Friday, April 19, 2013

DARASA LA SABA SASA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU NCHINI



Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao.

Udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo 2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi ya chuo kikuu.

Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B.
 

Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu, lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo maalumu.
 

Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama ‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine.
 

Sifa zinazotakiwa
 
Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.

“Mwombaji anatakiwa kuwa na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma.
 

Awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuoni,”alisema Dk Maronga na kuongeza:
 

“Kuna watu wameishia darasa la saba, lakini wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa mahakama, mwandishi wa habari kwa muda mrefu. Hivyo mfumo huu utawawezesha kuendelea na masomo bila tatizo.”
 

Vigezo
 
Mkurugenzi huyo alisema, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu, ambayo mtahiniwa ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B.

Alisema daraja la kwanza linaloanza na alama A ni 75-100, daraja B+ ni 60-75, B ni 50-59, C ni 40-49, D ni 35-39 na daraja E ni 0-34.
 

“Katika mitihani mitatu atakayoifanya, atatakiwa kupata wastani wa daraja ‘B’ na somo husika la fani yake atatakiwa kupata alama B ili kuwa na vigezo vya kupata cheti kitakachomwezesha kuendelea na masomo yake,”alisema Dk Maronga.
 

WASSIRA AMTETEA RAIS KIKWETE KUWA YEYE SI MUASISI WA UDINI HAPA NCHINI



WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira, amepinga vikali madai yaliyotolewa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema) akidai kuwa Rais Jakaya Kikwete ndiye muasisi wa udini. 

Akizungumza bungeni jana, Wassira alimshangaa Lema kwa kutoa kauli hiyo, ambayo alisema imemvunjia heshima rais na kwamba hiyo ni kinyume cha Katiba. 

“Mimi nimesikitishwa sana na kauli ya Lema (Mbunge wa Arusha Mjini) aliyoitoa jana (juzi) humu ndani akisema Rais Kikwete ndiye mwasisi wa suala la udini.

“Nimeshangazwa kwa sababu tuhuma hizi dhidi ya mkuu wa nchi ni nzito hazipaswi kusemwa tu hivi hivi, mimi nafikiri hili Bunge sasa sijui tunakwenda wapi.

“Kwa maneno haya Lema amevunja Katiba kwa kusema makali kiasi hiki dhidi ya rais, tunataka Lema alete ushahidi juu ya tuhuma hizi.

“Rais anapoteua wakuu wa mikoa na wilaya anashauriana na waziri mkuu ambaye huyu tuliyenaye leo ni mkiristo.

“Anapoteua makatibu wakuu anashauriana na katibu mkuu kiongozi, Ofisi ya Rais ukimwondoa yeye mwenyewe waliobaki wote ni Wakristo. Huo udini uko wapi?

“Lema lazima ajue kuna hotuba za kijiweni na hotuba za bungeni lazima atofautishwe, lakini hapa kinachofanyika watu wanaleta hotuba za kijiweni badala ya hotuba za Bunge.

“Mgogoro wa kuchinja, mimi nilikwenda kule Geita kwenye mgogoro tukamaliza huu mgogoro kwa kuwashirikisha waumini wa dini, nashanga Lema anasema Serikali haijachukua hatua yoyote.

“Namtaka Lema popote alipo ajue kwamba Serikali inafanya kazi kwa utaratibu, alitaka tuende pale tutoe amri, asubiri atakapoingia madarakani sijui ni lini ndipo aendeshe Serikali kwa amri tu bila kushirikisha watu

Wassira alikuwa akihitimisha hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais (Utumishi) ambapo alisema hisia za udini nchini zimechochewa zaidi kupitia mikanda (CD) mbalimbali ya kidini.

Alisema Kanda hizo zilikuwa zikihamasisha na kuwataja viongozi na maaskofu wa Kikristo, lakini zote zimekamatwa na serikali imeahidi kuwalinda viongozi hao.

Alisema kanda zote zimekamatwa na yeyote mwenye nazo akikamatwa atachukuliwa kuwa ni mchochezi sawa na waliotengeneza kanda hizo.

