Monday, June 3, 2013

KILICHOJIRI MBEYA LEO,SHULE YAUZWA NA MAHAKAMA WANAFUNZI WAKIWA NDANI..WATOLEWA VITU NJE


 Hii ndiyo Shule ya Msingi ya Besta Sae Mbeya.
  
 Vibarua waliopewa jukumu la kuhamisha mizigo shuleni hapo
 Viti  vikiwa vimetolewa eneo la shule ya Msingi Besta
 Gari la mizigo likichukua mizigo kuelekea eneo Jengine
 Waliopewa Dhamana ya kuchukua mizigo wakiwa  wanaingia ndani kwa nguvu kutoa vitu katika shule hiyo ya Besta
 Wanafunzi wa Shule ya Besta wakiwa Hawaelewi cha kufanya wakati mizigo yao aikichukuliwa

 Mmiliki wa Kampuni ya Ulinzi  ya Retired Army Bwana Kubaja akiimarisha ulinzi baada ya kupewa jukumu la kulinda shule hiyo na Wamiriki wapya.
 Kipande cha Shule ya Besta
 Polisi wakiwa na watu waliopewa dhamana ya kutoa vitu Besta wakiwa wanaendelea kutoa vitu hivyo
 Baadhi ya vitu ambavyo vilitolewa nje ya Shule ya Besta
Vijana waliopewa Dhamana ya kutoa vitu vya Shuleni hapo wakitoa Magari nje ya Shule hiyo
 Msikiti ambao upo ndani ya shule ya Msingi Besta ambao pia wananchi wa Jirani wanatumia , nao pia umenunuliwa kwa Amri ya Mahakama
 Wanafunzi wa Shule ya Msngi ya Besta wakiwa Bado hawajui cha kufannya

 Wanafunzi wa Shule ya Msingi wa Besta wakiwa wanakusanya Madftari yake pamoja na Mitihani yao.

 Mmiriki wa Shule ya Besta Ndugu Hamis Othnman akimsihi Askari ampe nakala ya kuondolewa kwake Shuleni Hapo.
  Mmiriki wa Shule ya Besta Ndugu Hamis Othnman akikataliwa na Askari hoja yake yakupewa nakala ya kuondolewa kwake na kutakiwa kumuona Mkuu wa kituo cha Polisi kati au Kumuona msajili wa Mahakama Kuu


***************
Na Ezekiel Kamanga
Mahakama kupitia dalali wa Mahakama imepiga mnada Shule ya Msingi Besta iliyopo Sae jijini Mbeya kutokana na madai ya mdai katika kesi hiyo .
Mdai wa kesi hiyo namba 212 ya mwaka 2003 ni Kampuni ya Mohamed Enterprises ambapo alikuwa anamdai Hamis Othman kiasi cha Shilingi Milioni 270 ambazo alishindwa kulipa . Kesi hiyo namba 27 ilianza kusikilizwa mwaka 2003 huku Othman  akitetewaa na Wakili Mkumbe ambapo hukumu ilitolewa 4.6.2012  majengo ya shule yauzwe, mpaka sasa madai hayo  hayaja jurikana yalikuwa yanahusiana na nini.
Wamiliki wapya wa majengo  hayo ni Mbeya Heritage Company ambao walikabidhiwa majengo hayo na Dalali wa Mahakama Chini ya usimamizi wa mtendji kata ya Ilomba Erasto Mwakapoma  na Mwenyekiti waa Mtaa wa Sae Erias Mwakyusa huku  Jeshi la Polisi Likishuhudia makabidhiano hayoyakifanyika kwa amani.
Zoezi lilisitishwa kwenye Msikiti kutokana na Imani waumini wa Msikiti huo wataalifiwe ili ndani ya siku Mbili wawe wameondoka eneo hilo. 
Adha kubwa ilikuwa ni kwa wanafunzi wliokuwepo shuleni hapo ambapo mitihani yao ilioekana kuzagaa hovyo kutokana  na purukushani zilizo kuwepo bila taarifa yoyote na kutojua Hatma yao  ya masomo yao kutokana na Madarasa kuhodhiwa  na mmiliki mwengine Licha ya kuwepo kwa mabweni kando ya Shule hiyo na kufanya mizigo yote kulundikwa nje ya mabweni.

