Thursday, May 2, 2013

BAD NEWS: WANAFUNZI WANAODAIWA KUFANYA BIASHARA YA UKAHABA CHUO KIKUU CHA UDOM HAWA HAPA



Taarifa ya habari ya Star tv ya saa mbili usiku ya tarehe 23/11/2012 imeeleza kuwa wanafunzi wa kike katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wanadaiwa kufanya biashara ya ukahaba katika maeneo mbalimbali ya starehe mjini Dodoma!

Habari hii inasikitisha hasa ukizingatia umuhimu wa wasomi hawa katika Tanzania na hatari inayoweza kuwapata kama taarifa hii ina ukweli. 
 
Kama jamii tujiulize, tatizo ni nini mpaka mtu wa level kama hiyo kuamua kuvaa vichupi na kujiuza kwenye clubs na sehemu zingine??
CHUO KIKUU cha Dodoma UDOM kinadaiwa kukumbwa na kashfa ya ngono kufuatia madai kwamba baadhi ya wananafunzi wa kike wanajihusisha na biashara ya kuuza miili yao kwa lengo la kujikimu kimaisha...
Bofya "Endelea" ucheck picha za wanazuoni wanaojiuza nighmbovu ma'clubang'ers

...tuhuma hizo zimebainika wakati wa mahafali ya tatu ya UDOM huku takribani wahitimu 6392 wakitunukiwa vyeti,stashahada,shahada za kwanza,uzamili na shahada za uzamivu. 

Chuo Kikuucha Dodoma ambacho kilianzishwa rasmi mwezi machi mwaka 2007 kimejipatia sifa kemkekm za kitaaluma licha ya ukweli kwamba bado ni kigeni machoni pa wengi. 


Tuhuma za ngono miongoni mwa wanafunzi wa kike zinadaiwa kusababishwa na ukata hatua inayowalazimu kutoroka chuoni nyakati za usiku na kujiunga na baadhi ya wasichana wa mitaani waliokubuhu kwenye ukahaba maarufu kama machangudoa kwa lengo la kujiuza. 

Wakizungumza na star tv wakati wa mahafali hayo baadhi ya wahitimu wanathibitisha uwepo wa vitendo hivyo vilivyo kinyume na maadili. 


Kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof.Idris Kikula anatoa onyo kali kwa wote watakaobainika. 


Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amenukuliwa kwa nyakati tofauti akisisitiza suala la maadili chuoni hapo hatua inayodaiwa kupuuzwa na wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Kwa wote wenye kero au Jambo lolote wapige number zifuatazo


Freeman Mbowe(Kiongozi wa Upinzani Bungeni) 0784779944, SAID A.ARFI (Mpanda Mjini) 0786/0767001122,Tundu A.M Lissu(Singida Mashariki) 0754447323, John MNYIKA(Ubungo) 0784222222, Joseph Mbilinyi(Sugu) 0716627344, Zitto Kabwe(Kigoma Kask.) 0713730256, Mch. Msigwa(Iringa mjini) 0754360996, Halima Mdee(Kawe) 0713569823, Dr. Slaa(Katibu Mkuu CHADEMA) 0784666995,
Vicent Nyerere(Musoma Mjini) 0763177737, Joshua Nassari (Arumeru Mash.) 0716807944, David Silinde(Mbozi Magh.) 0789985444, Ezekiah Wenje(Nyamagana) 0785479302. Ungana nao ktk bunge hili la Bajeti kwa kuwatumia kero au jambo lolote ambalo unaona lina maslahi kwa Taifa letu.

Magazeti ya leo Ijumaa May 03 haya Hapa. Kuna stori za siasa,michezo na udaku



...
.
.
.
.
.
.
.
..
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

MASWALI MATANO ALIYOULIZWA GADNER G KUHUSIANA NA WOSIA WA KIFO CHA LADY JAYDEE




Jana  Lady Jaydee  alitoa  wosia  akidai  kuwa  SIKU  AKIFA  RUGE  wa  CLOUDS  fm  asiguse  katika  mazishi  yake  na  Radio Clouds  Fm  isithubutu  kutangaza  wala  kutia  neno  lolote  katika  msiba  huo......

