Thursday, March 28, 2013

HONGERA DINA KWA KUPATA TUZO YA WOMEN OF THE YEAR



Leo hii kupitia tuzo za Tanzania Women Of Achievement Award (TWAA), mtangazaji wa Clouds Fm, kupitia kipindi cha Leo tena, Dina Marios, amejichukulia tuzo ya "Women of the year" , katika sherehe zilizofanyika katika hoteli ya Serena, iliyoko jijini Dar es salaam.
"sikutegemea kama nitapata tuzo hii, maana kila mmoja aliekuwa karibu yangu nilimuona kama mtu mzima sana, nikasema hawa ni watu wazima sana mimi hapa sidhani kama kuna changu, ila nikajipa moyo nikasema, hawa akina mama waliopata tuzo wamefanya kazi nzuri sana mpaka kufikia hapa, lakini kabla sijamaliza nikasikia wanataja jina langu ikiwa ni tuzo ya mwisho kutolewa. huwezi kuamini hata sikumbuki nilitoa speech gani pale ila kila mtu alisifia, nimeshukuru sana" amesema Dina
all the best to you, na mungu akuzidishie


HII NDIO COVER MPYA YA SINGLE INAYOFATA YA KANYE WEST


HII NDIO COVER MPYA YA SINGLE INAYOFATA YA KANYE WEST

Top Talent
Wakati wote Kanye anapotaka kutoa album yake inakuwa kama ni event, matokeo yake vyombo vya habari na ,mashabiki wanashindwa kusubiri kujua kuhusu ujio wake mapema iwezekanavyo.
kwa bahati mbaya, matarajio yao yanapelekea kuwepo kwa nyepesi nyepesi na ripoti ambazo saa nyingine zinakuwa sio za kweli, kwanfano kumekuwa na ripoti kadhaa kuwa album ya 6 ya West itakuwa inaitwa black American physcho, mara Rich Black American, na sasa kuwa ni Iam God
kutokana na post ya The Huffington, mtu wa karibu sana na Kanye kuwa "Iam God" sio jina la tittle ya album, lakini haliko mbali na tittle ya single yake inayofata.
msanii chini ya G.O.O.D. Music,Malik Yusef amethibitisha tittle kupitia mtandao wa twitter
@teamkanyechi its “I am(A) GOD” FAMO #psalms 82
— Malik Yusef (@malikyusef) March 26, 2013
inasemekana title hiyo imetokana na passage kwenye biblia Psalms 82:6-7 ambayo inasema “I have said, Ye are Gods and all of you are children of the Most High. But ye shall die like men, and fall like one of the princes.”
tofauti ndogo ya kuongeza “a” kuifanya iwe “I Am A God” ni kutofautisha kuwa wimbo hau suggest kuwa Kanye mwenyewe ndio the Creator lakini mtu huyo huyo ananguvu ya kuwa greater being.
West amekuwa na historia ya kuhusisha idea na picha za kidini katika kazi zake. moja kati ngoma zake zilizofanya vizuri ni “Jesus Walks” kutoka kwenye album ya off The College Dropout, alitokea kwenye cover ya Rolling Stone akiwa na taji la miba ambalo huwa linaonekana kwenye picha ya yesu, cheni kubwa yenye miungu ya Egymp Horus katika video ya "Power" na "Watch the throne", No church in the wild" amegusia theme ya morality versus decadence.
mpaka sasa haijatangazwa single wala album hiyo itatoka lin

28 March 2013 0 Comments 28 March 2013 By Admin Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP Suleiman Kova akiwa maeshikilia baadhi ya vipande vya meno ya Tembo vilivyokamatwa hivi karibuni katika eneo la Kimara Wilaya ya Kinondoni. Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP Suleiman Kova akifafanua kuwa Jeshi la polisi limeweka mikakati ya mpango kazi ikiwa ni pamoja na kushirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama pamoja na kikosi cha zimamoto ili kuhakikisha kuna udhibiti wa matukio ya uhalifu au fujo. Aidha amesema jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata bunduki mbili aina tofauti, moja ikiwa ni Shotgun yenye namba AB 44736 na ya pili ni Greener yenye namba 10883 pamoja na risasi 17. Na.INaMoTO Blog Team Jeshi la polisi kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kukamata vipande vya meno ya Tembo vipatavyo 13 ambavyo thamani yake haikufahamika mara moja. Tukio hilo limetokea katika eneo la Kimara wilaya ya Kinondoni ambapo askari walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema. Pamoja na kukamatwa kwa vipande hivyo pia amekamatwa mtuhumiwa Christopher Julius mwenye umri wa miaka 18, mwanafunzi wa Kidato cha Nne – Kibaha sekondari. Katika hatua nyingine kupitia misako mikali inayoendelea Jeshi la polisi limefanikiwa kukamata noti bandia 32 za shilingi elfu 10,000/= zenye thamani ya shilingi 320,000/= za kitanzania. Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP Suleiman Kova ametoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini hasa katika kuelekea siku kuu ambapo watu wasio na nia njema wanapenyeza pesa bandia kwa nia ya kujiongezea kipato binafsi.