KAMATI YA NGWEA YAKUSANYA MILIONI 32....MAMA MZAZI APANDWA NA PRESHA BAADA YA MWILI WA NGWEA KUZUIWA HUKO AFRIKA KUSINI



KAMATI ya Mazishi ya aliyekuwa Msanii wa Bongo Fleva, Albert Mangwea ‘Ngwea’, mpaka jana mchana ilikuwa imekusanya jumla ya Sh milioni 32 kutoka kwa wadau mbalimbali.

Kamati hiyo inahitaji Sh milioni 50 kwa ajili ya kusaidia kusafirisha mwili wa marehemu kutoka Afrika Kusini mpaka Morogoro kwa ajili ya mazishi. Fedha hizo pia zinahitajika kwa ajili ya kuratibu shughuli nzima ya mazishi.

Mangwea alifariki dunia Jumanne iliyopita nchini Afrika Kusini akiwa usingizini kwa madai ya kuzidisha matumizi ya madawa ya kulevya. 

Alitarajiwa kuwasili nchini jana lakini kushindwa kutoka kwa ripoti ya uchunguzi wa madaktari kwa wakati, kumesababisha isijulikane atatua lini, licha ya kudaiwa kuwa anaweza kutua leo.

Kamati ya Mazishi bado inaendelea na mchakato wa kuratibu shughuli hiyo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mwandishi wetu akiwa Mbezi Goig jijini Dar ambako ndiko kwenye msiba huo, mmoja wa waweka hazina wa kamati hiyo, Paul Matthysse ‘P-Funk’, alisema mpaka sasa kamati yake imefikisha Sh 32,259,000 ingawa wanatarajia kuendelea kupokea michango mbalimbali kutoka kwa wadau.

Miongoni mwa watu wa kwanza kutoa michango yao katika msiba huo ni P-Funk aliyetoa Sh milioni tano, Clouds Media Group (Sh milioni tano) na Push Mobile (Sh milioni tano). 

Juzi Kampuni ya Global Publishers ilitoa Sh milioni moja.
“Nawasisitiza Watanzania waendelee kutoa michango yao kwa ndugu yao ili kuonyesha umoja tulionao. Fedha zikiwa nyingi tunataka kumfanyia kitu mama yake ili kuendelea kumfariji kwani kipindi hiki ni kigumu kwake,” alisema P-Funk.
 

Wakati huohuo jana  taarifa zilisema mama mzazi wa Mangwea aishie Morogoro, Denisia Mangwea, alipandwa na presha baada ya jana kupata taarifa kuwa mwili wa mwanaye umezuiwa Afrika Kusini kutokana na uchunguzi wa madawa ya kulevya. Alikimbizwa hospitali na inadaiwa anaendelea vizuri.

Mangwea aliwahi kutamba na nyimbo kadhaa kali zikiwemo Gheto Langu, She Got a Gwan, Mikasi na Tupo Juu.

LADY JAYDEE NA T.I.D WASAMEHEANA BAADA YA KUZINGUANA KISA SHOW YA JIDE



Wakati mwingine matatizo hukutanisha watu waliokosana na kuufufua tena urafiki wao. Harakati za maandalizi ya mazishi ya marehemu Albert Mangwea zimewakutanisha marafiki wawili walioingia kwenye tofauti hivi karibuni, Lady Jaydee na TID.

Hivi karibuni TID alitangaza kujitoa kwenye show ya miaka 13 ya Jaydee na kuweka sababu tatu. Kutokana na uamuzi huo wa TID, watu walimchukulia kama msaliti kwa Jide aka Anaconda waliyewahi kufanya hit ya pamoja, Understanding.

Hata hivyo Jaydee amesema alikutana na TID kwenye kamati ya mazishi ya Mangwea na kuweka tofauti zao pembeni.


