Sunday, June 2, 2013

MABADILIKO: MWILI WA NGWEA UTALETWA JUMANNE NA SIYO KESHO



 Mwili wa ngwea  utaletwa Tanzania siku ya jumanne  na  siyo  kesho ...

Taarifa hizi nikwa mujibu wa tweet alotweet Millard Ayo aliyeko nchini africa kusini ulipo mwili wa marehemu Ngwair

"TANZANIA HAIWEZI KUIOMBA RADHI NCHI YA RWANDA"......BENARD MEMBE



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema kamwe Tanzania haitaiomba radhi Rwanda, baada ya Rais Jakaya Kikwete kuishauri nchi hiyo kufanya mazungumzo na upinzani ili kumaliza vita katika eneo hilo la Maziwa Makuu.
 
Serikali ya Rwanda iliitaka Tanzania iombe radhi kwa madai kuwa kauli ya Rais Kikwete ni kama tusi kwao na kwamba wao hawawezi kukaa na kuzungumza wapinzani ambao ni wauaji.
 
“Kama Rwanda haitaki kufuata ushauri wa Rais Kikwete inatakiwa kuuacha na siyo kumtaka aombe radhi,” alisema.
 
Membe alitoa ufafanuzi huo bungeni jana wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika mjadala wa makadirio ya matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka 2013/2014.
 
Tamko hilo la Serikali limekuja ikiwa zimepita takriban siku sita tangu Serikali ya Rwanda kutoa tamko la kupinga ushauri huo uliotolewa na Rais Kikwete wakati akiwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU), uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia.
 
Akijibu pendekezo hilo la Rais Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo alisema kuwa Rwanda haiko tayari kufanya mazungumzo na watu ambao walishiriki kwenye mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, dhidi ya Watutsi na kwamba kufanya hivyo ni sawa na kuhalalisha mauaji kwa wananchi wake.
“ Wale wote wanaodhani kuwa Rwanda itaanzisha majadiliano na waasi wa FDLR nadhani kwa ukweli hawajui kile wanachozungumza. Rwanda haiwezi kujadiliana na wauaji,” alisema waziri huyo wakati akizungumza na Idhaa ya Kimataifa ya Radio Ufaransa.
 
Alisema kuwa wakati serikali ya Rwanda imefaulu kuzika mienendo inayopalilia mauaji ya halaiki, lakini bahati mbaya kumesalia makundi ya watu ambayo bado yanahubiri itikadi zinazokumbusha uchungu na kutonesha kidonda kilicholeta maafa makubwa kwa wananchi.
 
“ Kumbe kuna wasemaji wengi wa kundi la FDLR. Wengine wao wanaendelea kufungamana na itikadi za kundi hili. Rwanda ilifaulu kutokomeza mauaji ya halaiki lakini hatukutokomeza itikadi za kundi hili,” alisema waziri huyo.
Kauli ya waziri huyo imeungwa mkono na baadhi ya wasomi pamoja na wanaharakati waliosema kuwa kuiomba Rwanda ianzishe majadiliano na kundi hilo, wanapaswa kufikiri mara mbili.
 
Katika ufafanuzi wake Membe alimnukuu Waziri Mkuu wa zamani wa Israel, Isaack Rabin kwamba mwaka 1995 aliwahi kutoa tamko lililosema, ‘Tunajenga amani na tunajadiliana na maadui zetu na si marafiki’.
 
Alisema kama Serikali ya Rwanda itakuwa imesikia kauli hiyo inatakiwa kufanya mazungumzo ya amani na maadui, na wasingoje kufanya mazungumzo ya amani na Tanzania, ambayo wana uhusiano mzuri na ni nchi rafiki kwa muda mrefu.

“Sijui kwa nini wanaliepuka suala hili. Israel na Palestina wanazungumza, sasa wao ni nani mpaka wakatae kufanya mazungumzo? Sasa watapigana mpaka lini wakati wameshindwa kutatua tatizo hilo kwa miaka 16?” alihoji Membe na kuongeza;
 
“Sijui kwa nini wanaona aibu kufanya mazungumzo na upinzani. Ningependa serikali ya Rwanda ijue kuwa kwa tabia yetu tangu uhuru tunatoa kipaumbele kwa mazungumzo ya amani. 

 Tumekwenda katika kikundi cha M23 na tumemhimiza Rais Yoweri Museveni wa Uganda afanye mazungumzo.”