  • 28 March 2013
  • By 
Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP Suleiman Kova akiwa maeshikilia baadhi ya vipande vya meno ya Tembo vilivyokamatwa hivi karibuni katika eneo la Kimara Wilaya ya Kinondoni.
Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP Suleiman Kova akifafanua kuwa Jeshi la polisi limeweka mikakati ya mpango kazi ikiwa ni pamoja na kushirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama pamoja na kikosi cha zimamoto ili kuhakikisha kuna udhibiti wa matukio ya uhalifu au fujo.
Aidha amesema jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata bunduki mbili aina tofauti, moja ikiwa ni Shotgun yenye namba AB 44736 na ya pili ni Greener yenye namba 10883 pamoja na risasi 17.
Na.INaMoTO Blog Team
Jeshi la polisi kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kukamata vipande vya meno ya Tembo vipatavyo 13 ambavyo thamani yake haikufahamika mara moja. Tukio hilo limetokea katika eneo la Kimara wilaya ya Kinondoni ambapo askari walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.
Pamoja na kukamatwa kwa vipande hivyo pia amekamatwa mtuhumiwa Christopher Julius mwenye umri wa miaka 18, mwanafunzi wa Kidato cha Nne – Kibaha sekondari.
Katika hatua nyingine kupitia misako mikali inayoendelea Jeshi la polisi limefanikiwa kukamata noti bandia 32 za shilingi elfu 10,000/= zenye thamani ya shilingi 320,000/= za kitanzania.
Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP Suleiman Kova ametoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini hasa katika kuelekea siku kuu ambapo watu wasio na nia njema wanapenyeza pesa bandia kwa nia ya kujiongezea kipato binafsi.

JACK WOLPER ATWAA TAJI LA IJUMAA SEXIEST GIRL




Jacqueline Wolper (kulia), akipokea cheti cha ushindi kutoka kwa DK. Cheni aliyekuwa jaji mkuu wa shindano hilo.  Wolper akiwa ameshikiria cheti chake muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi. Dok. Cheni akiwa kwenye pozi na Wolper juu ya jukwaa. Msanii wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz akiwajibika jukwaani na mnenguaji wake.
Chidy Benz akikamua jukwaani hapo.
Omm Dipoz akizungumza na mashabiki zake jukwaani.
Dogo Asley akiwajibika.
Awali jana mchana hawa ni baadhi ya watoto wakichezeshwa ukumbini hapo.
Watoto hawa wakijiandaa kushindanishwa moja ya mchezo wa kuzungucha rigi kiunoni jana mchana ukumbini hapo.
Mmoja wa watoto waliofika Dar Live mchana akikabidhiwa baiskeli baada ya kuibuka mshindi katika mchezo wa kuruka kamba.
Mchekeshaji maarufu Mtanga, akizungumza na mmoja wa watoto ndani ya Dar Live.
Sehemu ya umati uliyojitokeza ukumbini hapo.

MSANII wa chimbo la filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe, usiku wa kuamkia leo ameibuka kidedea kwenye shindano lililokuwa likiwashirikisha mastaa wa kike Bongo la Ijumaa Sexiest Girl ndani ya Ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.

Wolper amejizolea heshima lukuki na kitita cha sh. milioni 2 ikiwemo na ofa ya kulipiwa saluni kujiremba kwa mwaka mzima. Usiku wa leo pia ndani ya ukumbi huo kulikuwa na burudani kibao kutoka kwa Ommy Dimpoz, Chidy Benz, Dogo Asley, TOT Taarab na michezo kibao ya watoto iliyosindikizwa na shindano la Mkali wa Mic.



