kumtetea au kuunga mkono kutetea muziki wa Tanzania, kuonyesha anapinga mwenendo wa wanaolazimisha kuwabagua wasanii au kufanya mambo kwa mabavu kwa kuwa wameshika mpini.

Hakuna aliyesikia kilio cha Sugu, wasanii wanaochipukia bila ya kujua wasemacho, kisa nyimbo zao zinapigwa redioni, ili kuonyesha shukrani za dhati wakaanza kutangaza Sugu anatapatapa na amekwisha kimuziki!

Ajabu, asilimia kubwa ya maneno yake ndiyo yanayozungumzwa leo, ndiyo yanatumiwa na kila msanii anayebanwa au kuhisi kaonewa. Angalia, hata Jaydee naye ameingia huko! Swali langu hapa je, Jaydee na wengine wanaolalamika, wamekwisha kisanii?

Ndiyo maana nasema, tasnia ya muziki hasa muziki wa kizazi kipya umejaza watu wavivu kufikiri, wenye mioyo ya ‘Kichina’, wasio na uwezo wa kuthubutu hata kidogo ambao wanasubiri wayumbe au kuumizwa wao ili wamtafute wa kumuangushia lawama.

Jiulize, kama Jaydee alibebwa kwa miaka 10, halafu leo analalamika atakuwa sahihi? Sitaki kumpinga kwa kuwa kuna kitu anakiona lakini ninaamini alikiona tokea mapema, akauchuna.

Bado nasisitiza, yeye na wengine wote wanaolia baada ya kuguswa wao nawaita wanafiki, wanapigana kwa ajili yao na si kwa muziki wanaoutumikia. Iwapo wangekuwa tayari kupambana kwa ajili ya muziki huo, msanii kama Jaydee asingeanza vita leo.

NARUDI KWA JAYDEE


Sijawahi kuingia naye katika malumbano zaidi ya miaka 10 tokea alipokuwa mwanahabari mwenzangu na sasa msanii. Lakini nathubutu kumueleza kuwa ni kati ya wasanii wasiojali muziki wa Tanzania na wanajiangalia wao zaidi.

Picha ya unafiki na kujiangalia mwenyewe inaonekana sasa ingawa takribani miaka mitano iliyopita nilianza kuinusa. Leo analia, anabaniwa na anauona moto unaounguza muziki wa Tanzania ulivyo mkali.

Naamini aliuona miaka kibao nyuma, lakini kwa kuwa alikuwa akitetewa hakuweza kuangalia kwamba rafiki zake, wasanii waliombeba kabla walikuwa wakiungua. Akaendelea kuwapita kwa raha zake mustarehe.

Tungeweza kumuita Jaydee ni mpambanaji kama angewakosoa hao anawakosoa sasa katika kipindi walichokuwa wamempa mbeleko yeye, basi kweli ingeonekana anapigania muziki wa Tanzania. Sasa anapigania chake tu!

Jaydee amefika mbali kimuziki, alikuwa bora jukwaani na nyimbo kadhaa na nyingi zikapewa ‘over promotion’ lakini bado ninaweza kumuita mkongwe. Ajabu alibaki chipukizi hadi leo katika suala la kutetea haki za wasanii na muziki wenyewe.

Sitaki kumkatisha tamaa kwa mapambano aliyoyaanza, ninaamini ana nafasi ya kuanza kuusaidia muziki ambao umemsaidia. Lakini ndiyo kipindi ambacho anaweza kupata machungu waliyopata wasanii wenzake kunyeshewa mvua na kuunguzwa na jua wakati akiwa kivulini kwa ‘msaada’.

Anachokifanya leo Jaydee ni nyongeza tu ya walichokifanya Sugu au Afande Sele au wasanii wachache walioamua kuwa wakweli au wale walioamua kuwa wabunifu kama Ambwene Yessaya ‘AY’, aliyekimbia vita ya redio na kuingia katika kurekodi video bora zilizoendelea kumng’arisha.

Simzuii, Jaydee kuendelea kupambana, lakini namuasa anachokifanya kama ni kwa ajili ya muziki akipozwa tena, asirudi nyuma.

Ninachomkumbusha, hata yeye amekuwa kundi moja na analowalaumu ambao angeweza kuwashauri mapema ‘ndani ya mjengo’ kama angekuwa na nia nzuri na muziki wa kizazi kipya.  Msisitizo ‘Joto Hasira’ liwe la kweli.

LULU MICHAEL "FAKE" ABEMBELEZA MASTAA WAMFOLLOW TWITTER




Inaonekana muigizaji wa filamu Elizabeth ‘Lulu’ Michael ameingia location kufanya filamu yake inayoaminika kuwa ya kwanza tangu atoke mahabusu mwezi January mwaka huu.

Kupitia Instagram, juzi Lulu ameshare picha inayomuonesha akiwa location na muigizaji Hashimu Kambi na kuandika, take 1 action, Mic location, me doing my thng.”

Katika hatua nyingine, Lulu amelalamika kuwepo kwa akaunti fake ya Twitter yenye jina lake iitwayo @Lulu_actress.

 “Haya lulu mwingne huyo on twitter…..!am tired jaman…nyie ma lulu nioneeni huruma basi…..!!!nimechoka kusikia case’z zenu!!!!NIMECHOKA JAMANI ,” ameandika Lulu kupitia Instagram.

beaab90cab3211e2a7d622000a9e298f_7
 

Katika akaunti hiyo Fake, mtu huyo ameandika profile yake isemayo: 

Am a bongo movie actress|caring,loving and loved lady| latest movie coming soon by the name The end of tourture| starring wil be me and jb 

Akaunti halisi ya Lulu kwenye mtandao wa Twitter ni ile yenye jina @hotlulumichael.

MPENZI WA ZAMANI WA CHRIS BROWN AAMUA KUPIGA KUTOKA NUSU UCHI KULIPIZA KISASI KWA RIHANNA




 Karrueche amepiga hizi picha siku kadhaa tu baada ya Rihanna nae kupiga picha kama hizi kwa ajili ya interview nyingine ya Jarida.

 Karrueche pia hivi karibuni amezindua Clothing line yake inayoitwa THE KILL.

PREZZO AUMBUKA BAADA YA PICHA YAKE YA UTUPU KUVUJA




Jackson Makini a.k.a. Prezzo is in trouble…..on Saturday after the release of his new and controversial track Liqher,  his n*ked photos enjoying some private time with two lasses were leaked to the internet.

Check out the first PHOTO>>>
Source:Daily post

GODBLESS LEMA AIBUKA KIDEDEA...RUFAA YA KESI YAKE IMETUPILIWA MBALI





Rufaa ya kesi ya Mbunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema imetupiliwa mbali na mahakama kumtangaza mbunge huyo kuwa ni halali.

Rufaa hiyo ilisikilizwa na majaji watatu wa Mahakama Rufaa Tanzania ambao ni Engili Kileo, Salum Massati na Benard Luanda kwa pamoja wametupilia madai ya rufaa hiyo.

Mahakama hiyo  imewaamuru tena wakata rufaa walipe gharama zote za kesi.

THE MAKING OF ‘GLASS HEWANI’ MUSIC VIDEO BY SMASHOW FT WIN





Video location was Java Lounge Seacliff Hotel Masaki.
Artists; SMASHOW FT. WINI
Song; GLASS HEWANI
Prod; SEI RECORDS
Dir; JERRY MUSHALA (Director of Jambo Jambo - Steve RnB's Hit song)

VIDEO to be released officially on 24th April 2013 on Yotube @ Jerry Mushala 
and all social medias. Stay tuned .