Saturday, March 2, 2013

Ommy Dimpoz Ft Vanessa Mdee - Me and You ( Official Video )



Polisi mbaroni kwa mauaji



Maafisa wanane wa Polisi nchini Afrika Kusini wamekamatwa kuhusiana na kifo cha dereva taxi, ambaye anadaiwa kuburuzwa nyuma ya gari la polisi.
Uchunguzi ulianzishwa kufuatia kutolewa kwa picha ya video, iliyomuonyesha mwanaume mmoja akiwa amefungiwa pingu kwenye gari na kisha kuanza kubururwa katika barabara ya Daveyton, mashariki mwa mji wa Johannesburg.
Mtu huyo ametajwa kuwa ni Mido Macia, raia wa Msumbiji mwenye umri wa miaka 27, ambaye alifariki baadae akiwa katika kizuizini mwa polisi.
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameliita tukio hilo kuwa la kutisha kabisa na lisilokubalika huku taafifa zikisema takriban maafisa wanane watafikishwa mahakamani Machi 4, 2013 kuhusiana na tuk