Monday, April 29, 2013

Jihadhari Kufanya Ngono Kwenye Fukwe za Bahari Dar-Ona Hawa Wamekamatwa Coco Beach Wakifanya yao






NI aibu sana! Ndivyo unavyoweza kusema juu ya Oparesheni ya Fichua Maovu iliyosimamiwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar, OCD Wilbroad Mutafungwa na Ofisa wa Oparesheni, Inspekta Jacob Swai kwa kushirikiana na Global Publishers iliyonasa wanawake wanaojishughulisha na mambo ya ngono usiku kucha.

Katika oparesheni hiyo iliyofanyika usiku wa Jumapili iliyopita watu kibao walinaswa hasa katika Ufukwe wa…

NI aibu sana! Ndivyo unavyoweza kusema juu ya Oparesheni ya Fichua Maovu iliyosimamiwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar, OCD Wilbroad Mutafungwa na Ofisa wa Oparesheni, Inspekta Jacob Swai kwa kushirikiana na Global Publishers iliyonasa wanawake wanaojishughulisha na mambo ya ngono usiku kucha.

Katika oparesheni hiyo iliyofanyika usiku wa Jumapili iliyopita watu kibao walinaswa hasa katika Ufukwe wa Coco, jijini Dar akiwemo bibi harusi mmoja na mtoto wa kigogo (jina linahifadhiwa).

BIBI HARUSI LAIVU KWENYE BAJAJ
Kwenye ufukwe huo, mwanamke mmoja ambaye jina halikupatikana, aliyedaiwa kufunga ndoa Ijumaa iliyopita, naye alikamatwa katika msako baada ya kunaswa na mwanaume wakifanya ngono kwenye Bajaj.

Katika tukio hilo, mwanaume alifanikiwa kutoka nduki huku akimwacha demu wake akijikusanya kwa kuvaa nguo.
Mwanamke huyo naye alifanikiwa kuwatoka askari hao na kukimbilia chooni ambapo aliwakuta wanawake wengine waliojificha hivyo wakakamatwa wote kwa pamoja.
Ili kuweka ushahidi, askari hao wa kazi waliikamata Bajaj hiyo.

ALIKWENDA KUKUMBUSHIA ENZI ZAKE
Kwa mujibu wa mwanamke huyo, mkazi wa Kinondoni-Manyanya, usiku huo alifika mahali hapo kukumbushia enzi zake kabla ya kuolewa ambapo ilidaiwa kwamba alikuwa akijiuza ufukweni hapo.
Alijitetea kuwa mume wake alisafiri hivyo akaona akakumbushie enzi zake kabla hata ‘hina’ aliyopakwa wakati wa harusi haijafutika mwilini.
Pamoja na maelezo hayo, mwanamke huyo aliishia kwenye ‘difenda’ la polisi tayari kwa kupelekwa kituoni kwa maelezo zaidi.

BINTI WA KIGOGO
Katika kundi hilo la wanawake na wanaume zaidi ya hamsini waliokamatwa ufukweni hapo usiku huo wa saa 9 na ushee, kulikuwa na mtoto wa kigogo mmoja serikalini katika idara nyeti ambaye alinaswa mchangani baharini akiwa kwenye kundi la makahaba.
Mtoto huyo aligundulika kuwa ni binti wa mnene wakati wa kutoa maelezo kituoni Oysterbay.

MASIKINI ALIKUWA NA ‘BOIFRENDI’ WAKE
Akijitetea wakati wa kutoa maelezo, binti huyo aliyeonekana mrembo na mwenye mvuto wa ajabu, alisema kwamba alikuwa na ‘boifrendi’ wake na kuwa alitoroka kwao usiku huo.
Binti huyo aliomba chondechonde asipigwe picha kwani endapo itaonekana gazetini basi atakuwa amejipalia makaa nyumbani kwa vile hataeleweka kwa sababu anapatiwa fedha za matumizi pamoja na ada ya shule.
Ukiacha mwanamke na binti huyo wa kigogo, wanawake wengine wengi walikamatwa, wengi wao walikutwa wakifanya vitendo vya ngono mchangani wakiwa ‘pea’.

MACHANGU WAFUNGUKA
Kati ya wote waliokamatwa, wanawake kumi na tano walikiri kujishughulisha na biashara ya kuuza miili ambapo walisema wanafanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha.
ACD MUTAFUNGWA ANASEMAJE?
Kwa upande wake OCD Mutafungwa alisema wameamua kuyafanyia kazi malalamiko ya wananchi kwa kuvamia eneo hilo.

INSPEKTA SWAI ATIA NENO
Naye Inspekta Swai aliyekuwa ‘front’ katika zoezi hilo alisema kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu kila wiki ili kukomesha vitendo viovu katika ufukwe huo.

JB ATANGAZA NIA YAKE YA KUGOMBEA UBUNGE MWAKA 2015........HIKI NDO ALICHOKISEMA




HATIMAYE nguli wa sanaa za maigizo Bongo, Jacob Stephen Mbura ‘JB’ amelianika jimbo atakalogombea ubunge mwaka 2015.


