Thursday, April 4, 2013

http://t.co/Ww1mWwS0Zp

Mandela arudishwa hospitalini Pretoria



 11 Machi, 2013 - Saa 09:07 GMT
Mandela apelekwa hospitalini tena
Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela amepelekwa hospitalini kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.
Taarifa kutoka kwa afisa ya Rais wa Afrika Kusini zimesema kuwa uchunguzi huo ni wa kawaida tu.
Kwa muujibu wa tovuti ya Urais, Madaktari wanaomfanyia uchunguzi Mzee Mandela wamesema hakuna haja ya kuwa na taharuki yeyote.
Kwa muda mrefu sasa hali ya kiafya ya rais huyo mstaafu imekuwa ni swala la kutia wasiwasi.
Mandela mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini kwa siku 18 mwezi wa Desemba mwaka jana kutokana na kutatizwa na mapafu pamoja na vijiwe ndani ya kibofu chake cha mikojo.
Taarifa iliyoandikwa kwenye mtandao wa Ofisi ya Rais Jacob Zuma zimeeleza kuwa Mzee Mandela alipelekwa katika Hospitali ya Mjini Pretoria kwa uchunguzi wa kawaida wa ki-afya.
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na matatizo yanayoambatana na umri wake mpevu.
Mzee Mandela alihudumu kama rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 1994 hadi 1999 na ndiye rais wa kwanza mweusi kuwahi kuitawala nchi hiyo.
Kutokana na juhudi zake za kupigania demokraisa na kupambana na sera za ubaguzi wa rangi nchini humo, Mzee Mandela anatambulika kama Baba wa Taifa nchini Afrika Kusini.
Tangu mwaka 2004 Mzee Nelson Mandela amekuwa hajitokeza hadharani au kushiriki katika shughuli zozote za umma.

Magazeti ya Leo


.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC03823
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC03834

