Monday, April 8, 2013

MAKUNDI YA WANAUME NA MITAZAMO YAO YA KIMAPENZI KWA WANAWAKE



MDAU wa safu hii, leo ni siku nyingine ya Jumatatu ambapo tunakutana katika kilinge chetu cha XXLove tunachokitumia kuhabarishana masuala ya mapenzi hususan kuboresha ndoa kwa waliooana. Hebu tuendelee na mada hii ya Makundi ya wanaume na mitazamo yao ya kimapenzi kwa wanawake, utajifunza kitu...
Hazina iliyopo ndani ya mwanamke/mwanaume bora anayeonekana ana sifa mbaya, inaweza kuvumbuliwa na mtu mwerevu, mvumilivu, anayeamini katika kufundisha. Yule mwenye imani kwamba kila mbaya, ndani yake kuna historia ya kuumiza.

Pengine mwanamke/mwanaume amekuwa na hulka mbaya kwa…
MDAU wa safu hii, leo ni siku nyingine ya Jumatatu ambapo tunakutana katika kilinge chetu cha XXLove tunachokitumia kuhabarishana masuala ya mapenzi hususan kuboresha ndoa kwa waliooana. Hebu tuendelee na mada hii ya Makundi ya wanaume na mitazamo yao ya kimapenzi kwa wanawake, utajifunza kitu...
Hazina iliyopo ndani ya mwanamke/mwanaume bora anayeonekana ana sifa mbaya, inaweza kuvumbuliwa na mtu mwerevu, mvumilivu, anayeamini katika kufundisha. Yule mwenye imani kwamba kila mbaya, ndani yake kuna historia ya kuumiza.
Pengine mwanamke/mwanaume amekuwa na hulka mbaya kwa sababu ni majeruhi wa uhusiano mbaya. Huko nyuma aliingia kwenye uhusiano na wanaume/wanawake pasua kichwa. Naye kichwa chake kikapasuka mpaka akayachukia mapenzi, hivyo kuanza kuishi kama kicheche.
Mapenzi pasua kichwa yamemfanya awe waluwalu wa mtaani. Sasa basi, mtu wa aina hiyo, anaweza tu kurejea kwenye hali bora ya kimapenzi kama tu atampata mwenzi bora wa maisha, atakayemfanya ajitambue alipo na kujikosoa kwa kuanza kushika njia sahihi.
Atakayemfanya agundue kwamba kumbe yale mapenzi pasua kichwa, yalisababishwa na wapenzi pasua kichwa aliokuwa nao. Kwamba siyo watu wote wana tabia hizo, kwani wengine Mungu amewapa utulivu na ubora utadhani malaika ndani ya dunia.
Wanaume wa kundi hili wanajitosheleza kimaadili. Umakini na busara zao za kufundisha ndiyo chachu ya kuwageuza wale wanawake ambao awali walionekana wameshindikana, hadi kuwa wake bora, hivyo kujenga uhusiano imara na familia yenye afya.
Ni mara chache sana kuwakuta wameteleza. Ikitokea, huwa hivyo kwa sababu nao ni binadamu, kwa hiyo hawana ukamilifu wa asilimia 100. Hata hivyo, ubora wao huonekana waziwazi kutokana na jinsi wanavyokuwa na makosa machache, vilevile wanavyojisahihisha mapema, pale wanapokosea.
TATHMINI YAO KIMAPENZI
Nyoyo zao huwa hazisemi uongo kuhusu hisia zao za kupenda. Hutulia mahali walipo bila kutetereka. Maisha yao siyo ya mitego, kwa maana hutawakuta wakijishughulisha kufuatilia nyendo za wenzi wao ili kujua makosa yao au kubaini kama wanawasaliti.
Wanajua kunyenyekea pale inapostahili wanyenyekee, kadhalika huwa hawachukui uamuzi wa papara hata pale wanapohisi kwamba wenzi wao watakuwa wanafanya usaliti. Umakini wao, huwafanya waonekane kuwa viumbe waliobarikiwa zaidi.
Wanaweza kuhisi kitu kinachokaribiana na ukweli lakini watapuuza kwa vile hawana ushahidi. Ni waangalifu sana kuzungumza au kufanya mambo ambayo yanaweza kuwakera wenzi wao. Siyo wabinafsi, huwekeza furaha zao kwa kuhakikisha wenzi wao ni wenye furaha.
Imani yao ni kwamba wenzi wao wanapokuwa na furaha ndipo nao wanaweza kufurahi. Ukiwafuatilia utagundua kwamba marafiki hawachukui nafasi za wapenzi wao. Hawapo kama wale ambao wanatumia muda mwingi vijiweni au baa na marafiki na kuwaacha wenzi wao wakiwa wapweke.
Ni hodari wa kuzingatia mzani. Maisha yao hayana longolongo. Ikitokea wakatekwa na Shetani, hivyo kutengeneza nyumba ndogo, huwa hawahamishi mapenzi yote nje. Huendelea kuwajibika ndani ya familia zao kwa nidhamu na ufanisi wote unaotakiwa.
Kuna wanawake wa pembeni ambao huanzisha uhusiano na wanaume wa watu wenye sifa zinazowafanya waunde kundi hili.

No comments:

Post a Comment