Monday, April 8, 2013
TANZANIA YAONGOZA KWA UNYWAJI WA POMBE CHAFU MAARUFU KWA JINA LA MATAPUTAPU....
Utafiti wa Kituo cha Habari cha Marekani CNN, umebainikwambaTanzania ni nchi ya sita barani Afrika kwa watu wake kunywa pombe chafu (mataputapu).
Utafiti huo wa Machi 23 mwaka huu, ulibaini kwamba Uganda inaongoza kwa kunywa pombe chafu maarufu kama Luwombo kwa asilimia 14.52 ikifuatiwa na Rwanda kwa asilimia 6.44.
Kwa mujibu wa utafiti huo,Tanzania inashika nafasi ya tano kwa kuwa na asilimia 4.52,ikiwa nyuma ya Burundi yenye asilimia 5.07.Ivory Coast imekuwa nyuma ya Tanzania kwa kuwa asilimia 3.55 huku Tanzania ikiipiku Burkina Faso iliyoambulia asilimia 3.77, kwa wa watu wake kunywa pombe chafu.
Ripoti ya utafiti huo ilisema asilimia kubwa katika nchi za Afrika, wanapenda kutumia pombe kali kwa lengo la kuondoa msongo wa mawazo.
Mtaalamu wa masuala ya afya katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Kitengo cha Figo, Dk Francis Fulia aliwataka wananchi waache kunywa pombe hizo kwa sababu zinatengenezwa katika mazingira ambayo si salama.
Alisema hali hiyo inahatarisha usalama wa afya zao.“Watanzania waachane na matumizi ya pombe hizo kwa kuwa zinatengenezwa katika njia sizisokuwa salama, pia zinasababisha magonjwa mbalimbali kama figo, ini,moyo ,kupata upofu ama kupoteza maisha,” alisisitiza.
Dk Fulia pia alipinga juu matumizi ya pombe katika kuondoa msongo wa mawazo.“Pombe haina uhusiano wowote katika kupunguza mawazo,inatumika katika kumsahaulisha mtu tatizo lake kwa kipindi kifupi” alisema.
Aliongeza kuwa njia salama ya kuepuka msongo wa mawazo ni kusuluhisha kwa kutafuta chanzo cha msongo huo au kupata ushauri nasaha kutoka katika vituo mbalimbali vya afya.
Katika miaka ya hivi karibuni,kumekuwa na matukio ya wananchi kujitumbukiza katika unywaji pombe uliokithiri ikiwamo kunywa pombe aina ya virobo gongo na pombe nyingine
BARUA YA ZITTO KABWE INAYOMTAKA "LWAKATARE ATIMULIWE CHADEMA" YAZUA BALAA
CHADEMA TAIFA VIPANDE VIPANDE! SOMA BARUA HII YA ZITTO
zitto kabwe ameandika barua kwa katibu mkuu dr slaa akitaka mambo mawili yafanyike ..
1.Lwakatare achunguzwe na chama
2.Lwakatare ajiuzulu nyadhifa zote alizokuwa nazo ndani ya chama
3. Ushauri huu usipofanyiwa kazi atafanya maamuzi magumu yatayokigharimu chama zaidi.
Taarifa zaidi kutoka ndani ya vyanzo zinaeleza kuwa kitilla mkumbo naye ameandika barua kama ya zitto lakini yeye anataka lwakatare atoswe kwa sababu ameshachafuka ili kukinusuru chama...
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa ushauri huu umesababisha mtafaruku na mgawanyiko mkubwa ndani ya uongozi wa taifa kwani baadhi wanapinga ushauri na wengine wanaunga mkono.
Wanaopinga wanadai kuwa lwakatare alikuwa kazini hivyo lazima chama kimlinde hadi dakika ya mwisho..
Hata hivyo,Leo Zitto Kabwe amezijibu tuhuma za barua hii akiadai kushangazwa jinsi barua hii ilivyovuja na kuishia kusema kuwa kuna kirusi ndani ya chama chao
Source:Jamii Forums
Source:Jamii Forums
CHID BENZ AZINGUANA NA PRODUCER LUCCI BAADA YA KUTAKA KUREKONDI WIMBO BURE
Rapper Chidi Benz na producer Lucci wameingia kwenye mgogoro baada ya kutofautiana katika makubaliano ya wimbo walioufanya pamoja. Chidi anamlaumu Lucci kwa kubadilisha msimamo wake ambapo alidai kumfanyia wimbo huo bure.