Jacqueline Wolper (kulia), akipokea cheti cha ushindi kutoka kwa DK. Cheni aliyekuwa jaji mkuu wa shindano hilo.  Wolper akiwa ameshikiria cheti chake muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi. Dok. Cheni akiwa kwenye pozi na Wolper juu ya jukwaa. Msanii wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz akiwajibika jukwaani na mnenguaji wake.
Chidy Benz akikamua jukwaani hapo.
Omm Dipoz akizungumza na mashabiki zake jukwaani.
Dogo Asley akiwajibika.
Awali jana mchana hawa ni baadhi ya watoto wakichezeshwa ukumbini hapo.
Watoto hawa wakijiandaa kushindanishwa moja ya mchezo wa kuzungucha rigi kiunoni jana mchana ukumbini hapo.
Mmoja wa watoto waliofika Dar Live mchana akikabidhiwa baiskeli baada ya kuibuka mshindi katika mchezo wa kuruka kamba.
Mchekeshaji maarufu Mtanga, akizungumza na mmoja wa watoto ndani ya Dar Live.
Sehemu ya umati uliyojitokeza ukumbini hapo.

MSANII wa chimbo la filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe, usiku wa kuamkia leo ameibuka kidedea kwenye shindano lililokuwa likiwashirikisha mastaa wa kike Bongo la Ijumaa Sexiest Girl ndani ya Ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.

Wolper amejizolea heshima lukuki na kitita cha sh. milioni 2 ikiwemo na ofa ya kulipiwa saluni kujiremba kwa mwaka mzima. Usiku wa leo pia ndani ya ukumbi huo kulikuwa na burudani kibao kutoka kwa Ommy Dimpoz, Chidy Benz, Dogo Asley, TOT Taarab na michezo kibao ya watoto iliyosindikizwa na shindano la Mkali wa Mic.

"MAKALIO YANGU HUNIFANYA NIKOSE AMANI MTAANII".....AGNESS MASONGANGE


VIDEO Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ambaye muda mwingi amekuwa akiishi Afrika Kusini ameelezea jinsi maisha ya Bongo yalivyomchosha huku usumbufu anaopata kutokana na makalio yake makubwa ikiwa moja ya sababu.

Akipiga stori mwandishi wetu, Masogange alisema umbile lake hilo limekuwa likimfanya akose amani anapokatiza mitaani, tofauti na Sauzi ambako wanawake wengi wamefungashia huku yeye akionekana ‘cha mtoto’.


“Muda mwingi niko Sauzi, Bongo miyeyusho na hili umbo langu nimekuwa nikisumbuliwa sana na wanaume lakini Sauzi hili langu la kawaida, wengi wamefungashia ile mbaya, kwa hiyo muda mwingi nitakuwa huko, huku nitakuwa nakuja na kuondoka,” alisema Masogange

RIPOTI YA GAZETI LA IJUMAA KUHUSU WABUNGE KUTEMBEA NA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DODOMA ( UDOM )




MITANDAO mingi ya kijamii na kurasa binafsi za mawasiliano zinazopatikana ndani ya simu za viganjani kama Instagram, WhatsApp na BBM (Blackberry Messenger) zinazomilikiwa na baadhi ya wasichana wanaosoma Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) zimejaa mambo ya ngono na kashfa kwa baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Unyemeleaji taarifa uliofanywa na Ijumaa kwa muda mrefu kwenye huduma hizo za mawasiliano ya kisasa  umebaini wanafunzi wa kike wamewabatiza jina la ‘mabuzi yao’ baadhi ya wabunge.


Bila kupepesa mitandao hiyo imekuwa pia ikitumiwa na wasichana hao kuuza miili yao huku ufahari kama si ujanja ukiwa ni mtu kujipatia bwana mwenye cheo cha ubunge ambaye anaaminika waleti yake haikaukiwi fedha kutokana na posho za vikao na utumishi wa umma.

 
SIKILIZA TUKUPASHE
“Shoga naona unawapanga tu waheshimiwa,” mchangiaji mmoja kupitia kundi la BBM alichangia kwenye moja ya picha aliyoweka rafiki yake akiwa amepozi na mbunge mmoja kutoka mikoa ya Magharibi  (jina kapuni) ambapo bila haya majibu ya mwenye ukarasa huo yalikuwa: “Maisha bila mabuzi hayaendi bi dada.”

