Sunday, May 12, 2013

MAMA AMCHOMA MOTO MTOTO WA WIFI YAKE SEHEMU ZA SIRI KWA KOSA LA KUNYWA UJI WA MTOTO




ELIZABETH Bureko (26), mkazi wa Kata ya Nyamatare, Manispaa ya Musoma, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Musoma, kwa tuhuma za kumchoma na moto sehemu za siri mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minane.
 


Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Baraka Maganga, ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Sajini Stephano Mgaya, kuwa mwanamke huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 24 mwaka huu, saa 3 asubuhi.

Kwa mujibu wa mwendesha mashitaka huyo, mshitakiwa alikiuka kifungu cha sheria namba 169 cha mwenendo wa makosa ya jinai kama sheria hiyo ilivyofanyiwa marekebisho na kuwa namba 16, mwaka 2002.

Alidai kwamba, mshitakiwa huyo alimchoma katika sehemu zake za siri na mdomoni baada ya kumtuhumu mtoto huyo wa wifi yake, kwamba alikuwa akinywa uji wa mtoto aliyekuwa akimnywesha.
Mshitakiwa alikana shitaka na kurudishwa mahabusu hadi Mei 25 mwaka huu, kesi yake itakapotajwa tena

NGONO ZEMBE ILIVYOKITHIRI BARABARA YA KUELEKEA ZAMBIA



 makahaba-ngono-zembe

Licha ya kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya Ukimwi, Mkoa wa Mbeya bado unatajwa kuwa eneo lililokithiri kwa vitendo vya ngono bila kuwa na tahadhari (ngono zembe).

Sababu kubwa ya hali hiyo inaelezwa kuwa ni kuwepo kwa maegesho ya malori ya mizigo yanayoelekea Zambia huku madereva wake wakitajwa kuwa wateja wakubwa wa ngono.


Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi  katika maeneo yanayotajwa kwa biashara ya ngono yaani Kata ya Igawa na Igurusi, umethibitisha kuwepo kwa vitendo hivyo.  

Igawa
Akizungumza na mwandishi wetu, mmoja wa madereva wa taxi eneo la Igawa aliyejitambulisha kwa jina la Felix, alisema kuwa kwa sasa biashara hiyo imedorora kwa sababu madereva wa malori wamepunguza kusimama hapo.  


“Zamani ungefika hapa saa hizi ungewakuta barabarani kabisa. Lakini siku hizi, malori yameacha kusimama hapa, ndiyo maana nao wamepungua. Lakini wapo baadhi yao ni wahudumu wa baa,” alisema dereva huyo.

Kwa kuwa muda ulikuwa umekwenda na usafiri usiku ni wa shida, mwandishi aliendelea Kata ya Igurusi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Igurusi

Ni majira ya saa mbili usiku, baada ya kuchukua chumba kwenye nyumba ya wageni iliyo mbali na barabara kuu, nikarudi kwenye baa moja. Kabla sijaondoka, nikamuuliza mama mwenye gesti kama naweza kuleta mwanamke wa kulala naye. Akanijibu kuwa ni uamuzi wangu kwani haizuiwi.

Nilipofika katika baa moja iliyo pembeni mwa barabara (jina linahifadhiwa) nilikuwa nikipata kinywaji huku nikiangalia jinsi ya kumpata mtu wa kuzungumza naye kwa kina.
Namjaribu mhudumu mmoja wa baa hiyo kwa kumtongoza, lakini akasema hawezi kutoka na mimi kwa kuwa bado yuko kazini.


Nahamia baa nyingine ng’ambo ya barabara kwa lengo hilohilo. Hapo nakutana na mama mmoja wa makamo, kisha kumweleza shida yangu kwamba natafuta mwanamke wa kulala naye usiku huo.

“Ni kweli hapa wapo kina dada, ukiwataka mnaelewana tu. Mimi mwenyewe ninaye binti yangu ila nimetuma dukani, labda umsubiri. Lakini kama unaona utachelewa, basi nenda baa ya jirani hapo wapo wengi tu,” alisema mama huyo.

Nikaamua kwenda kwenye baa hiyo jirani na hapo nawakuta kina dada wapatao watano, huku wateja wakiwa wachache tu. Nikaagiza soda na kuanza kuinywa taratibu. 


Bila kupoteza muda nikamuuliza dada aliyeniletea soda (jina linahifadhiwa)  kama naweza kupata mshichana wa kulala naye usiku huo. Mahojiano yetu yakawa hivi
 

Mhudumu: Hapa wapo wengi tu… wote unaowaona hapa ndiyo kazi zao, sijui unamtaka nani?
Mwandishi: Mimi nakutaka wewe..