Chidi Benz na Lucci wametumia Twitter kulizungumzia suala hilo kama ifuatavyo:
Chidi Benz: Unachofanya c sawa.usipindishe maneno na usifoc makubaliano.siku tunarekod hukusema khs mkwanja,ulisema tufanyeni kazi.u mi n kk
Lucci: Ofisi na simu zipo, KWELI kuna haja ya kuhusisha watu zaidi ya 7,000? Kwani walikwepo tukifanya kazi? B professional and call me
Chidi Benz: Unahisi hio ni point koz unajaribu kutafuta points.tym tunarekod ulitweet na ukifurahia.mnakimbiliaga huku mwisho.mimi m real. Professional ni wewe kuchange deal,hatuna lazima ya hio kazi but haukua mpango uliopangwa,tumetumia energy.Tamaa imekubadilisha.
Lucci: Kwani mimi sijatumia energy?!? Mara ngapi nimekuambia uje ofisini tuandikishane makubaliano? Hata vya BURE hua na maandishi.
Chidi Benz: Hakukuwa na bure,hatukutaka koz hatukuingia na force kwenu wala hatukuvunja mlango.thou ulituelekeza studio ilipo.Nakuona…
Lucci: Ulitumiwa email ya mkataba na ofisi yangu @TransforMaX_R HUKUJIBU wala hukusema terms unazotaka. JE, nifanye lipi la ZIADA?
Chidi Benz: Unafanya kazi ndio unapewa mkataba au unapewa mkataba kisha unafanya kazi? KK ananambia khs mkataba na mi sina mail. Studio ipo kwenu ndani chumbani I thnk pale,unahisi mtu anaweza toka Ilala na hajui terms zako?hajui anakuja kufanya nini?
Lucci: Cha msingi ni mkataba, na hicho ndiyo kilio changu. Chumbani, Jikoni, kote kazini.
Chidi Benz na Lucci wametumia Twitter kulizungumzia suala hilo kama ifuatavyo:
Chidi Benz: Unachofanya c sawa.usipindishe maneno na usifoc makubaliano.siku tunarekod hukusema khs mkwanja,ulisema tufanyeni kazi.u mi n kk
Lucci: Ofisi na simu zipo, KWELI kuna haja ya kuhusisha watu zaidi ya 7,000? Kwani walikwepo tukifanya kazi? B professional and call me
Chidi Benz: Unahisi hio ni point koz unajaribu kutafuta points.tym tunarekod ulitweet na ukifurahia.mnakimbiliaga huku mwisho.mimi m real. Professional ni wewe kuchange deal,hatuna lazima ya hio kazi but haukua mpango uliopangwa,tumetumia energy.Tamaa imekubadilisha.
Lucci: Kwani mimi sijatumia energy?!? Mara ngapi nimekuambia uje ofisini tuandikishane makubaliano? Hata vya BURE hua na maandishi.
Chidi Benz: Hakukuwa na bure,hatukutaka koz hatukuingia na force kwenu wala hatukuvunja mlango.thou ulituelekeza studio ilipo.Nakuona…
Lucci: Ulitumiwa email ya mkataba na ofisi yangu @TransforMaX_R HUKUJIBU wala hukusema terms unazotaka. JE, nifanye lipi la ZIADA?
Chidi Benz: Unafanya kazi ndio unapewa mkataba au unapewa mkataba kisha unafanya kazi? KK ananambia khs mkataba na mi sina mail. Studio ipo kwenu ndani chumbani I thnk pale,unahisi mtu anaweza toka Ilala na hajui terms zako?hajui anakuja kufanya nini?
Lucci: Cha msingi ni mkataba, na hicho ndiyo kilio changu. Chumbani, Jikoni, kote kazini.
UNYAMA: BABA AWANYONGA WATOTO WAKE WATATU NA KISHA KUWATUPA KISIMANI PAMOJA NA MAMA YAO
UKATILI wa kusikitisha! Watoto watatu wa famila moja, wameuawa kikatili kwa kunyongwa huku mama yao akishuhudia. Miili yao pamoja na mama yao akiwa hai, wakatumbukizwa katika kisima cha maji. Baba wa watoto hao, Justine Albert (24) anatuhumiwa kufanya unyama huo.