Upekuzi wa kiintelijensia wa Ijumaa ulichungulia dokezo za wachangia mada na kubaini kuwa waheshimiwa wanaoingia mjengoni kama wawakilishi wa wananchi wanachukuliwa kama mabuzi kwa tafsiri ya kuchunwa fedha huku kipindi cha vikao vya bunge vikichukuliwa kama nyakati za migodi kutema dhahabu.

MAMBO YA KUFEDHEHESHA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wasichana hao wa chuo wamekuwa wakihifadhi picha za utupu za wabunge wenye uhusiano nao kwenye simu zao za mikononi walizowapiga walipokuwa wakifanya nao ngono ambapo wakati mwingine huzitundika mitandaoni kwa kubipu na kuziondoa haraka lengo likiwa ni kuwaonesha ushahidi huo marafiki zao.

Miongoni wa wabunge waliokumbwa na aibu hiyo ambao Ijumaa liliziona picha zake za aibu ni pamoja na mbunge anayetoka kanda ya Kusini, mwingine kanda ya ziwa na mmoja kutoka jijini Dar es Salaam huku waziri mwenye heshima kubwa naye akiingia mkenge kwa kupiga picha na msichana wakiwa kitandani vifua wazi.

WANAFUNZI WA KIUME WANASEMAJE?
Ijumaa lilipowauliza baadhi ya wanafunzi wavulana wanaosoma chuoni hapo juu ya kuwepo kwa tabia za  baadhi ya wabunge kutembea na wanafunzi wa kike walikiri na kuongeza kuwa ukata ndiyo unaosababisha baadhi ya wanachuo wajitongozeshe kwa waheshimiwa.

“Wanachofuata ni fedha siyo mapenzi, wapo wasichana hapa kipindi cha bunge hawaonekani kabisa chuoni, wanakuwa na waheshimiwa wakistarehe, kuna wengine wanasomeshwa, wanahudumiwa,” alisema mwanafunzi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Bonny.

IJUMAA LINASEMAJE?
Dawati la Ijumaa linawatahadharisha waheshimiwa wabunge wenye tabia za ukware kuachana na mambo ya kihuni, badala yake wajiheshimu vinginevyo watajikuta matatizoni na kuambulia aibu kubwa mbele ya jamii kwa kuanikwa kwenye magazeti siku si nyingi pia picha zao za aibu zitafikishwa kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda.


RIPOTI IMEANDIKWA NA  GLOBAL PUBLISHERS

MENEJA WA KAMPUNI YA NDEGE YA FASTJET ATIWA MBARONI




MENEJA wa Wafanyakazi wa Ndani ya Ndege wa Kampuni ya Fastjet Emma Donovan, alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam kujibu shtaka linalomkabili la kutoa lugha ya matusi.

Emma (40) alipandishwa kizimbani jana na kusomewa shtaka hilo na Wakili wa Serikali Nassoro Katuga, mbele ya Hakimu Joyce Minde.
Katuga alidai Machi 19 mwaka huu Emma alimtolea lugha ya matusi Samson Itinde jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Emma alikana shtaka hilo ambapo Katuga alidai upelelezi umekamilika na kuomba kupangiwa tarehe kwa usikilizwaji wa awali.

Hakimu Joyce alisema kuwa dhamana ya mshtakiwa iko wazi lakini kwa kuzingatia vigezo vya dhamana vitakavyotolewa kwa kuwa mshtakiwa ni raia wa kigeni.

Alitaja masharti ya dhamana kuwa mshtakiwa anatakiwa kuwasilisha hati yake ya kusafiria au kutoa fedha taslim sh milioni tano na pia awe na wadhamini wawili ambao ni Watanzania.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 9 ili kupangwa tarehe ya kuanza kwa usikilizwaji wa awali.


Katika  kile  kinachoonekana  kuwa  ni  mwendelezo  wa  ugomvi  wa Sintah  na Rayuu, wasanii  hawa  wameendelea  kurushiana  matusi  ya  nguoni  na  kuumbuana  kila  siku......

