Friday, April 12, 2013

HII NDO RIPOTI YA UBOVU WA MATOKEO KIDATO CHA NNE ILIYOKUWA IMEFICHWA



Ni Ripoti ya utafiti iliyokuwa commissioned na ofisi ya Waziri Mkuu kuchunguza matokeo mabaya ya Kidato cha Nne mwaka 2010 ambayo ilitoka mwaka 2011.

- Ajabu ni kwamba ripoti hii haikufanyiwa kazi na mwaka huu Ofisi hiyohiyo ya Waziri Mkuu imeunda kamati nyingine kuchunguza tatizo hilohilo!
 Sijui tunaelekea wapi?

Watanzania, bila kujali tofauti zetu kisiasa tusikubali mambo kama haya. Ni kuchezea raslimali zetu na hatari kwa vizazi vyetu na mustakbali wa Taifa letu.

Man Stuck Inside After Getting Caught with Someone's Wife

PETTY FT. GODZILLA & STEVE RnB - NAUMIA MOYO (OFFICIAL VIDEO) Canon T2i ...

HIVI NDIVYO AMBAVYO MSANII SHAA ANGEVUA NGUO HADHARANI NA KUBAKIZA KIVAZI CHA KUOGELEA TU




April 8, Shaa alitweet, “Lava Lava Video imefikisha views 44,000+ leo ikifikisha 100,000 naenda kuogelea coco beach mchana kweupe lets do.

 Hata hivyo hits 100,000 hazikufika. Lakini mchoraji Maarufu, Dennis aka Kapwipwi ameamua kutuonesha jinsi muonekano wa Shaa ungekuwa iwapo hits hizo zingefika na kutimiza ahadi yake.

HIZI NDO SABABU KUU ZA WANAWAKE WENGI KUVAA NUSU UCHI




Wakati mwingne wanaume au watu tofauti hudhani kwamba, wanawake wanaovaa nusu uchi huwa wanafanya hivyo kwa sababu ya kutafuta soko kwa wanaume.
 
 Inawezekana kukawa na wale ambao wana sababu hizo, lakini wapo wale ambao wanalipa fidia kutokana na kuamini kwao kwamba wanamapungufu kwa mfano sura zao zimewaangusha, hivyo miguu yao mizuri inabidi kuziba pengo au udhaifu huo. 
 
Wakati mwingine hata wanawake wanaodhani au kudhaniwa kuwa ni wazuri, wamekuwa wakivaa nguo fupi zinazoonyesha maungo yao.Hawa nao ni lazima wanalipa fidia ya kasoro fulani waliyo nayo.
 
 Inawezekana wameshindwa kulinda ndoa zao, au inawezekana hawajaolewa na sasa wanataka kuonyesha kwamba, pamoja na kutoolewa kwao, bado wao wana sura na miguu au miili mizuri.



Udhaifu wowote ambao unamkera mwanamke iwe ni wa moja kwa moja au kupitia nyuma ya ubongo wake, unaweza kuonyeshwa kwa mwanamke huyo kuyatangaza yale maeneo ya mwili wake ambayo anaamini ni mazuri. 
 
Kuyatangaza huko humpa ahueni kwa kuamini kwamba bado anayo thamani, kwani ataangaliwa sana na wanaume, kusifiwa na pengine kutongozwa. 
Hebu angalia wanawake ambao wanavaa nguo za kubana huku wakiwa na makalio makubwa. Hawa mara nyingi wana sura ambazo wao au wengi huamini kwamba ni mbaya. 
 
Huvaa nguo hizi ili kuonyesha kwamba, pamoja na ubaya wa sura zao, bado wao ni wazuri sana katika maeneo mengine ya mwili ambayo wanaume na hata wanawake wengi huyapenda au kutamani kuwa nayo. 

Wengi hawavai tu nguo hizi za kubana kwa sababu ni fasheni, la hasha, wengi hili ni kimbilio la udhaifu wao

TATIZO LA ELIMU TANZANIA SIYO VIBOKO.....BORESHENI MIUNDO MBINU KWANZA BADALA YA KUFIKIRIA KUTEMBEZA VIBOKO



Taifa liko katika wakati mgumu juu mustakabali wa sekta ya elimu kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili.  Kuna mengi yanazungumzwa, yamependekezwa na mengine bado yanaendelea kutolewa juu ya njia sahihi ya kukoa elimu ya watu wa taifa hili.