Gadner  G  ameamua  kuvunja  ukimya  na  kuufafanua  wosia  huo kupitia  TBC FM  wakati  alipohojiwa  na  mtangazaji  Dan Chibo  katika  kipindi  cha  
The Takeover na  haya  ndo  mazungumzo  yao...
------------------------------------
Leo nilipata nafasi ya kuzingumza na Gadan G Habash ambaye ni Meneja na Mume wa Mwanamuziki maarufu nchin Lady Jay Dee, sote tunafahamu juu ya maneno aliyoyasema Lady Jay Dee kama ni Wosia wake.

Kupitia kipindi cha The Takeover kinachorushwa na kituo cha TBC fm haya ndio yalikuwa majibu ya maswali niliyomuuliza Gada G; 
Ipi ni Kauli yako juu ya Wosia wa Lady Jay Dee...?

Gadna G: Ni maneno ambayo yametoka moyoni mwake na ni maneno mbayo anajitetea kama msanii, mimi kama Meneja ukiacha pia kama mke wangu naendelea kumsapot kwa kile ambacho anaona ni sawa, basi mimi nitaendelea kumsaport na kujaribu kuzungumza na Lady Jay Dee, mara nyingi anasema tu kwamba watu wasifikilie ni swala la wimbo kupigwa au kutokupigwa, hayo ni mambo ya kawaida lakini wafikirie tu kwamba huyu mtu anaongea kutokana experience yake aliyokuwa nayo na wale watu.
Baada ya mwaka 2003 kuacha kufanya kazi kwenye management yao ya Smooth Vibe, yalitokea mambo mengi hapa katikati ila hakusema lakini siku za hivi siku za karibuni kuna mengine ambayo yametokea, ndio akaona hapana nisipo sema nitazidi kukandamizwa na matokeo yake nitakufa kisabuni.

Hii ni kama vita mmejipangaje..?

Gadna G: Unapoamua kusema ukweli swala la kujipanga mara mbili huwa halipo, ni kwamba unasema ukweli watu wasikie naukizungumzia uhasama watu watauliza juu ya uhasama lakini ulikuwepo tayari kwahiyo tu watu wanajua kwa sasa kwa kuwa jdee ameamuwa kuongea lakini tu hawajui tu kwamba jdee alikuwa na matatizo na wale watu tangu kipindi cha nyuma sababu wale watu wanafumo dume ya kufanya kazi na alipoachananao aliona kama wanamfatilia kulekule ambapo yeye alipo

Nini mlikiona kama chokochoko...?

Gadna G: Unajua kwa mfano unaweza kumuomba mtu maji akakwambia sina, ukayaona yale pale ukamwambia niuzie akakuuzia ila bado alivyokuuzia akaona kama unafaidi, mwisho akakwambia yameisha nenda sehemu nyingine, ukaenda sehemu nyingine na ukayapata bure, akaona umepata akaamua kukufata kulekule na akakukuta unakunywa maji kwenye grasi kisha akakuputa, sasa hapo inabidi useme hapa unavyofanya sio sawa ndo hicho anachofanya Jay Dee sasa hivi.

Hali hii imewaathiri kwa kiasi gani...?

Gadna G: Cha kushukuru Mungu ni kwamba msanii au hata pia stesheni ya redio inategamea umma wa Watanzania au hata mashabiki kwa ujumla kwa kuwepo kwake.
 
Jay Dee anapata saport nzuri kutoka Watanzania, basi ujue hata hajaathirika chochote, na pia tu anaendelea kufanya kazi kwa bidii, ila tu isipokuwa unapoona mtu anafanya madhara ili tu mtu apate athari fulani ndio unasimama kuongea, ndiyo maana tuna Bunge na watu wanasimama, watu wanaongea, watu wanatetea hoja, ndiyo maana yake. Yani lazima mtu usimame useme ukweli kwa unalohisi hili jambo litanipa madhara nisiposema.