Sintah aliwahi  mtuhumu  Rayuu  kuwa  ni  kahaba  mwenye  kiwango  na  aliyeshindikana.Tuhuma  hizo  zilikuja  baada  ya picha  za uchi za msanii Rayuu  kuvuja  mtandaoni  zikionesha  makalio  na  matiti  yake.....

Baada  ya  tuhumu  hizo, Rayuu  naye  ameendelea  kufichua  mambo  mengi  kuhusiana na Sintah kwa  kudai  kuwa  Sintah  ni  kahaba  na  haoni  aibu  maana  umri  wake  umeenda....

Rayuu  anadai  kuwa  ukahaba  ulimfanya  Sintah aachwe  na Juma  Nature.Msanii  huyu  ameenda  mbali  zaidi  baada  ya  kudai  kuwa  amewahi  muona  Sintah  kwa  macho  yake  akijiuza  maeneo  ya  Manzese.....

Hiyo  ni  post  ya  Rayuu aliyoitupia  facebook  jana. 

SERIKALI YATANGAZA NAFASI ZA KAZI 1,134




Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia Watanzania wenye sifa na uwezo kujaza nafasi wazi za kazi kama zilivyo katika Tangazo la Lugha ya Kiingereza na Kiswahili.

Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya Waajiri mbalimbali wa ofisi za umma.


Daudi alifafanua kuwa Waajiri hao ni pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Katibu Mkuu wizaraya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa, Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo Jinsia na Watoto, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara. Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Katibu Ofisi ya Rais Maadili,

Wengine ni Katibu Tawala wa Mkoa Kagera, Iringa, Ruvuma, Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Manyara, Dar es Salaam, Morogoro, Geita, Pwani, Mara, Kilimanjaro, Lindi, Singida, Tabora, Tanga, Katavi na Arusha, Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Iringa, Songea, Shinyanga,
Morogoro, Singida, Kigoma/Ujiji na Temeke.

Nafasi nyingine ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Mufindi, Kyela, Rungwe, Mbeya, Chunya, Biharamulo, Bukoba, Muleba, Namtumbo, Songea, Morogoro, Makete, Mkuranga, Mbinga, Tunduru, Ukerewe, Sengerema, Ilemela, Busega, Maswa, Meatu, Shinyanga, Kishapu, Kilosa, Msalala, Rufiji, Rorya, Ruangwa, Lushoto, Mkinga, Mpanda, Monduli, Ngorongoro,Kigoma, Nachingwea, Rombo, Same, Singida, Urambo, Tabora, Babati, Mbulu, Simanjiro, Kiteto, Handeni, Pangani, Kibondo, Chamwino, Mtwara, Nanyumbu, Mpwapwa, Kongwa naTandahimba. Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe, Kibaha, Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na TEMESA.

Katibu huyo amesema kuwa nafasi hizo zilizotangazwa zimegawanyika katika kada zifuatazo; Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta daraja la II – (Nafasi 10), Afisa Vipimo II – Nafasi 6, Mpima Ardhi daraja la II (Nafasi 26), Mhandisi daraja la II – Ufundi Umeme – Nafasi 9,  Afisa Mipango Miji daraja la II– Nafasi 13, Mhandisi daraja la II - Ujenzi (Nafasi 16), Mhandisi daraja la  II - Maji (Nafasi 13), Afisa Misitu daraja la II (Nafasi 7), Afisa wa Sheria daraja la II – nafasi 3, Mtakwimu Daraja la II – nafasi 8, Mthamini daraja la II – Nafasi 7,  Mkadiriaji Ujenzi daraja la II  – nafasi 4, Afisa Ufugaji Nyuki Daraja la II – nafasi 1, Mhandisi Daraja la II – Nishati (Nafasi 3), Msanifu Majengo Daraja la II– (nafasi 3) na Mjiolojia Daraja la II – Nafasi 7, Fundi Sanifu daraja la II (Ujenzi) -Nafasi
26, Mvuvi Msaidizi Daraja la II – nafasi 8 na Fundi Sanifu Msaidizi (Maji) -nafasi 19.