HUDDAH TOKA KENYA AYAAGA MASHINDANO YA BIG BROTHER..... MWAKILISHI WA TANZANIA ALIA NA WAVUTA BANGI


Maneno  huumba....!!!  Huddah  ameliaga  shindano hilo...
------------------------
Huddah ambaye ni mshiriki kutoka Kenya   alijikuta akibubujikwa na machozi  jana wakati akimuelezea Angelo (SA) kuhusiana na uhusiano wake wa kimapenzi ambao ni wa ku-beep yani vuta nikuvute ambao amekuwa nao nchini kwao.

Mrembo huyo hakutaja jina la mpenzi wake lakini inahisiwa alimaanisha kuwa katika mahusiano na Rapper Prezzo wa Kenya. Kwa muda sasa kumekuwa na umbea mtaani kuhusiana na uhusiano wa kimapenzi kati ya wawili hao lakini haijafahamika kinaga ubaga kama Huddah alimaanisha kum-miss Mr. President. ..

Mrembo huyo akizidi kufunguka, alielezea jinsia anavyo-miss mabusu motomoto, anavyo-miss kung'atwa shingoni n.k. “I miss the way that he kisses me. I miss him biting my neck”.. 
LEO  MACHOZI  YAKE  YAMELIPWA  BAADA  YA  MREMBO HUYO  KUONDOLEWA  NDANI YA  JUMBA  HILO....Mashabiki  wamepiga  kura  ya  kumwondoa  ili  asiendelee  kumlilia  mpenzi wake.....
Mshiriki mwingine  aliyeaga  mashindano  hayo  ni  Denzel wa Uganda....

KWA UPANDE MWINGINE, mrembo wa Tanzania ,Feza anayeiwakilisha Tanzania alijikuta katika simanzi kali wakati alipoelezea kuhusu jinsi ambavyo kaka yake aliteseka kutokana na kujihusisha na madawa ya  kulevya .. 'drugs'.
Feza alitumia fursa hiyo kuwasihi watu hasa vijana kujiepusha kabisa na madawa ya kulevya kwani ni hatari sana katika jamii inayotuzunguka..

WABUNGE WANASWA KATIKA DANGURO LA UCHI MJINI DODOMA....WALIKUWA WAKITOA PESA KWA KUZIWEKA MAKALIONI



Katika ukumbi maarufu wa muziki au kwa jina jingine ‘club’ (jina linahifadhiwa) uliopo mjini  Dodoma mengi yanatokea.

Watu wanaingia mmoja mmoja, wengine kwa makundi na baadhi wapo nje wakipunga kwanza upepo kabla ya kuingia.

Siku hizi wanawake wanaingia bure au kwa jina jingine ‘ladies free’jambo linalosababisha ukumbi huu ufurike watu.
Katika ukumbi huu, yapo maeneo mawili. Kuna sehemu ya kawaida ambayo kiingilio chake ni kuanzia Sh5,000 hadi Sh10,000 kutegemeana na matukio au burudani ya siku hiyo.
Pia kuna eneo jingine ambalo ni kwa watu maalumu ama waweza kusema ni ‘VIP’ ambapo wateja wake hutakiwa kulipa Sh20,000.
Ukumbi wa VIP upo juu na ule wa kawaida upo chini. Hata hivyo maeneo yote haya hujaza watu kwa kiasi kikubwa.

Mwandishi wetu alifika katika ukumbi wa VIP saa tano usiku, hata hivyo bado watu ni wachache katika eneo hili ukilinganisha na kule kwa watu wa kawaida.


Ukumbi wa VIP si mkubwa kieneo . Kuna kaunta ya vinywaji, makochi madogo madogo aina ya sofa yenye meza mbele yake, viti vilivyoizunguka kaunta na katikati ya ukumbi huu kuna meza mbili za duara zenye mti wa chuma katikati.
Kadri dakika zinavyojongea, ndivyo watu wanavyoendelea kumiminika mmoja baada ya mwingine.
Saa saba za usiku ndipo Mwandishi wetu  aliposhuhudia kiongozi mmoja wa kitaifa ambaye hekima zake zinategemewa na Serikali na hata chama chake akiingia katika ukumbi huu akiwa na mabinti wadogo watatu.

Alipata nafasi ya kuketi, katika moja ya sofa zilizokuwa katika ukumbi huo, akaagiza vinywaji na kuendelea kunywa.