Kuna hoja zinatolewa kwamba sekta ya elimu imeachwa kuporomoka hadi kufikia hali mbaya ya sasa kutokana na kuminywa kwa bajeti ya sekta hiyo, matokeo yake ni janga la kufeli kwa wananfunzi wengi katika mitihani yao kama ilivyodhihirika kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliomaliza elimu ya sekondari mwaka jana kwa zaidi ya asilimia 60 kupata daraja sifuri.

Ukiacha suala la kufeli, kuna hoja za kweli na zenye mashiko zinazojengwa kwamba wanafunzi wengi wanaomaliza viwango mbalimbali vya elimu, kuanzia msingi, sekondari hadi vyuo vya elimu ya juu, hawafanani na matarajio ya watu kwa kuwa na uwezo wa kielimu kwa waliopita kwenye ngazi hizo za elimu.
Wapo wanafunzi wanamaliza darasa la saba bila kujua kusoma wala kuandika, lakini wanafaulu mtihani wa kuendelea na elimu ya sekondari; wapo wanaomaliza sekondari, lakini hawawezi hata kuandika sentensi moja iliyonyooka.

Kuna mgogoro mkubwa sana wa mitalaa ya elimu, mgorogo huu umejadiliwa kwa mapana yake na wadau wa elimu, ulifikishwa bungeni, lakini serikali kwa kutumia mlango wa nyuma iliikimbiza hoja hiyo kutoka bungeni kabla ya kupata mjadala wa kina ili ufumbuzi upatikane kwa nia ya kuokoa elimu ya nchi hii.

Katika harakati hizi na kizunguzungu katika sekta ya elimu, Waziri Mkuu ameunda Tume kuchunguza chanzo cha anguko kubwa la elimu kutokana na taifa kushtushwa na matokeo mabaya ya kidato cha nne kuliko mengine yote ambayo yamepata kuikumba nchi hii tangu uhuru.

Wakati hali ya elimu ikiwa katika mkanganyiko mkubwa, juzi Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, aliibuka na kusema kuna mpango wa kurudisha viboko pamoja na kupiga marufuku wanafunzi kumiliki simu shuleni kama njia ya kuokoa sekta ya elimu nchini.

Alisema hayo jijini Dar es Salaam katika hafla ya utambulisho wa tovuti ya www.shuledirect.co.tz ambayo
imeanzishwa na aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2004, Faraja Kotta, huku akisisitiza kuwa wanafunzi wasipopigwa viboko, mambo hayaendi, ndiyo maana mwanafunzi anaingia darasani saa tatu yaani muda anaoutaka yeye, lakini anaachwa tu bila kuadhibiwa, matokeo yake wakifeli wizara inalaumiwa.

Inawezekana Mulugo ana hoja, kwamba maisha ya binadamu bila utaratibu na makubaliano yanayojenga wajibu mambo hayaendi, kwa maana hiyo kuibua hoja ya kucharaza wanafunzi fimbo, kunaweza kutajwa kuwa ni sehemu mojawapo muhimu ya kujenga uwajibikaji kwa wanafunzi katika kutimiza wajibu wao. Hili linawezekana na linajadilika.

Naibu Waziri huyu hapana shaka anasukumwa na uzoefu wa alikotoka, kwamba zamani wanafunzi walikuwa wanacharazwa viboko ndiyo maana walikuwa na nidhamu, walikuwa wanasoma kwa bidii, walifaulu vizuri na kwa maana hiyo taifa halikuwa na aibu kama hii ya kufeli kwa wanafunzi kwa kiwango hicho.

Pamoja na hoja ya Naibu Waziri kuwa na msimamo huo, fimbo pekee hazikwezi kupandisha ubora wa elimu, fimbo haziwezi kuokoa elimu kama tabia ya nchi hii kuhusu uwekezaji finyu katika sekta ya elimu itaendelea kuwa kama ilivyo sasa.

Kabla ya serikali kufikiria habari ya fimbo tungefarijika kama ingetambua kuwa ina kazi nzito na ngumu kufanya katika kurejesha sekta ya elimu katika mstari wake.