Nafasi nyingine zilitotangazwa na Serikali ni Nahodha Daraja la II – Nafasi 6, Fundi Sanifu daraja la II - Haidrolojia -Nafasi 6 ,Fundi Sanifu Daraja la II -Nafasi 6, Msaidizi Misitu Daraja la II – nafasi 7, Fundi Sanifu Daraja II – Ramani – Nafasi 6, Fundi Sanifu Daraja la II –Maendeleo ya Jamii– Nafasi 3, Dereva Mitambo Daraja la II– nafasi 1,  Mpiga chapa msaidizi- Nafasi 5, Operata wa kompyuta msaidizi - nafasi 3, Fundi Sanifu Daraja la II - Migodi – nafasi 9, Polisi Msaidizi– Nafasi 5, Mpokezi–Nafasi 1, Katibu Mahsusi daraja la III-nafasi 10, Mlinzi –Nafasi 100, Dereva Daraja la II – nafasi 178,   Msaidizi wa Ofisi– Nafasi 30, Afisa Kumbukumbu daraja la II– nafasi 1,  Mwenyekiti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya – nafasi 5, Afisa Mtendaji wa Kata Daraja la III– nafasi 10, Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la II– nafasi 6.

Aidha, kada nyingine ni Afisa Mtendaji wa Kijiji daraja la III) – nafasi 232, Afisa Mtendaji Mtaa daraja la III– nafasi 3, Afisa Lishe daraja la II– nafasi 4, Fundi Sanifu Daraja la II - Ufundi na Umeme, Afisa Biashara msaidizi– Nafasi 1, Mchapa Hati daraja la II – Nafasi 1,  Mhandisi Daraja la II –Baharini-(nafasi 1), Dereva Mitambo Daraja la II – (nafasi 1), Dereva wa Vivuko daraja la II – Nafasi 3, Mkufunzi Mwandamizi Daraja II - Nafasi 1, Mkufunzi Daraja ii - Nafasi 2, Fundi Sanifu Msaidizi (bomba)–nafasi 3, Fundi Sanifu Msaidizi (Umeme) –Nafasi 4, Mkufunzi Daraja II– nafasi 3, Mkufunzi daraja la II -Jiolojia – nafasi 1, Mkufunzi Msaidizi– Jiolojia – nafasi 1, Fundi Sanifu daraja II -Ubunifu Mipango Miji – nafasi 1, Fundi Sanifu daraja II- Urasimu Ramani – Nafasi 5, Fundi Sanifu daraja II- Uchapaji Ramani –Nafasi 4, Fundi Sanifu Daraja la II -Maabara– nafasi 13, Fundi Sanifu Msaidizi (Ujenzi– nafasi 1), Fundi Sanifu daraja la II -Nafasi 4, Wakufunzi wasaidizi – nafasi 54 na Mhasibu Mkuu daraja II.

Katibu alifafanua kuwa nafasi 949 zilizoko katika tangazo la Kiswahili ni kwa ajili ya Waajiri walioainishwa hapo juu na kwa Tangazo la nafasi wazi 185 zilizoko katika tangazo la lugha ya Kiingereza ni kwa ajili ya Taasisi na Wakala mbalimbali za Serikali.

Daudi amesema mwisho wa kupokea barua za maombi ya kazi ni tarehe 9 Aprili, 2013.


Aidha, amewataka waombaji wote wa fursa za ajira kufungua matangazo yote mawili ya kazi na kuzingatia masharti ya Matangazo yote kama yalivyo katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili kabla ya kutuma maombi yao.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.  27 Machi, 2013

Kwa maelezo zaidi; wasiliana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
kwa Barua pepe; gcu@ajira.go.tz  au Simu; 255-687624975

"SIPO TAYARI KUJIUZULU KWA KUOGOPA MAJUNGU YA VYAMA VYA UPINZANI".....NAIBU WAZIRI WA ELIMU




Victoria fm ya mjini Mwanza jana asubuhi kipindi cha matukio wameripoti kuwa wamefanya mahojiano na naibu waziri wa elimu Bw.Philip Mulugo kuhusu tuhuma zinazomkabili ambapo amesema hawezi kujiuzulu kwa kuogopa majungu ya vyama vya upinzani wanaopika uongo juu yake ili kuwika kisiasa.

Mulugo amekanusha madai yote yaliyoandikwa na gazeti la Mwananchi na kudai kuwa kama kuna mwenye wasiwasi na elimu yake aende akamuoneshe vyeti vyake vya elimu ya sekondari hadi vya taaluma na chuo alichosoma