MAGHOROFA 100 JIJINI DAR NI FEKI.....SERIKALI YAWA BUBU




Dar es Salaam.
Kuporomoka jengo lililopo Mtaa wa Indira Gandhi Jijini Dar es Salaam, huenda ikawa mwanzo tu wa kuporomoka majengo mengine zaidi hasa kufuatia matokeo ya tume iliyoundwa mwaka 2006 iliyobaini zaidi ya majengo 100 Jijini Dar es Salaam yamejengwa bila kuzingatia viwango.
Kwanini Serikali haichukui hatua kwa majengo hayo 100 yaliyobainika kuwa hayajajengwa kwa kuzingatia viwango? Wenye akili timamu wanaweza kuendelea kujiuliza maswali mengi zaidi na kujibu wanavyoweza.
Wapo wanaoweza kusema rushwa ndio inasababisha mambo mengi kutofanyiwa kazi kwa ufasaha, lakini mbele ya sheria utaombwa utoe ushahidi, hapo bila shaka patafanya wengi kubadili maneno kwamba aaah labda Serikali inaendelea kufanya mchakato, mpango mkakati, mkakati yakinifu nk dhidi ya majengo hayo
.
Kubomoa jengo lenye ghorofa 16 au hata chini au zaidi ya hapo baada ya kulibaini halijazingatia viwango, ni lazima uwe na uso mgumu. Baadhi ya wananchi wanasema wenye majengo bila shaka hawawezi kutulia wakisubiri sheria ifanye inachotakiwa kufanya, hapo ndipo ugumu unapoanzia.
Pinda analo na kujibu
Baadhi ya watu wanafikiri kuondolewa madarakani kwa viongozi walio katika wizara husika na sakata hili akiwemo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye ofisi yake ilichunguza na kubaini maghorofa zaidi 100 kuwa ni feki, kunaweza kuwa ni mojawapo ya mambo muhimu kwa sasa.
Mke na watoto wafukiwa
Licha kwamba jengo hilo liliporomoka saa 2.30 asubuhi, baadhi ya watu waliofukiwa na kifusi cha jengo hilo walikuwa wakiwasiliana na jamaa zao kwa njia ya simu na wengine wakipiga kelele za kuomba msaada.
Idd Baka ambaye alikuwa akiwasiliana na mkewe ambaye aliegesha gari huku ndani kukiwa na watoto wake wawili alikwenda dukani kununua bidhaa, mara jengo hilo likaporomoka, alikuwa akiwasiliana nae hadi majira ya mchana simu ya mke wake haikuwa inapatikana.
Vifaa duni
Ni dhahiri kwamba endapo kungekuwapo na vifaa vya kutosha katika zoezi la uokoaji lingewezaa kufanikiwa kwa  muda mfupi na kwa kiasi kikubwa hivyo kuwapata majeruhi wakiwa hai.  
Katapila latumika
Cha  ajabu na aibu kwa taifa kutokuwa tayari kwa kuwa na vifaa vya kuokolea kwani tangu saa 2:30 hadi ilipofika saa 4.30 ndipo lilipatikana katapila moja ambalo nalo halikuwa na tija kutokana na kuwapo kwa uwezekano wa kuwakandamiza au kuwajeruhi zaidi  watu waliofukiwa na kifusi hicho.
Kutokana na kutokuwepo na vifaa vya kukatia nongo waokoaji iliwachukua takribani dakika 15 kukata nondo zilizokuwa zimemkandamiza.
Umati wa watu ulivamia kifusi na kuanza kukisomba kwa mikono  ili hali jambo hili lilikuwa kama mchezo wa kuigiza ambao umegharimu uhai wa watu zaidi ya 35 pamoja na kuharibu magari yaliyobondwa na kuwa kama chapati takribani matano.
Mashuhuda
Ali Mparang’ombe mmoja wa mafundi wa jengo hilo anasema kudondoka kwa jengo hilo ni mtiririko wa majengo mengine kutokuwa katika viwango vinavyotakiwa.
“Ndugu yangu mimi ni fundi nilikuwa nimeingia ndani, lakini nilitoka kwenda upande wa pili kutafuta chai kwani leo (Ijumaa iliyopita) ni sikukuu mama lishe hawakuwepo wengi hapa”anasimulia Mparang’ombe na kuongeza:
“Ndipo kwa kule nilisikia kishindo kikubwa, kuja kuangalia ni jengo nililotoka takribani dakika 15 tu limeanguka, nimepoteza watu muhimu sana ambao tulikuwa tukifanya sote kazi, sasa sijui itakuwaje”.
Mparang’ombe anasema jengo hilo lilikuwa likijengwa chini ya viwango kwani katika ndoo 12 za mchanga walikuwa wakichanganya saruji mfuko mmoja.
Majengo mengi feki
“Hapa kama kama ndoo 12 mfuko mmoja wa saruji unategemea nini, na ni majengo mengi hapa mjini ambayo yamejengwa kwa aina hii, hivyo ni kudra za Mwenyezi  Mungu zinahitajika”anasema Mparang’ombe.
“Jengo hili lilipofika ghorofa ya 12 lilisimamishwa kujengwa na ghorofa ya 15 lilisimamishwa tena lakini hatujui alikuwa anatumia njia gani hadi akawa anaruhusiwa kuendelea na ujenzi,” anasema.
Kibali cha jengo lililoanguka
Naibu Meya wa Halmashauri ya Ilala, Kheri Kessy alisema mwaka 2007 walitoa kibali kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kushirikiana na ‘Aliraza Investment Limited’ kujenga jengo la ghorofa 10.
Alipotakiwa kueleza kwa nini hawakuchukua hatua baada ya kuendelea kujengwa hadi kufikia ghorofa zaidi ya 10,  alisema hawahusiki, ila kuna taasisi zingine za Serikali zinazosimamia majengo zinatakiwa kuulizwa.
Matokeo ya tume yanapuuzwa
Mwaka 2006 Tume iliyoundwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa ilibaini kuwa zaidi ya maghorofa 100 yaliyopo jijini Dar es Salaam yalikuwa chini ya viwango.
Idadi hiyo ni tone tu la maghorofa yaliyo chini ya viwango nchi nzima ambayo bila shaka kuyabomoa ugumu unakuja pale wamiliki wake kuwa vigogo na wafanyabiashara mashuhuri.
Hali kadhalika akiwa bungeni wakati wa majumuisho ya Ofisi yake Bungeni mwaka 2008/09, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema ofisi yake ingechukua hatua za makusudi dhidi ya majengo ili kuzuia vifo kama hivi visivyo vya lazima. Kufumbia macho mambo ndiko leo kumesababisha watu zaidi ya 35 kuuawa, achilia mbali mali zingine yakiwemo magari

WEMA SEPETU AAMUA KUTOKA KIMAPENZI NA "SERENGETI BOY" ILI KUMUUMIZA DIAMOND PLUTNUM



Wema Sepetu  ameamua  kuhamishia majeshi  yake  kwa  kiserengeti  boy  ili  kulipiza  kiasi  kwa X wake  wa zamani, DIAMOND.....