Hali ya shule nyingi ni duni mno, hakuna walimu, hakuna vifaa vya mafunzo, walimu hawana motisha yoyote ya maana, ujira wao ni wa kijungu jiko mazingira ya kazi kama nyumba za kuishi hazipo, heshima kwa walimu kutoka kwa serikali yao na hata kwa jamii hakuna kabisa.

Kwa miaka mingi serikali imekuwa inaahirisha matatizo ya sekta ya elimu, malalamiko ya walimu yamepuuza kwa kitambo kirefu sasa, shule nyingi za umma zimegeuka kuwa mahame, siyo mahali panapompa mwanafunzi motisha ya kusoma na kujifunza kwa bidii.

Viongozi wengi ambao wamepewa jukumu la kusimamia sekta ya elimu wamegeuka kuwa waigizaji badala ya kuyakabili matatizo ya elimu kisayansi. Kwa kifupi hali ni mbaya katika sekta ya elimu.


Ni kwa kuangazi haya tunaamini kabla ya Mulugo kuanza kuzungumzia habari ya kurejesha viboko shuleni, angeangazia kwanza matatizo ya kumsingi ya sekta hii.

Wenzetu waliopiga hatua ni marufuku hata kumfokea mwanfanzi achilia mbali kucharazwa bakora, viwango vyao vya elimu viko juu. Shule nyingi za binafsi haziruhusu viboko hapa nchini, viwango vya ufaulu katika shule hizo uko juu mno kulinganisha na za umma ambako pamoja na bakora kuwa ruksa kwa utashi wa mwalimu, ziko chini kwa ubora.

Ni hali hii tunawaomba viongozi wa sekta ya elimu wajaribu kusumbua vichwa vyao zaidi kupata majibu ya maana kuhusu changamoto za elimu nchini.

VIDEO YA DAYNA NYANGE NA KALA JEREMIAH WAKIWA CHUMBANI SINGIDA YAVUJA NA KULETA BALAA



MSANII wa vichekesho nchini, Mussa Kitale, amewafanyia umafia wasanii wawili wa muziki, Kala Jeremia na Mwanaisha Said Dayna, baada ya kuwalaza chumba kimoja na kitanda kimoja akiwaambia eti anawafundisha namna ya kucheza filamu.
 
Picha zilizovuja za Dayna na Kala Jeremia wakiwa mkoani Singida
Hata hivyo, baada ya kufanikiwa kuwapiga picha, alisambaza krip hiyo kwenye baadhi ya mitandao ambapo ilianza kutoa hisia tofauti kwa wadau wa sanaa, wakiamini kuwa wawili hao walikuwa wakifanya ngono katika chumba hicho.

Katika mtandao wa Youtube, watu wengi walikuwa wakiporomosha matusi wakisema kuwa wasanii hao wanataka kutumia ngono kama mbeleko yao ya kuwabeba kisanaa.

Dayna alipoulizwa juu ya tukio hilo la kulala chumba kimoja na Kala Jeremia mkoani Singida, alisema kuwa hawapo kwenye uhusiano wa kimapenzi, ila Kitale anaandaa filamu ambayo wao watakuwapo kwenye kazi hiyo ya aina yake.

“Ni kweli nasikia mengi mtaani na wengine wanatukana wakisema eti sisi ni wahuni au tupo kwenye mapenzi, ingawa ukweli ni kuwa tupo kwenye filamu zaidi.
“Mimi ni msanii, hivyo kuambiwa nicheze filamu kwangu ni kwepesi zaidi, ndio maana naomba wadau na mashabiki wangu waelewe kuwa sipo kwenye mapenzi na Kala,” alisema.

Hata hivyo Dayna hakuweza wazi ni filamu gani anayocheza na Kala, huku akisema kuwa mwenye uwezo wa kuizungumzia zaidi ni muandaaji mwenyewe Kitale.

WEMA WEPETU AMFIKISHA POLISI MAMA YAKE BAADA YA KUMFANYIA VURUGU NYUMBANI




NI kivumbi! Kuna madai kwamba, staa wa Bongo asiyechuja, Wema Sepetu amemfikisha mama yake, Miriam Sepetu kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar kwa madai ya kwenda nyumbani kwake na kufanya vurugu zilizosababisha kuharibika kwa samani mbalimbali...

Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu hiyo ilijiri usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, jijini Dar.


Mbali na mama mtu, wengine waliofikishwa kituoni hapo ni dada mkubwa wa Wema aitwaye Nuru na kijana aliyefahamika kwa jina moja la Bestizo ambaye inasemekana ni mshirika mkubwa wa Diamond kwenye masuala ya mtandao wa msanii huyo.


“Wema alikuwa nyumbani kwake usiku huo, watuhumiwa hao wakamzukia na kuanza kumchapa makofi ya ‘kelbu’ ambapo katika mshikemshike huo, baadhi ya vitu vilivunjika na kumtia hasara staa huyo,” kilisema chanzo.


Haikujulikana mara moja ni kitu gani kilisababisha mama mzazi huyo, dada mtu na kijana asiyekuwa ndugu kwenda kwa Wema na kutenda kosa hilo.


Wema alikwenda polisi na kuandikisha maelezo ambayo yameingizwa kwenye jalada lenye kumbukumbu; KJN/RB/2755/2013 SHAMBULIO, KUHARIBU MALI.

MZEE CHILO AWACHANA LAIVU WASANII WANAOVAA NUSU UCHI




STAA wa filamu za Kibongo, Ahmed Uloto ‘Mzee Chilo’ amewachana wasanii wa filamu wanaovaa nusu uchi huku akieleza kuwa, kufanya hivyo ni kuiabisha tasnia ya fimlamu Bongo.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Mzee Chilo alisema amekuwa kwenye tasnia hiyo kwa muda mrefu sana na kuwashudia wasanii kama vile Suzan Lewis ‘Natasha’ na mama Mjata wakiigiza filamu zao kiheshima lakini siku hizi anashangazwa na uvaaji unaokiuka maadili, si kwenye filamu tu bali hata kwenye maisha yao ya kila siku.

“Mbona kuna hawa wakongwe ambao wanaigiza vizuri na kufikisha ujumbe bila kuvaa nusu uchi? Kwa kweli hali sasa hivi ni mbaya na wasanii hasa wa kike wanatakiwa kujirekebisha wanapokuwa wanaigiza na hata kwenye maisha yao ya kawaida,” alisema Mzee Chilo.

MWANAUME AKIKWAMBIA USIPENDE PESA ZAKE NA BADALA YAKE UMPENDE YEYE HUYO NI MUONGO"....ANGELITA GODWIN


"


Angelita  ni  binti  anayeamini  kuwa  mapenzi  bila  pesa  hayapo  hapa  duniani......

Anadai  kuwa  mwanaume  akimwambia  asipende  pesa  zake  huyo  ni  mdanganyifu  na  hafai  kumili  mwanamke  yeyote  yule.....

Hii  ni  kauli yake  niliyokutana  nayo  facebook 




Angelita Jennifer Godwin
"mmmh!!if i were a boy,nisingetaka mwanamke anaenipenda mimi kama nilivyo,ningetaka apende hela zangu ili nizidi kuzitafuta,na ukweli hamna mwanamke anaempenda mwanaume kama alivyo we all looking for someting,...

Sasa huo usemi wa kuambiana usipende pesa zangu nipende mimi sijui unatokea wapi,acheni kudanganywa jamni ukimpata mwanaume anakwambia nipende mimi na si pesa zangu my dear run.............

coz huyo kaplan kufa maskini au muoga wa maisha....u suppse 2 love them both!!!!!!"

AIBU: MKE WA MTU ANASWA LIVE AKIFANYA MAPENZI NDANI YA GARI MAENEO YA MWENGE-DAR





KUFUATIA vitendo vya usaliti wa ndoa, uasherati, ufuska na ukiukwaji wa maadili ya Kitanzania kwa wanandoa, wiki iliyopita Ijumaa iliendelea na Operesheni Fichua Maovu kwa kuzunguka jijini Dar usiku wa manane na kunasa tukio la mke wa mtu akifanya uzinzi ndani ya gari.


Kabla ya kufanya operesheni hiyo, waandishi  walitaarifiwa kwamba Wilaya ya Kinondoni jijini Dar ndiyo inayoongoza kwa wake na waume  za watu kufanya vitendo vya ngono kwenye magari.



