Saturday, June 1, 2013

FACEBOOK WAMEKUJA NA "VERIFIED ACCOUNT " NA RAIS UHURU AWA WA KWANZA.


Facebook imefuata mkondo Twitter kwa kuanzisha akaunti na kurasa zilizothibitishwa (verified pages/accounts) ili kuwawezesha watu mashughuli kuthibitisha akaunti akaunti na fan page zao. Facebook wamesema wamefanya hivyo ili kusaidia watumiaji wa Facebook kuzitambua akaunti za kweli za mastaa na watu wengine mashughuli wanaotumia mtandao huo, pia ikiwemo biashara zenye majina makubwa.

Kurasa zilizothibitishwa zitakua na alama ya blue ya pata “check-mark” kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu. Watu wataoruhusiwa kutumia huduma hiyo ni, viongozi wa serikali, waandishi wa habari maarufu, makampuni au bidhaa maarufu. Hivyo kuanzia sasa, utaweza kufahamu akaunti/pages zipi ni za kweli na zipi ni feki.

Ili mtu mashughuli kupata akaunti iliyohakikishwa, mhusika atahitaji kuwasilisha kitambulisho halali kinachotambuliwa kiserikali. Nadhani celebrities (mastaa) Wengi wa Afrika wataipenda hii. Kama mfano Wema, kuna page zaidi ya kumi zinazodai kuwa ni “Wema Sepetu”

WANYARWANDA WANASWA LIVE WAKIJIUZA JIJINI DAR



POLISI Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam imeendesha oparesheni maalum ya kuwanasa machangudoa wanaofanya biashara hiyo haramu katika eneo lao na kufanikiwa kuwaweka ‘mtu kati’ makahaba kibao, wakiwemo raia wa Rwanda na Burundi...

Kamatakamata hiyo ilichukua nafasi usiku mnene wa Alhamisi ya Mei 23, mwaka huu kwenye danguro kubwa la makahaba lililopo Kariakoo, jijini Dar ambalo machangu hao hutegea mingo zao kwa ajili ya kuwanasa wateja.

Katika hali iliyowashangaza polisi, midume iliyokutwa na makahaba hao ilitimua mbio ili kujiokoa na mtego huo wa polisi uliodhamiria kusafisha eneo la Kariakoo kwa ukahaba uliopitiliza.


Baadhi ya wanaume wakati wakitimua mbio walisikika wakisema kuwa wakukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola ni wanawake hao kwa vile wanavaa kimitego huku wakijua binadamu anapitiwa na shetani wakati wowote.

“Sisi kosa letu nini? Wakamateni haohao machangudoa, watavaaje kimitego mbele yetu sisi wanaume? Shetani naye atakuwa wapi wakati huo?” alisikika akisema mmoja wa wanaume hao huku akichanganya miguu kupita kawaida.
 
Awali kabla ya zoezi la kuwanasa makahaba hao halijaanza, afande mmoja alipowauliza wanachofanya hapo, kahaba mmoja aliuliza: Una maswali mengi kwani we ni polisi?

Mei 24, mwaka huu, makahaba hao walipandishwa kwenye Mahakama ya Jiji na kusomewa mashitaka yao na mwendesha mashitaka, John Kijumbe mbele ya Hakimu Timoth Lyoni.

Waliosomewa mashitaka ni Natasha Bahati, 30 (Mrundi), Asma Athuman, 23 (Mrundi), Niyonkuru  Evelinde, 29 (Mnyarwanda), Zaimana Hawa, 20 (Mrundi) na Wabongo 35.
 