Kwa Wasanii wengine unawaambiaje...?
Gadna G: Uwoga ni kitu ambacho binadamu tumeumbiwa, wakati mwingine unasaidia wakati mwingine unakudhiru uwoga wako,kwa sababu wanasema adui wa maendeleo yako mwenyewe ni wewe mwenyewe, ndiyo maana uwoga wako unaeza ukasabishwa ukakandamizwa zaidi, ndiyo maana wazee wetu waliweza kusimama na kuikomboa hii nchi kwa sababu walisimama hawakuogopa. 
Wangeogopa hii leo hii nchi tusingekuwa huru, kwa hiyo kama kuna mtu ana jambo na anaogopa kusema hilo ni jambo la kawaida kuogopa, lakini wakati wa kusema ukifika usiogope kusema ili mradi useme ukweli, basi inatosha....
Kauli yako ya mwisho ni ipi..?

Gadna G: Ni kwamba wanahitaji kujua ukweli na kuambiwa ukweli, mtu yoyote anayejua kitu cha kweli anaweza kusema sio sawa, utaendelea kukandamizwa. Kauli ya mwisho ndo hiyo wanahitaji kuambiwa ukweli na kusikia ukweli ili kama wanakosea wasiendelee kukosea wabadilikee….

50 CENT AMFANANISHA RICK ROSSY NA MWANAMKE......USHAHIDI WA PICHA



Wote tunafahamu kuwa hakuna maelewano mazuri kati ya rapper 50 Cent na boss wa MayBach Rick Ross, leo kupitia Instagram kaweka picha ya Rick Ross akiwa na P.Diddy ambayo ukiitazama kwa haraka haraka  inaweza kukupa tafsiri tofauti kidogo, na kisha akaandika caption 'Good Morning Girl. love is in the air". Itazame hapa

NEEMA KWA WALIOFELI FORM 4:..MARKS ZAO ZITAPANGWA UPYA



TUME ya kuchunguza sababu za kufeli kwa kiasi kikubwa kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliofanya mitihani ya kuhitimu mwaka 2012 imekamilisha kazi yake na taarifa za uhakika zilizolifia gazeti hili zinasema , upangaji alama zao utafanyika upya.


Kama ambavyo gazeti hili lilivyobaini katika uchunguzi wake wa kiuandishi kwamba kulifanyika mabadiliko ya utoaji alama kwa ajili ya mitihani waliyofanya wanafunzi mwaka huo (2012) bila maandalizi kwa wadau, tume hiyo imependekeza alama zipitiwe upya (regrading).


Katika alama za awali, alama D anapoyopewa mtahiniwa baada ya mtihani wake kusahihishwa ilikuwa ni kuanzia alama 21 kwenda mbele na F ilikuwa 20 kushuka chini lakini katika mabadiliko yaliyoleta ‘maafa’ ya kufeli kwa watahiniwa wa mwaka jana, alama D ilianzia 35 na kuendelea, wakati ile ya kufeli (F) ilianzia alama 34 kushuka chini.


Vyanzo mbalimbali vya habari vimeeleza ya kwamba Jumatatu wiki hii, Baraza la Mawaziri lilikutana mjini Dodoma na kujadili, pamoja na mambo mengine, uamuzi wa kurejea upangaji alama za mitihani hiyo ya wanafunzi iliyosahihiswa kwa kutumia alama za juu (yaani kufeli ni kuanzia alama 34 badala ya 20).


“Baraza limeafikiana na ripoti kwamba upangaji alama ufanyike kwa vigezo vya zamani kwa sababu uamuzi wa kutumia alama mpya ulifanyika bila maandalizi ya kutosha, ikiwa ni pamoja na kutowapa muda wa kutosha wadau.