Muda wa saa saba, alitokea msichana aliyevaa sidiria na kisketi cha kujimwaga kifupi sana ambacho hata hivyo kiliuonyesha mwili wake waziwazi.
Msichana yule alipanda katika moja ya meza za duara zenye chuma na kuanza kucheza muziki uliosikika katika spika za ukumbi huo.
Baada ya kucheza kwa zaidi ya nusu saa, alivua kisketi cha rangi nyeusi alichokivaa na kukirusha… akabaki na nguo ya ndani aina ya ‘bikini’ ya rangi nyeupe, kisha akaendelea kucheza kwa kupandia vyuma katika meza hizo za duara. 

Baadaye alivua sidiria, akaendelea kucheza na kadri watu walivyokuwa wakimtunza fedha aliendelea kuonyesha ujuzi wake katika kucheza.
Baada ya muziki huo kukolea, msichana huyo alibadilisha mchezo, akalala kifudifudi na kuishusha nguo yake ya ndani hadi nusu ya makalio yake.
Wanasiasa waliokuwepo katika ukumbi huo pamoja na watu wengine walionekana kumpa fedha kwa kumwekea katikati ya makalio msichana huyo kadri walivyofurahishwa na uchezaji wake.
Wakati huohuo mwanasiasa mwingine kijana aliingia ukumbini hapo akiwa na rafiki zake na kuendelea kushuhudia dansi hiyo.
Baada ya kucheza kwa saa kadhaa, msichana yule alishuka katika meza, kisha akapanda msichana mwingine na kuendelea kucheza.
Aliposhuka, aliingia katika choo cha wanawake na kurudi akiwa amevaa suruali aina ya jeans na tisheti. Wanaume waliokuwa eneo hilo walimwita na kumpongeza, huku wakimnong’oneza maneno ambayo…yalikuwa siri yao.
Chanzo chetu cha habari kinaeleza kuwa wasichana hao ni raia wa Kenya ambao wanadaiwa kuwapo nchini kwa ajili ya kucheza dansi za aina hiyo.
“Wanafanya kazi ya kuhudumia wateja hapo kaunta, lakini unapofika wakati wa kucheza wanacheza,” kinasema chanzo hicho.
Kinaeleza kuwa pamoja na kulipwa kiasi cha fedha kama mshahara na wamiliki wa ukumbi huo, wasichana hao wanajipatia fedha wanazotunzwa wakati wa kucheza.
Chanzo kingine cha habari kinaeleza kuwa wasichana hao ni muunganiko au jumuiya ya vijana waliotoka nchi jirani kuja kufanya biashara hiyo ambayo imeshamiri nchini mwao.
Chanzo hicho kinaeleza kuwa, si wanasiasa hao waliokuwapo siku hiyo pekee, bali wanasiasa wa kiume kadhaa wenye majina nchini hufika hapo kutazama wanawake wachezao utupu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Hassan Ngwilizi, Mbunge wa Mlalo (CCM) anasema kwa kuwa wamefanya jambo hilo nje ya Ukumbi wa Bunge hivyo, hawastahili kuhukumiwa bali sheria inatakiwa kuwabana kama wananchi wa kawaida.

Hata hivyo, anasema kitendo hicho ni kinyume cha maadili na hakitakiwi kufanywa na viongozi kama hao.

Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe anasema sheria za nchi haziruhusu kumbi za starehe kuajiri watu wanaocheza utupu. Waziri Chikawe ambaye pia ni Mbunge wa Nachingwea anasema ni aibu kwa viongozi kutazama dansi za namna hiyo na baya zaidi kuwatuza fedha wachezaji.

“Wanapowatunza fedha, ni kama wanasifia hicho kitendo, ni kama wanasema hivi ndivyo inavyotakiwa” anasema Chikawe na kuongeza:

“Hata hivyo, wanapata wapi leseni za kuendesha huduma kama hizo?”

Anasema Tanzania ni nchi inayozingatia maadili ndiyo maana siku za karibuni Bunge lilipiga marufuku ‘kanga moko’ licha ya hao wacheza utupu.

Anaongeza: “Viongozi wanaotakiwa kuwa mfano wa kuigwa wanapoangalia dansi hizo, wanaendelea kumong’onyoa maadili”

Waziri Chikawe aliahidi kuzungumza na naibu wake, Angela Kairuki ili kuchukua hatua stahiki kwa klabu zinazoruhusu wasichana kucheza uchi.