Maeneo yaliyodaiwa kwamba wazinzi hao hupenda kuyatumia ni Coco Beach, Leaders Club, Mlimani City na sehemu kubwa ya vitongoji vya Sinza na Mwenge, Dar.

Mbali na waume na wake za watu, wengine wanaotajwa kufanya vitendo vya ngono ndani ya magari ni mastaa wakubwa ambao wanaogopa kwenda kukodi vyumba mahotelini na gesti wakihofia watajulikana kutokana na umaarufu wao.

 Jumatatu ya Aprili Mosi, mwaka huu, waandishi wetu walianza mchakato wa kutembelea vitongoji walivyoezwa kwamba, watu hususan wake na waume za watu hupenda kuvitumia kufanyia ufuska.


Waandishi wetu walitinga kwenye Ufukwe wa Coco uliopo Oysterbay, Dar ambako walishuhudia wasichana wengi waliokuwa wakifanya biashara ya kujiuza ‘machangudoa’ katika viunga hivyo.



Mbali na wasichana hao, pia kulikuwa na vibaka wengi waliokuwa wakiwalinda machangudoa hao ili wasipate matatizo.

Pia, wanaume wengi walikuwa wakifika na wanawake ndani ya magari yao na kupozi kwenye maegesho, wengi wao hawakuonekana kama ni watu na wake zao.

 Hata hivyo, waandishi walibaini kwamba magari mengi yanayotumiwa katika eneo hilo ni yale yenye vyoo vyeusi ‘tinted’ hivyo ni vigumu kujua kinachoendelea ndani yake.

Kwa ujanja, waandishi wetu walibaini kwamba ‘pea’ nyingine zilikuwa zikifanya vitendo vya ‘kudendeka’ na wengine kufika mbali zaidi lakini walishindwa kuwavaa kutokana na usalama mdogo katika eneo hilo.


Waandishi  wetu walihamishia mtego wake Leaders Club, Kinondoni mida ya saa 8:05, baada ya kupiga misele ya hapa na waandishi walifanikiwa kumbamba mmoja wa wazinzi.

Waandishi walitulia baada ya kuliona gari aina ya Toyota Land Cruiser  likiwa katika eneo la maficho nje ya viwanja hivyo.

Gari hilo lilikuwa likitikisika kuonesha kwamba mchezo ulikuwa ukiendelea ndani yake.

Wakati waandishi wakijipanga kulivamia, ghafla waliokuwa ndani walishtuka na kupozi kwa muda.

Hata walipoachiwa ili waendelee, machale yaliwacheza na kuwasha gari kisha kuondoka kwa kasi.


Pamoja na kulikosakosa tukio hilo, waandishi hawakukata tamaa, kuanzia Jumatatu hadi Jumapili waliendelea na utaratibu wa kutembelea viwanja husika.


Jumapili iliyopita baada ya kutembelea viwanja vyote kusaka ‘wahalifu hao’, hatimaye mtego ulinasa.


‘Patroo’ ikiwa kazini maeneo ya Mwenge, Dar jirani kabisa na hoteli moja inayopata umaarufu mkubwa siku za hivi karibu, ghafla gari aina ya Toyota Corona likiwa limepaki kwenye eneo la giza, chini ya mti lilikuwa likitikisika kuonesha kwamba kulikuwa na watu waliokuwa wakifanya ngono.

Safari hii, bila kufanya makosa, waandishi wetu waliwasogelea ambapo na wao hawakuonekana kujali wapita njia....

Credit: GPL-Ijumaa 

UNYAMA: BINTI ANYONGWA KWA KUTUMIA SURUALI YAKE




Tukio hili la kikatili limetokea huko Brazil (Cuiaba public square). Inasemekana kuwa binti huyo mwenye miaka 22 aliuawa na watu kisha wakamning'iniza kwa kutumia suruali yake aina ya jeans ili ionekane kama alijinyonga.

Wazazi wa binti huyo wanamshuku 'x-boyfriend' wake kuwa muhusika wa tukio hilo kwani hawakua na maelewano baina yao siku kadhaa kabla ya tukio.

TAZAMA KILICHOANDIKWA NA MAGAZETI YA LEO APRIL 11 2013 KURASA ZA MWANZO NA MWISHO




.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.