“Mitihani ya shule na kikanda ilikuwa ikiandaliwa na kusahihishwa kwa alama za zamani, kumbe kulikuwa na alama mpya zimewekwa kitaifa, kwa hiyo kuna uzembe ulifanyika wa kuwafahamisha wadau kwa wakati,” kinaeleza chanzo kimoja cha habari.


Katika uchunguzi wake, Raia Mwema lilibaini kasoro kadhaa zilizochangia kufeli kwa idadi kubwa ya wanafunzi katika mitihani ya kidato cha nne mwaka 2012 na kati ya kasoro hizo ni kutumia alama mpya za kupanga matokeo badala ya alama za zamani, bila kufanyika kwa maandalizi ya kutosha. 


Kutokana na kufeli huko, Februari mwaka huu, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliunda tume ili kuchunguza sababu za kufeli kwa wanafunzi wengi waliohitimu kidato cha nne mwaka 2012. Katika matokeo hayo ya kidato cha nne 2012, asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kuhitimu walipata daraja sifuri.


Tume hiyo ilihusisha baadhi ya wadau wakiwamo kutoka shule na vyuo binafsi vya elimu, Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (Tahossa), asasi zisizo za kiserikali (NGOs) zinazojishughulisha na masuala ya elimu.

KIINGEREZA CHAMUUMBUA DIAMOND...MASHABIKI WAMPA MAKAVU





Katika pitapita  instagram kuna picha ya msanii Diamond Platnumz alipost (hiyo hapo juu), na hapo wakatokea watu kukosoa kingereza alichotumia huku wengine wakionekana kutetea. JAMANI ENGLISH si Lugha yetu jamani. angalia hapa chini


LIL WAYNE AZIDIWA NA KULAZWA TENA





Lil’ Wayne amelazwa tena hospitali kutokana na kushambuliwa na kifafa. Kulazwa kwake kumekuja wiki kadhaa baada ya kulazwa tena kwa tatizo kama hilo.



Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Wayne alipekwa hospitali ya Cedars-Sinai juzi usiku na walinzi wake ambako alitibiwa na kutolewa jana.

HUSANA IDD NA NAOMI WA BONGO MOVIE WAGOMBEA PENZI LA JANUARY




Msanii anayechipukia kwenye soko la filamu na muziki, Naomi Mbaga ameibuka na kumuonya Husna Idd ‘Sajent’ amuachie bwana wake, January.
 Akizungumza na mwandishi wetu, Naomi aliweka bayana kuwa January ambaye ni Mwanamuziki wa Bendi ya Victoria ni mpenzi wake wa muda mrefu hivyo alishangazwa kuona habari mitandaoni kuwa Sajent amejituliza kwa mpenzi wake huyo baada ya kumwagana na mzazi mwenzake, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’.

“Aniachie bwana wangu, kama ameachika kwa huyo Chaz Baba atafute bwana mwingine na siyo wa kwangu. Ole wake nimkute naye siku, atanitambua,” alisema Naomi.

"TANZANIA NI MUHIMU KULIKO CHADEMA.....SIPO TAYARI KUSUSIA MCHAKATO WA KATIBA".....HAYA NI MAJIBU YA PROFESA BEREGU KWA DR SLAA




Raia Mwema:
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Mwesiga Beregu, amekataa kata kata wito wa chama chake wa kumtaka ajotoe ndani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba,huku yeye akiweka msimamo wake wazi kwamba Tanzania ni muhimu zaidi kwake kuliko chama chake hicho.

Habari zilizoppatikana na kuthibitishwa Profesa Baregu, zinasema katibu Mkuu wa chama hicho Dk Wilbroad Slaa, alimwiita msomi ambae ni mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, akimtaka ajitoe. Ndani ya Tume hiyo kwasababu za kisiasa kwa madai kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeuteka mchakato huo.

