Monday, June 10, 2013

BREAKING NEWZZZZZ:MSANII WA BONGO MOVIE KASH AFARIKI DUNIA MUDA HUU


Marehemu Jaji Khamisi (Kashi)

Habari iliyotufikia hivi punde ni kwamba msanii wa filamu nchini Jaji Khamis (Kashi)aliyewahi kutamba na michezo ya ITV enzi zile akiwa na wasanii kama mzee Masinde,Samson na wengine katika mchezo wa Tamu chungu na mingine mingi Amefariki dunia mchana huu katika hosptali ya taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa,akizungumza na rais wa shirikisho la wasanii amesema kuwa tasnia yake bado inaendelea kukumbwa na majanga  lakini amedai yote ni kazi ya mungu
Nae mzee Masinde ambaye alikuwa nae katika kundi moja akiwa kama kiongozi wake amesema kashi ni msanii ambaye alikuwa mpiganaji na kwa hakika ni pigo kubwa katika tasnia yetu
Mungu ailaze roho ya marehemu Jaji Khamis (Kashi) mahali pema pepponi Amini.

HATIMAYE H. BABA NA FLORA MVUNGI WAFUNGA NDOA.....


BAADA ya maneno kibao katika uhusiano wao, hatimaye wasanii wa filamu na muziki Bongo, Hamis Ramadhan Baba ‘H. Baba‘ na Flora Mvungi, wametiza ahadi yao ya kufunga ndoa ya nguvu.

H Baba na mkewe Flora Mvungi katika pozi.
 
Wawili hao walifungishwa ndoa na Shehe Maulid katika Msikiti wa Kibo, uliopo Ubungo, Dar, Jumamosi iliyopita na baada ya ndoa kufungwa sherehe ilifanyika nyumbani kwa akina Flora maeneo ya Kibo.


“Tumefurahi sana na tunamshukuru Mungu kwa kuwa tumetimiza ndoto yetu kwani maneno yamesemwa mengi sana juu ya uhusiano wetu lakini Mungu ameendelea kutuweka pamoja mpaka tumefunga ndoa,” alisema Flora.


Flora akimnywesha mumewe kinywaji.
Baada ya watu kula na kunywa na maharusi kusaini vyeti vya ndoa, waliondoka kuelekea nyumbani kwao Mikocheni, Dar ambako kulikuwa na sherehe ya maulidi kulikokuwa na vyakula na vinywaji vya kutosha.
H Baba akisaini kitabu cha ndoa.
Akizungumza na mwandishi  wetu, H. Baba alifunguka kuwa aliamua kutokufanya sherehe ukumbini kutokana na wazee wake kukataa kwani kwa dini ya Kiislamu hairuhusiwi kufanya sherehe ukumbini ndiyo maana wakaamua kufanya maulidi tu.
 Flora naye akisaini kitabu cha ndoa.

"MWANAFUNZI WANGU WA KIKE ANANITAKA KIMAPENZI.. KILA SIKU HUKAA MBELE TENA KIHASARA"...MWALIMU

Mimi  ni mwalimu wa shule moja  ambayo sitaitaja. mwezi uliopita mwanafunzi wangu wa kike ambaye  yuko  kidato  cha  tatu alinifuata na kuniambia anataka kunipa zawadi...

Sikuwa na hili wala lile, hivyo nilimwambia ni poa tu kama ameamua  kunikumbuka mwalimu wake..

Zawadi aloniletea ilinifanya  nishike  kichwa maana  sikutegemea.Yule mwanafunzi  aliniletea chupi aina ya boxer 3  na  tangu siku hiyo kila akiniona ananifanyia vituko mpaka ananikalia nusu  uchi  darasana nikiwa nafundisha  kwa vile anakaa viti vya Mbele....

Nikiwa  kama  mwalimu, nimejaribu  kutumia  viboko  ili  kumuonesha  kwamba  sina  mpango  naye lakini  bado  imeshindikana..

Nifanyaje  ndugu  zangu?  Maadili  ya  kazi  yananibana.Hata  hivyo, mwanao  ni  mwanetu  sote.