Kabla ya mauaji hayo, inadaiwa baba huyo alimfunga kamba mkewe na kumziba mdomo kwa kitambaa ili asipige kelele, kisha akaanza kuwanyonga watoto wake wote watatu kwa zamu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, alisema mauaji hayo ya kikatili yalifanyika juzi saa 11:30 alfajiri katika Kijiji cha Majimoto, Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Mlele mkoani humo.
Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, kisa cha kufanya mauaji hayo ni mzozo wa mtuhumiwa na mkewe, Jacqueline Luvika (21), kwamba baadhi ya watoto hao mama huyo kazaa na jirani yao.
Watoto hao ni Frank Justine (6), Elizabeth Justine (4) na kitinda mimba Maria Justine, mwenye umri wa miezi minne.
Baada ya kuwanyonga watoto hao, inadaiwa baba huyo alibeba miili ya watoto Frank na Eliza, na kwenda kuwatumbukiza kwenye kisima cha jirani yao, Kawaida Jonas.
Kwa mujibu wa madai ya Kamanda Kidavashari, mtuhumiwa baada ya kuwatumbukiza watoto hao kisimani, alimfungua kamba mkewe na kumtoa kitamba alichomziba mdomoni, kisha akamburuta hadi kwenye kisima hicho na kumtumbukiza.
Kugundulika Baada ya matukio hayo yanayodaiwa kufanyika alfajiri, kulipopambazuka baadhi ya wakazi wa kijiji hicho, waliodamka kwenda katika shughuli zao, waliuona mwili wa mtoto ukiwa umetelekeza kando ya njia na kutambua kuwa ni Maria, ambaye ni kitindamimba katika familia hiyo.
Inadaiwa wakazi hao walisitisha safari yao na kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa, kumpatia taarifa hiyo ya kuhuzunisha, huku wakiuliza mama wa mtoto aliko.
Kamanda Kidavashari alidai mtuhumiwa aliwaeleza wakazi hao kuwa mama wa mtoto huyo, alikuwa ametoroka kwenda kusikofahamika na watoto wote.
Majibu hayo ‘rahisi’ kwa mujibu Kamanda Kidavashari, yalisababisha wakazi hao wamtilie shaka mtuhumiwa, wakaamua kutoa taarifa kituo cha Polisi kijijini hapo, ambao walifika ulipo mwili wa mtoto Maria.
Wakati wakiwa katika eneo la tukio, Kamanda Kidavashari alidai walibaini alama za mburuzo ardhini, wakaanza kuifuatilia na zikawafikisha kisimani. Walipofungua mfuniko wa kisima hicho, walishtuka kuona miili wa watu watatu, ikielea kwenye maji kisimani humo.
Askari Polisi kwa kushirikiana na wakazi wa kijiji hicho, waliopoa miili yote, lakini watoto hao wawili tayari walikuwa wamefariki, huku mama yao akiwa amekunywa maji mengi na kupoteza fahamu.
Kutokana na hali hiyo, wakazi hao walipandwa na hasira na kwenda kuvamia nyumba ya mtuhumiwa na kumkamata ili wamchome moto. Hata hivyo, Kidavashari alisema polisi walifanikiwa kufika kwa wakati katika eneo hilo na kumwokoa mtuhumiwa, ambaye kwa sasa bado ameshikiliwa Polisi kwa mahojiano.
Mama wa watoto hao kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, alikimbizwa katika Kituo cha Afya cha Kijijini cha Mamba wilayani humo, ambako amelazwa kwa matibabu, lakini hadi jana bado alikuwa amezirai. Mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara tu baada ya uchunguzi wa awali wa shauri lake kukamilika.
TUKIO ZIMA LA WACHAWI WAWILI WALIODONDOKA NA UNGO HUKO KAHAMA- SHINYANGA
WAZEE WANAOSADIIWA KUWA NI WACHAWI WAKIWA CHINI YA ULINZI KITUO CHA POLISI,KUTOKA KUSHOTO NI MWAJUMA MPONI (70) NA KULIA NI SHIJA NKWABI (80)
Watu wawili wamenusurika kuuwawa usiku wa kuamkia juzi katika kijiji cha Mhongolo wilaya ya kahama mkoani shinyanga, baada ya kukutwa katika mazingira yanayodaiwa kuwa ya kishirikina.
Watu hao waliojitambulisha kwa majina ya Mwajuma Mponi (70) wa Nduku, na Shija Nkwabi(80) wa Nyashimbi wilayani humo, wameanguka kijijini hapo wakitokea kijiji cha nduku wiyani humo wakielekea Nyihogo Kahama kwa shughuli za kishirikina.