Profesa Beregu anaelezwa kumjibu Dk Slaa kwa kutumia maneno ya kiingereza, "If I am told to choose between my country and my party (Chadema), I will choose my country", akiwa na maana kwamba kama angetakiwa kuchagua kimoja kati ya nchi yake na chama chake cha Chadema, angechagua nchi yake kwanza.

Akizungumza na Raia Mwema juzi Jumatatu jijini Dar es Salaam, Profesa Baregu amekiri kutoa msimamo huo Katibu Mkuu wake Dk Slaa, pamoja na chama chake cha Chadema, akisema viongozi wenzake hao wanapaswa kujishauri mara mbili mbili kabla ya kuchukua uamuzi huo wa kujitoa ikizingatiwa. Kwamba tangu mwanzo chama hicho ndicho kilichoasisi suala zima la Tanzania kuwa na Katiba Mpya tofauti na hii ya sasa.

Itakumbukwa kwamba Chadema, kupitia kwa Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, wakati akiwasilisha hotuba mbadala ya kambi rasmi ya upinzani kwa Ofisi ya Waziri mkuu, alitangaza kujitoa katika mchakato wa mabadiliko ya katiba akitaja sababu kadhaa, zikiwamo za mchakato mzima huo kutekwa na CCM na lakini pia kwamba wajumbe wa Tume hiyo hawana weledi wa kutosha kufanya kazi hiyo.

"Ni kweli niliitwa na katibu Mkuu (Dk Slaa), akaniambia Kamati Kuu ya chama chetu imeazimia kwamba chama hakiridhishwi na mchakato mzima wa kutunga Katiba mpya, na kwa hiyo akaniambia chama kimeagiza nijitoe ndani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Akaniambia Kamati Kuu imeamua mambo mawili; kwanza kijitoe na pili, kikishajitoa kianzishe kampeni ya nchi nzima kuwahamasisha wananchi nao wasusie mchakato huo"anasema Profesa Baregu katika mahojiano maalum na Raia mwema.

Anasema aliomba kujulishwa rasmi maamuzi hayo ya CC kwa maandishi, ili ajue atachukua uamuzi ganilakini hadi anafanya mahojiano na Raia mwema hakuwa amepata majibu huku akisema kwamba kwa maoni yake kama kweli yalikua ni maamuzi ya kikao, basi Kamati Kuu itakuwa ilifanya makosa kufikia uamuzi wa kujitoa bila kumshirikisha.

"Kwanini? Mimi tangu mwanzo kaabisa sikuona kama suala hili la kuandikwa kwa Katiba mpya ni suala la mapambano kwa sababu kubwa moja kwamba Chadema ndiyo mwasisi wa mabadiliko haya ya katiba. Mimi nilikuwa Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2010 na nilishiriki kuandika ilani ya uchaguzi, na hili la kutaka Katiba mpya lilikuwemo ndani ya Ilani yetu.

Wakati ule wenzetu (CCM) waliweka msimamo wao wakisema hakuna sababu ya kuwa na katiba mpya, iliyopo inatosha,lakini baadae Serikali ikaona ipo haja ya kuwa na katiba mpya inayokidhi mahitaji ya sasa na yajayo. Muswada ukapelekwa Bungeni, wabunge wa upinzani wakasusa na kutoka nje. Chadema tukapewa fursa ya kwenda Ikulu kuonana na Rais kwa siku mbili mfululizo na karibu mapendekezo yetu yote yakakubaliwa."

"Muswada ukarudishwa Bungeni upya, sheria ikafaniwa marekebisho na kukubalika na wabunge wa kambi ya upinzani. Sasa leo hii, wabunge wale wale waliokubali, wanataka kukataa mchakato wa katiba unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria waliyoipitisha wao wenyewe....kwa maoni yangu, hadi sasa sijaona matatizo ya mchakato., yawe ya maandishi au ya malengo ya kisheria. Kama ningekuwa nimeona tatizo nisingekuwa humu, ningejitoa, Tunatengeneza Katiba yetu Watanzania wote, si Katiba ya Chama fulani...