“I met TID kwenye kikao cha msiba wa Ngwair. I love him, forgive him, he’s ma frnd ana matatizo yake pia but not naniliu,” ametweet Jide.

BIG BROTHER: MSHIRIKI WA TANZANIA APEWA KAZI YA KUTEMBELEA MIGUU NA MIKONO KWA MUDA WA SIKU TANO



SHINDANO la Big Brother Afrika limeendelea kwa washiriki wawili kutolewa katika wiki ya kwanza ya mchezo huo ambao unashirikisha washiriki wapatao 28 kutoka nchi 14 barani Afrika.

 Jumatatu iliyopita washiriki walipata nafasi ya kutoa mapendekezo yao ya kuchagua washiriki ambao wanaona wanafaa kuingia katika Danger Zone ambapo watano kati yao ndio waliotajwa mara nyingi zaidi na washiriki wenzao hivyo kuingia huko. 

Washiriki waliongia katika Danger Zone walikuwa ni Betty wa Ethiopia, Selly wa Ghana, Denzel wa Uganda, Natasha wa Malawi na Huddah wa Kenya ambapowatazamaji walitakiwa kumpigia kura mshiriki ambaye wanaona anafaa kubakia ndani ya jumba hilo. 

Katika kura zilizopigwa na watazamani kutoka nchi 14, Betty ndio alipata kura nyingi zaidi baada ya kupata kura 5, akifuatiwa na Selly na Natasha waliopata kura tatu kila mmoja huku Denzel na Huddah wao wakiambulia kura mbili hivyo kumaanisha kwamba safari yao katika kugombea dola 300,000 kuishia hapo.
 
 Baada ya kutolewa katika jumba hilo IK mtangazaji wa kipindi hichoaliwapa nafasi washiriki hao kulipa kisasi kwa kuchagua mshiriki mmoja ambaye hupewa kazi ambayo hutakiwa kuifanya kwa muda atakaopangiwa.
 
Wa kwanza alikuwa Denzel ambaye alitakiwa kuchagua mshiriki ambaye atatakiwa kila akitoka nje kupunga hewa kwenye jumba hilo awe anatembea kwa miguu na mikono kwa muda wa siku tano na kijana huyo hakusita kumchagua Nando mshiriki wa Tanzania kufanya kazi hiyo. 
 
Aliyefuata alikuwa na Huddah ambaye yeye aliambia achague mshiriki ambaye atakuwa akitandika vitanda vyote katika jumba hilo kwa muda wa siku mbili na mwanadada huyo mrembo kutoka Kenya alimtaja mwanadada mwenzake Dillish kutoka Namibia kufanya zoezi hilo. 
 
Shindani hilo linaendela tena leo ambapo washiriki watatakiwa tena kupendekeza majina ya washiriki ambao wataingia katika Danger Zone kwa ajili ya kupigiwa na mashabiki ambapo atakayepata kura chache ataliacha Jumba hilo Jumapili ijayo.
pro24

COCACOLA WAMNUNULIA GARI JIPYA DIAMOND

COCACOLA WAMNUNULIA GARI JIPYA DIAMOND


Ukikutana na Diamond mtaani akiwa na mchuma mpya wenye rangi nyeusi, usishtuke sana, jua ni courtesy of Cocacola.
16859d0ccbab11e29f3f22000a1f978e_7
Inavyoonekana ni kuwa Cocaboy kama anavyojiita siku hizi, amenunuliwa gari jipya na wadhamini wake kampuni ya vichwaji ya Cocacola.

“Ya all ready know what it’s….. tukutane Fuel station!! #CocaCola Mumetishaaaaaa,” aliandika jana kwenye picha ya Instagram ya gari hilo likiwa na maganda yake.
 
“Chatin infront of my Small baby… on @channeloafrica interview at my clib,” aliongeza.

Siku nzima ya jana, hitmaker huyo wa Kesho alikuwa busy kwenye interview na kituo cha runinga cha Channel O.
af471706cb8211e2896422000a1fb003_7