Huyu  ni  Haidary Cavilla  ambaye  ni mchumba  wa  miss  Tanzania namba  2 ,mwaka  2000, aitwaye  Mercy Galabawa....

Kama kawaida, jamaa  ni  mdogo kiumri akilinganishwa na Wema, lakini  inasemekana  kwama  Haidary  anamiliki  mkwanja mrefu  ulioichanganya  akili  ya  Wema Sepetu  hasa  baada  ya  kununuliwa gari aina  ya Audi Q7.....


Picha  hizi  zilipigwa  nyumbani  kwa wema  sepetu na  hatimaye  kuvuja  mitandaoni,hali inayoashiria  kulipiza  kisasi kwa Diamond  baada  ya kunaswa  akiwa  na  Penny....

  Wema sepetu ni mrembo anayekabiliwa na   skendo  chafu ya kubadiliwanaume kama  nguo.Alianza na..

1.HERRY SAMIR
2.KHALEED MOHAMED
3. Marehemu STEVEN KANUMBA
4.JUMBE YUSUPH  JUMBE
5.CHARLES GABRIEL
6.DIAMOND PLUTNUM
7. CLEMENT  ( Bado  wako pamoja)
8. HAIDARY CAVILLA
Na wengineo......       

DIAMOND AWEKA HISTORIA MPYA BUKOBA



Napenda kuchukua Nafasi Hii Kumshukuru mungu kwa
 uzima na afya tele aliyonijalia.....
Mpaka kuwasili salama bukoba tarehe 30 march mwaka huu
.....Pia napenda kuwashukuru mashabiki
wote wa mjini bukoba waliojitokeza kwa wengi katika 
usiku wa wasafi mjini bukoba..
Mashabiki walifurika kufikia kunifanya mimi kuwa na 
furaha na faraja kubwa wakati nipo
stejini....na kuzidi kufanya manjonjo mengi na ujuzi
mwingi nikiwa stejini kama kawaida yangu...

Nilikinukisha vilivyo kama kawaida yangu...Nikiwa
 na Silaha zangu za maangamizi
Jeshi la wasafi kwenye Steji....na Kuweka Historia 
Mpya ndani ya Bukoba kuwa 
mwanamuziki wa kwanza kupiga show mwenyewe na
 kujaza watu zaidi ya 3,000 hadi 
 kufikia Uongozi kusitisha kuuza Ticket kutokana na
 Jeshi la Polisi kutoa 
taharifa ingweza kutokea mahafa kama ilivyotokea
 kabla ya Mimi kupanda
Jukwani.....

Zifuatazo ni Picha za Show Ndani ya Bukoba....!!





Taratibu....Mdogo mdogo kusongesha mzigo...!!











Love ilitawala kwa mashabiki kufikia mimi kuvutwa chini na mashabiki 
ukumbini humo...!! kweli mashabiki wa BUKOBA walikuwa na mizuka...!!






Mikono Juu......wotee wotee....!!
Mizuka ishapanda sasa....Ni kukinukisha mpera mpera 
mwanzo mwisho...!!

Camera Man na mashabiki awakuwa nyuma kupiga picha za 
ukumbusho mahana
historia mpya iliwekwa ndani ya jiji la wahaya.....!!





kwenye show viuno mbele mbele...... aghaaa mule mule...!!



Mambo ya kanga moja laki si pesa.....walikuwemo pia....!!

KITU ndembe ndembe...kanga mpya ailoi maji......
!! kit6u ndembe ndembe....!!

kitu mwake waacha weeee....agha ghaaaaaaaa .......laki si pesa
milioni pocketman...!!