“Wale waliokimbilia nje ya nchi tunaendelea kuwatafuta kwa kutumia polisi wa kimataifa (Interpol) ili waje kujibu kesi ya uchochezi.

“Mheshimiwa Spika, hata hivyo udini unaoenezwa bado haujavuruga maisha ya wananchi, kwamba wananchi huko mitaani wanaendelea kushirikiana vizuri, hakuna kubaguana. Na nadhani tatizo halijawa kubwa kupindukia.

“Suala la udini linakuzwa zaidi na watu wenye malengo mabaya ya kisiasa, tangu huko nyumba hata Zanzibar yenye asilimia zaidi ya 90 waislamu haijawahi kuitangaza Zanzibar kuwa ni nchi ya kiislamu.

“Udini ulichochewa na wanasiasa mwaka 2010 kwa sababu ya watu kutaka madaraka. Mwaka huo haukuwa mzuri sana, lakini tuyaache, yaliyopita si ndwele.
 

“Wahenga walisema, usipoziba ufa utajenga ukuta, baba wa taifa, hayati Mwalimu Nyerere alisema ukisikia wanaopaza zaidi sauti za udini ndiyo wanaoueneza, kwa hiyo tuwe makini na wanaopiga kelele juu ya jambo hilo.

“Katika suala hili, ni vema Bunge litafute namna bora ya kushughulikia suala hili ili lisiendelee kuwa kikwazo kwa amani ya nchi yetu” alisema Wassira

"KUTOVAA NGUO ZA NDANI HUSUSANI KWA WANAWAKE NI KUJIDHALILISHA"....SHILOLE




IMEBAINIKA kuwa baadhi ya wasanii wa kike nchini hawavai nguo za ndani kwa madai kwamba joto linawaumiza na kuwasababishia michubuko katika baadhi ya sehemu za mwili wao

Hali hiyo ya kutovaa nguo za ndani inasababishwa na wasanii hao kutaka kupata hewa na kuepuka kubanwa kwa madai kuwa wanahitaji kuwa huru zaidi na mavazi wanayovaa huku baadhi ya sehemu zao za mwili kuonekana vizuri

Hayo yalibainishwa jijini Dar es Salaam juzi  na msanii wa filamu pamoja na muziki wa miondoko ya miduala Zuwena Mohamed 'Shilole' alipokuwa akizungumza na jarida hili ....Shilole alisema kuwa kutovaa nguo za ndani hususani kwa mtoto wa kike ni kujiaibisha na kujishushia heshima katika jamii

Alisema kuwa wapo wasanii ambao hawavai nguo za ndani kwa madai kuwa wanaogopa kuchubuka jambo ambalo yeye aliliona si sahihi hivyo na kudai kuwa tabia ya kujirahisisha katika maswala ya ngono ndiyo inayopelekea kuvaa bila nguo yoyote ndani

"Unajua kiukweli ni kujishusha thamani hauwezi kukaa bila ya kuvaa nguo ya ndani tena mtoto wa kike ni kujidharilisha hata kama ni kuiga tusifikie huko jamani"alisema Shilole

Pamoja na hayo aliongezea kuwa sababu nyingine inayosababisha wasanii hao kubaki utupu ni kuonyesha viungo vya mwili wao jinsi walivyoumbika jambo ambalo yeye aliliita ni njia moja wapo ya kujidharilisha na kuutangaza uhuni kwa jamiii

"Kama hauna makalio makubwa huna tuu hata usivae nini hayaonekani hivyo ni bora ujistili kama mtoto wa kike"alisema Shilole

Alipoulizwa kuwa na yeye ni miongoni mwa wasanii wanaokaa utupu Shilole alisema kuwa amelelewa katika mazingira ya kuvaa nguo mbili kabla haujavaa ile inayoonekana na jamii hivyo hawezi kutoka nyumbani bila ya kuvaa nguo ya ndani

Kwa upande wake mwanamitindo Joketi Mwegelo alisema kuwa wasanii hao wanaovaa nguo bila ya kuvaa za ndani wanatakiwa kujistiri na kwenda na mazingira ili waendelee kulinda heshima yao kwa jamii