Wote walikana mashitaka lakini walipelekwa Gereza la Segerea, jijini Dar baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

WAUMINI WAUKIMBIA MSIKITI WA DODOMA BAADA YA KAULI YA MBUNGE KUDAI KUWA UNAFUNDISHA UGAIDI


Kauli iliyotolewa na mbunge wa kilindi Beatrice Shelukindo ya kuwa msikiti wa barabara ya saba uliopo katika manispaa ya Dodoma unafundisha mafunzo ya ugaidi na kareti kwa waumini wake imeuathiri msikiti huo.
Akizungumza na Jombo Shekhe Mohamed Awadhi wa msikiti huo alisema kauli yake hiyo Imewaathiri waumini wake kutokana kuukimbia na baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakisoma masomo kuhamishwa na wazazi wao.
Awadhi alisema hivi sasa wapo katika wakati mgumu kutokana na waumini waliokuwa wakiswali ndani ya msikiti huo kuamua kuhama baada ya kutolewa kauli ambayo wanaamini ni ya uzushi na uchochezi kwa ajili ya kupotosha jamii na serikali.
Shekhe huyo alisema kuwa msikiti huo umejengwa kwa miaka mingi na karibu baadhi ya wanaoswali ni pamoja na viongozi wa kiserikali wakiwemo askari toka taasisi mbalimbali kama vile polisi,wanajeshi,usalama na takukuru.
“Sasa kama kweli sisi tungekuwa tunafundisha hayo mafunzo ya ugaidi na kareti,serikali pamoja na waumini kutoka vyombo vya dola kweli msikiti huo ungeachwa bila kuchukuliwa hatua zozote”aliuliza Shekhe Awadhi.
Naye mlezi wa wanafunzi wa msikiti huo wa barabara ya saba Husseni Hamedi Fundi,alikiri baadhi ya wazazi na walezi kuwahamisha watoto wao kutokana na kauli iliyotolewa na mbunge huyo wa jimbo la Kilindi.
Fundi alisema kuwa msikiti unapokea wanafunzi kutoka nje ya Mkoa wa Dodoma kama vile Kigoma,Singida,Mwanza,Pemba,Zanzibar,Tanga na Bukoba kwa ajili ya kujifunza  lugha ya kiarabu na elimu ya Quran.
“Lakini hivi sasa baadhi yao wamehamishwa na wazazi, walezi na hii yote ni kutokana na uzushi uliotolewa na Mbunge huyo wa Kilindi ambaye sisi kama waumini wa msikiti huo tunaona amepotosha jamii na serikali yetu,
''Kauli yake hiyo imetudhalilisha sana hivyo tunaamini Mwanamama huyo anatakiwa kusema ukweli ukizingatia kuwa sehemu anayoielezea ni Bunge ambalo linalotegemewa na Watanzania wote'', Alisema Fundi
Kauli hiyo iliyoleta utata ilitolewa na Mbunge wa  jimbo la Kilindi Beatrice Shelukindo mei 4, mwaka huu wakati akichangia bajeti ya Wizara ya mambo ya ndani alisema msikiti huo wa barabara ya saba unatoa mafunzo ya ugaidi na kareti.

  CREDIT: RICHARD MWAIKEND

BABY MADAHA NA WOLPER WAMALIZA BIFU LAO......KISA KILIKUWA NI NYUMBA YA KUPANGA



WASANII wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ na Jacqueline Wolper Massawe ‘Wolper’ wamemaliza bifu lao lililokuwa likifukuta kama moto wa kifuu mwishoni mwa wiki mbili zilizopita.


Akizungumza na mwandishi  wetu katikati ya wiki hii, Baby alisema alikuwa Mkoani Geita kwa ziara ya kikazi lakini alipigiwa simu na Wolper akimuomba msamaha kutokana na tofauti zao zilizosababishwa na nyumba ya kupanga.

“Nimeona bora yaishe kwa sababu Wolper amekubali kosa na mimi siwezi kuendeleza bifu lakini kama asingeniomba msamaha tungefikishana mbali,’’ alisema Baby Madaha na kuongeza:

“Nimemalizana na Wolper ila kesi itabaki kwa mwenye nyumba, nitapambana naye hadi atakaporejesha mkwanja wangu japokuwa nimepata nyumba nyingine maeneo ya Mikocheni.”


Wolper na Madaha waliingia kwenye bifu zito baada ya Madaha kukuta nyumba aliyoilipia shilingi milioni 3.6 kama kodi maeneo ya Kinondoni jijini Dar imechukuliwa na Wolper  kabla yeye hajahamia.