Katika maelezo yao wazee hao wamedai kuwa wameanguka baada ya kutokea ajali ya kishirikina huko angani, ambapo waligongana na wenzao ambao hawakuwafahamu walikotoka na walikokuwa wanaelekea.
Sambamba na hayo imeelezwa kuwa wazee hao walikuwa uchi wakati wakianguka kabla ya kusaidiwa nguo na mama mmoja wa maeneo ya Kafe Latino barabara ya Mhongolo.
Jeshi la Polisi la Wilayani humo likiri kutokeakwa jambo jambo hilo na kwamba uchunguzi bado unaendelea na taarifa zitatolewa baadaye.
WAZEE WAKIWA HOI,HUKU WA KUSHOTO AKIWA ANATEMA MATE OVYO KITUONI HAPO.
HAPA AKITEMA MAPOVU HUKU AKISEMA ANA NJAA SANA.
BIBI AKIWA AKIWA HOI BAADA YA KUDONDOKA USIKU WA LEO
HAPA BIBI AKISAIDIWA KUINUKA BABADA YA KUVALISHWA NGUO NA WASALIMIA WEMA.
ASKARI POLISI WAKIWASAIDIA KUWAPANDISHA KWENYE GARI.
HAPA WAKIPELEKWA KITUO CHA POLISI
MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA MAJIRA PATRICK MABULA AKICHUKUA MAELEZO TOKA KWA MASHUHUDA WALIOSHUHUDIA TUKIO HILO.
HAPA NDIPO ENEO AMBALO WACHAWI HAO WALIPODONDOKEA.
Tabia za Msichana Anayekupenda Kimapenzi Lakini Hawezi Kusema
2. Haoni aibu kugusa sehemu yako ya mwili. Msichana anayependa haoni aibu kukushika mkono ama kukutomosa au hata kukumbatia. Kwa kufanya hivyo hujua kuwa kwa asilimia kubwa hisia za kushikana kwenu kutamrahisishia kazi ya kuwa na wewe
3. Kucheka kwa nguvu hata kwa kitu kisicho chekesha endapo wewe umezungumza. Mara nyingi ataonesha uso wa furaha hata kama si furaha ya kweli
4. Wivu.
Hujisikia wivu anapokuona na wasichana wengine. Ukiwa unachart nao na ukiwaita majina ya kimahaba. Hapendi.
5 anakumbuka siku zako muhimu. Hukumbuka kama vile siku yako ya kuzaliwa hatowez kuisahau kufanya ipite bila kukutakia heri ya siku ya kuzaliwa kama sivyo ukifaulu mtihani au chochote katika maisha yako atakuwa mbele kukupongeza
6. Eye contact anapenda kukuangalia machoni muda wote ambao mtakuwa mkizungumza pamoja akidhani kuwa utaelewa ni kiais gani anakupenda kupitia vile ambavyo anakuangalia.
Ila wengine huona aibu kuwatazama wavulana wanaowapenda si wote wana ujasiri wa kuwatazama wapenzi wao.
7. Hupenda kukaa mmuda mwingi na wewe. Hawezi kupoteza hata sekunde ukimuhitaji kwa mazungumzo. Anajisikia furaha kukaa na wewe muda mrefu bila kuchoka. Anaweza akaacha kila kitu anachokifanya ili ajumuike na wewe.
8. Yupo tayari kuangamiza. Kama msichana anakupenda yupo tayari kusacrifice. Ni kitu ambacho hakuna mtu ambaye anaweza akafanya kwa mtu mwingine. Utaona vipi huyo msichana alivyo kwako na wa wengine. Yaani yupo tayari yeye akose lakini wewe upate na kwa mwingine anaweza akamwamba hana alichoombwa lakini akakupa wewe kama pesa na vitu vingine.
9. Anachukulia matatizo yako kama ni yake. Unapomueleza kuwa ana tatizo anajali tatizo lako kama vile ni lake na hujisikia vibaya sana na kuhuzunika na atafanya lolote ili aweze kukusaidia utoke katika hilo tatizo.
10. Mikwaruzano ikitokea katika urafiki wenu hayupo tayari kukupoteza kabla hajakuambia anakupenda. Kwa kuwa anakupenda endapo ikatokea mikwaruzano basi atafanya juu chini kuyaweka mambo sawa ili asikukose
Subscribe to:
Posts (Atom)