Alisema kuwa kama mtoto wa kike ni vyema ukafuata maadili na mazingira ya nchi hivyo basi kukaa utupu ni moja ya kujidharilisha na kushusha soko lako katika sehemu yako ya kazi na kuchangia kupunguza mashabiki ambao kwa namna moja au nyingine unaweza kuwapoteza kutokana na tabia

HII NDO LAANA INAYOTENDEKA MOMBASA......NASIKIA HUKO HADI WANAUME HUJIUZA




The 21st century generation seems to have thrown all caution and the respectable ways that the forefathers fought so hard to see their children grow up with are no longer there.

In Mombasa at some night clubs this is what goes down.

SPIKA WA BUNGE AWAKAANGA TENA WALE WABUNGE WALIOTIMULIWA BUNGENI.....







Leo asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu Mh Spika ametoa uamuzi kuhusu muongozo ulioombwa na Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kuhusu uhalali wa kutolewa nje na kisha kufungiwa vikao vitano kwa wabunge sita (6) wa Chadema uliotolewa juzi na Naibu Spika.
 Mh Spika anasema kwa kuwa kwa sasa hakuna kanuni kuhusu jambo hilo uamuzi wa Naibu spika utabaki halali na utaingizwa kwenye kumbukumbu za bunge kwa ajili ya kutumika huko mbele kwa ajili ya maamuzi pale itakapotokea tukio kama hilo.

Kwa uamuzi huo Wabunge hao watakosekana bunge bunge kwa siku tano ambazo ni Alhamisi (jana), Ijumaa (leo) pamoja na Jumatatu, Jumanne na Jumatano wiki ijayo.


Uamuzi wa Naibu Spika Mh. Job Ndugai, wa kumtoa nje Mh. Lissu na wengine  watano na kupewa adhabu ya kutoshiriki vikao vitano vya Bunge umebarikiwa na Mheshimiwa Spika..
 Hivyo Basi, Maamuzi ya Mh. Ndugai, yatakua Kanuni Rasmi kwa Tukio kama Hilo Na adhabu iliyotolewa.
Photo
Taswira ya vurugu zilizotokea bungeni dodom

MPENZI WANGU ANATOKWA HAJA KUBWA WAKATI WA TENDO..NAOMBENI USHAURI






Habari ndugu  mwandishi....

Natanguliza  samahani  kama  nikuwakwaza  kwa  namna  moja  au   nyingine.Kuna tatizo  kuwa  sana  linalomkabili  mpenzi  wangu .

Kulipeleka  kwa  daktari  tunaona  aibu  hivyo  nikaona  ni  bora  niombe  ushauri  kwanza  kabla  ya  kuamua  chochote.....

Ni  kama mwezi sasa nimekua na mahusiano na  huyu dada ambaye  kwa  sasa yuko chuo kikuu..

Ni dada mwenye sifa zote za kuitwa mwanamke.Nishakutana nae  kimwili kama mara nne hivi   na  mwisho ilikua jana usiku...

 Cha ajabu na kinachonishangaza ni kuwa wakati wa tendo ilikuwa  ni lazma atoe haja kubwa  japo si kwa wingi....

Nimejaribu kuchunguza kama ni mdau wa 0718 lakini anaonekana si muumini wa hayo mambo...

Nilipomuuliza kama ashawai bakwa siku za  hivi  karibuni amekataa,au kama ashawahi kutumia 0718  napo  kagoma...



Mwenyewe pia eti hajui ni kwa nin imekua hivyo na anasema hali hiyo imemuanza wakati yuko na mimi....

Ni kitu  ambacho  kimenichanganya   sana...Nimemuomba  amuone  daktari  amegoma  kabisa  kwa  kuogopa  aibu.

Nifanyaje  jamani..!!  