"Lakini pia, chadema tulipokutana na Rais (Jakaya Kikwete), alitushauri na tukakubaliana naye, twende hatua kwa hatu. Itungwe sheria yenyewe kwanza, halafu iundwe tume, baada ya hapo mambo mengine yaendelee kujadiliwa...(Angu wakati huo hadi sasa nadhani sisikama Tumetunafanya vizuri ikilinganishwa na wenzetu wa huko nje walioandika upya Katiba yao.

"Mchakato unaofuata sasa ni wa kuundwa kwa bunge Maalumu la katiba, hatua hii nayo Wananchi wanetakiwa wajiandae kutoa maoni yao juu ua muundo wa. Bunge hilo. Ushauri wangu kwa Chadema., naomba chama chetu kikae mkao wa kujenga nchi yetu, si. Mkao wa kuibomoam Kama Chama tukae na Watanzania kujenga Katiba yetu mpya kwa ajili ya Watanzania na Tanzania yetu hii kwasababu fursa hii haitakuja tena karibuni labda baada ya miaka 50 ijayo....kuzira, kujitoa, nasema Watanzania hawatatuelewa"

Kaifafanua msimamo wake alioutoa kwa Dk Slaa kwamba kama angeambiwa achague kati ya ncchi yake na chama chake, angechagua nchi kwanza, Profesa Baregu anasema "Ndio, chama kinaundwa kinapita, lakini Tanzania kama nchi itaendelea kuwepo daima. Ushauri wangu kwa Chadema ni kwambakwa kuwa sisi tulishajiweka katika kusimamia mchakato wa Katiba mpya, tusijiharibie kwa kuvuruga mchakato huu"

Akizungumzia kauli ya Mbowe katika hotuba yake bungeni kwamba Tume ya Mabadiliko ya Katiba haina watu weledi, Profesa Baregu anasema "Sisemi katika hili Chadema imekurupuka, nasema ijishauri upya, sijui ni weledi wa aina gani wanaousema, lakini naamini Tume yaMabadiliko ya Katiba imejaa watu weledi watupu, imejaa watu waadilifu na wasiokuwa na matope yeyote...,ndiyo maana tangu iundwe, hakuna Mtanzania yeyote ambae ameiita Tume hii kwamba ni genge jingine la mafisadi.

"Sitaki kuwasemea wajumbe wanzangu juu ya weledi wao, lakini mimi mwenyewe tu mbali na elimu yangu, lakini pia nimetumika katika Tume ya Month Ibrahim inayotathimini utawala bora wa marais wa Afrika kwa muhula mmoja, mtu huwezi huwezi kuwa katika tume hiyo kama huna weledi wa kutosha"

Dk Slaa alipotafutwa jana Jumanne,ili pamoja na mambo mengine alezee hatua hiyo ya Profesa Baregu kukataa kujiuzulu akiweka wazi kwamba hadi sasa hajaona tatizo lolote kubwa ndani ya Tume hiyo linaloweza kumshawishi akubaliane na msimamo wa chama chake, na msisitizo wake huo wa kuweka maslahi ya nchi kwanza mbele kuliko chama chake alisema "Saa hizi niko kwenye kikao, pole baba"

USHAURI: DADA YANGU ANA " JINSIA MBILI " NA NIMEZISHUHUDIA KWA MACHO YANGU





Habari  ndugu  zangu
 Naombeni  ushauri  wenu  kuhusu tatizo  la  dada yangu wa tumbo moja ambalo sikuwahi kulihisi, kulidhani wala kulijua kwa zaidi ya miaka 20. Kifupi mimi ni kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 23 ( Natimiza miaka 24 mwezi Juni mwaka huu ). Kwa sasa ninasoma mwaka wa mwisho katika chuo kikuu kimoja hapa nchini  .