HII NDO AIBU YA ZITTO KABWE NA HALIMA MDEE







Wakati Bunge la Tanzania likiendelea kufukuta kwa  vurugu na kauli za matusi na dharau, Wabunge hawa  Zitto Kabwe na Halima Mdee wamefunguka juu ya mambo yanayoendelea bungen kupitia mitandao ya kijamii  na  kudai  kuwa  na  aibu  isiyoelezeka.

Wanadai kuwa Bunge  limekosa  mwelekeo  na  kwamba  kwa  sasa   hawaoni  haja  ya  kuendelea  kuitwa  wabunge

MWANACHUO AVULIWA NGUO NA KUPEWA KICHAPO KIKALI BAADA YA KUIBA VIATU

 Mrembo  huyu  aliyejitambulisha  kwa  ni mwanafunzi  wa chuo  kikuu  kimojawapo mjini Iringa akilia baada ya kupokea  kichapo kutoka kwa mwanamke mfanyabiashara  eneo la Miyomboni mjini Iringa baada ya  kuiba viatu  vya mtumba na kuficha kwapani
Hapa  akimpigia  simu mpenzi  wake  ili aweze kumkomboa baada ya  kutakiwa  kulipa Tsh 50,000 kwa viatu pea mbili alizoiba .

----------------------------------------------------
Tukio la mrembo  huyo  kupokea  kichapo na kuvuliwa  nguo na  kupokonywa  simu yake na mikoba zaidi ya mitano  pamoja na kiasi cha TSh 15,000 ambazo alikuwa amezihifadhi limetokea  jumapili  wiki hii katika  eneo la Miyomboni mjini Iringa.

Akielezea juu ya mkasa  huo  wa aina yake  leo mfanyabiashara   huyo  mama Masawe  alisema kuwa eneo  hilo amekuwa na kawaida ya  kuibiwa  viatu katika  duka  lake la viatu  vya mtumba .....

Mama  huyu  anadai    kuwa  mbali ya  kukamatwa kwa mrembo  huyo  bado amepata  kukamata  vijana  zaidi ya  wawili watanashati ambao  wamekuwa wakifika na kujifanya wakichagua viatu na  kuishia  kuiba na kutoweka .

Binti   huyo ambaye  ni  mwanachuo   alifika  dukani hapo   na  kuanza kuchagua  viatu akijifanya  ni  mteja .....
Baada  ya  kuona  muuza  duka  ameangalia  pembeni, binti  huyo   alichukua  pea  moja  ya  viatu  na  kuificha  kwapani  asijue  kwamba  pembeni  kulikuwa  na  mtu  mwingine  aliyekuwa  akimwangalia....
Alipoaga na  kutaka  kuondoka ndipo timbwili la  kichapo  lilipoanza kwa mrembo huyo ambae aliomba asipelekwe  polisi  na  asipewe  adhabu  kubwa  kwa  kuwa   ana ujauzito  wa miezi mitatu tumboni.

Alisema  kuwa  kutokana na maombi ya mrembo huyo  kupunguziwa adhabu  hakuweza kumfikisha  polisi  zaidi ya kumpa kichapo  cha kufa mtu na kumpokonya  mali  zote alizokuwa ametoka  kuiba katika maduka ya  Miyomboni mjini hapa pamoja na  simu  yake ya kiganjani .

MAZISHI YA BI KIDUDE:... UMATI MKUBWA WAJITOKEZA KUMSINDIKIZA






Tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi 

Jeneza la bibi likielekea msikiti kwa ajili ya kusaliwa

Mtangazaji Hassan Bond, Fid Q, Diamond Platnumz na Ruge Mutahaba wakiwa msibani nyumbani kwamarehemu bi Kidude,  Zanzibar


Msanii Fid Q, Baraka cousin ya Marehemu Bi Kidude na Hassan Bond Mussa (FID Q ndo alikuwa msanii wa kwanza mkubwa kufika msibani kwa bibi)

Ruge mutahaba, Babu Tale and Guru. .......msibani kwa Bi Kidude

Guru G na Mh Bhaa mazikoni

Hassan na Fid Q wakiwa katika picha ya pamoja na familia ya Marehemu Bi Kidude

Sehemu ya umati wa Watu waliofika msibani