Kwetu tumezaliwa watatu dada zangu wawili, wa kwanza alizaliwa miaka ya sabini ( R.I.P ) na huyu wa pili ambaye ndie point of discussion, alizaliwa mwanzoni kabisa mwa miaka ya 1980. 



Ngoja niende moja kwa moja kwenye point, siku ya jumamosi iliyopita ( tarehe 27 APRILI 2013 ) saa nne kamili za asubuhi nilienda kumtembelea dada yangu ( hana mume, mtoto wala sijawahi kusikia chochote kuhusu kuwa na rafiki wa kiume yaani boyfriend )...


Nilienda pale kwa ajili ya kupiga mzinga kidogo na nilipanga kurudi hosteli ambako ninaishi siku iliyokuwa inafuata yani jumapili. 

Mida ya saa sita mchana, aliwasili mdada mmoja ambaye ninamjua kama rafiki wa karibu wa dada yangu, tulisalimia kisha dada akaja kumpokea mgeni wake kisha wakaelekea ukumbini, baadaye nikarudi zangu chumbani kwangu na kuendelea kucheza na laptop yangu.



 Yalipita kama masaa mawili hivi mdada mwingine aliwasili nyumbani na kuingia moja kwa moja chumbani kwa dadangu .Sikujua kilichokuwa kinaendelea maana wakati huo nilikuwa chumbani, ila nilikuja kujua baadaye kwamba kuna mdada mwingine alikuja nyumbani pale . 

Nilikuja kustushwa baadaye na kelele za ugomvi mkubwa sana, zikitoka chumbani kwa dada yangu ambako nilisikia kelele, na matusi mazito yakiporomoshwa, vilio na chupa zikivunjwa vunjwa hovyo, sikuwa na jinsi nikaamua kukimbilia upande kilipo chumba cha dada yangu kutoa msaada. 



Kufika sikuamini kilicho tokea, nilimkuta dada yangu na yule dada mwingine ambaye nilikuwa namjua kama rafiki yake wakiwa kama walivyo zaliwa, wamelewa wanagombana na huyu mdada mwingine aliyekuja wakati mimi nimo ndani, huyu dada mwingine alikuwa anamshambulia yule dada aliyekuja mara ya kwanza na dada yangu alikuwa anajaribu kumzuia.. 

Kilicho nishangaza zaidi kuhusu dada yangu ni kwamba ana u*me ( tena mkubwa tu kama u*me wa mwanaume rijali,  na umevalishwa kinga ), mwanzoni nilidhani labda amevaa midoli lakini haikuwa hivyo, nii u*me kabisa...


Nilicho kifanya ni kumtoa yule dada aliyekuja mwishoni hadi nje kisha nikarudi zangu chumbani kwangu.... 

Sikufanikiwa kuongea na dada yangu usiku huo hadi kesho yake lakini sikuongea chochote kuhusu kilicho tokea jana yake .Japokuwa  aliniomba radhi kwa kilicho tokea lakini hatukuzungumzia kabisa kuhusu suala la yeye kuwa na jinsia mbili..


Kusema ukweli suala hili linanikosesha sana raha na sijui  nini  cha  kufanya.Nimepanga  kutoongea   na yoyote wala sitawauliza wazazi wangu lakini picha hii nitakaa nayo kwa muda mrefu sana, simuoni tena dada yangu kama nilivyo kuwa naumona hapo zamani.. 

Naombeni  ushauri  wenu .
Majidai  

Magazeti ya leo Alhamisi May 02 haya hapa. kuna stori za siasa,michezo,udaku na Burudani. Enjoy



DSC 0009 8849dDSC 0001 bc82f
DSC 0002 77a6b
DSC 0003 2124b
DSC 0004 217ed
DSC 0005 0924a

DSC 0006 dc4dd
DSC 0007 662f7
DSC 0008 452f5
DSC 0010 60055
DSC 0011 6de79
DSC 0012 f7d04
DSC 0013 0844b
DSC 0014 c49bcDSC 0015 041f9
DSC 0016 ce4ec