JB aliyaongea hayo mwanzoni mwa wiki hii, jijini Dar es Salaam ambapo alisema macho yake yote yapo Mkoa wa Dar es Salaam ambao una majimbo nane.


JB: Niliposema natangaza kugombea ubunge mwaka 2015 wengi waliamini ni maneno tu, lakini nia yangu ni sahihi. Nitagombea na leo nasema jimbo langu lipo Mkoa wa Dar es Salaam.


Aliongeza kuwa, jimbo atakalogombea litaendelea kubaki kuwa siri ya moyo wake na meneja wake wa kampeni ambaye hakupenda kumtaja jina.


Majimbo yanaounda mkoa wa Dar es Salaam katika uwakilishi bungeni ni Ukonga, Ilala, Kinondoni, Segerea, Kawe, Kigamboni, Ubungo na Temeke.

MAANDAMANO MAKUBWA YANAENDELEA JIJINI ARUSHA BAADA YA GODBLESS LEMA KUACHIWA HURU




Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ameachiwa kwa dhamana hivi punde baada ya kushtakiwa kwa makosa ya uchochezi katika mahakama ya Mkoa wa Arusha huku maandamano yakifanyika hivi sasa katika mitaa ya Jiji la Arusha, Tanzania.

Katika Mahakama hiyo kulikuwa na umati mkubwa wa wafuasi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Mashabiki, wafuasi na wanachama wa chama hicho walifurika katika mahakama hiyo kwa ajili ya kumuunga mkono mbunge huo.habarimasai.com itaendelea kukuletea Taarifa zaidi baadaye.
 
Hivi sasa mashabiki, wafurukutwa na wanachama wa Chadema wanafanya maandamano makubwa kuelekea katika ofisi za chama hicho ambazo zipo katika eneo la Ngarenaro.

Hivi sasa wanapita katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mulongo kwa maandamano huku wakipiga kelele za kuzomea.

Kesi ya uchochezi dhidi ya Lema imefunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa wa Arusha na endeshwa na Hakimu Devota Msoffe.

Mwandishi wetu anasema kwamba kesi hiyo imeahirishwa mpaka Mei 29 mwaka huu. 

Katika hati ya mashtaka ambayo ipo katika mahakama hiyo inasema kwamba kosa la Lema ni ' kutoa maneno yanayodaiwa kuwa ni uchochezi. 

Endelea kuwa nasi  kwa taarifa moto moto.

PADRI WA KANISA KATOLIKI HUKO MOSHI AFUMANIWA LIVE NA MKE WA MTU AKIWA UCHI WA MNYAMA



KANISA Katoliki Jimbo la Moshi limeingia katika kashfa nzito baada ya padri wake, Father Urbanus Ngowi wa moja ya parokia zake kudaiwa kufumaniwa na mwanamke anayesemekana ni mke wa mtu

Father Ngowi akiwa ameduwaa baada ya kufumaniwa akiwa na mke wa mtu aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.
Sakata la fumanizi hilo linadaiwa kutokea Jumatatu ya wiki iliyopita chumbani kwa padri huyo, Marangu Wilaya ya Moshi  Vijijini ambako Father Ngowi inasemekana alikutwa ‘laivu’ akiwa na mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.

Pamoja na kunaswa huko, vyanzo havijaeleza humo chumbani wawili hao walikuwa wakifanya nini!


Habari zinadai siku ya tukio, mwanamke huyo aliingia nyumbani kwa padri huyo ambapo baadhi ya ndugu wa mumewe walikuwa wakimfuatilia baada ya madai yaliyokuwepo kwamba ana ukaribu wenye maswali mengi na mtumishi huyo wa Mungu.


“Unajua siku nyingi ilivuma kwamba Mama P na Father Ngowi wana ukaribu wenye maswali mengi, mume wake alifuatilia na kubaini ni kweli lakini akashindwa kuutenganisha ukaribu wao,” kilidai chanzo.

Father Ngowi akijaribu kuomba samahani baada ya kufumaniwa.

Chanzo kikaendelea kudai kwamba baada ya kuona mkewe amejikita kwa mtumishi wa Mungu, mumewe alinyoosha mikono juu na kumwachia Mungu.

Chanzo: Sasa siku hiyo baada ya ndugu wa mume kumfuatilia mpaka anaingia kwa Father Ngowi, wakaona ni bora watafute mpigapicha ili kupata picha za tukio ambazo zitakuwa ushahidi siku za mbele.


“Walipompata wakazama ndani, sekeseke likaanzia hapo. Walimkuta mwanamke huyo na mtumishi wa Mungu wapo kitandani.”

 
Father Ngowi na Mama P wakivaa nguo zao kwa aibu baada ya kufumaniwa.

Habari zinadai kwamba kufuatia tukio hilo, tayari Kanisa Katoliki limemweka kitimoto padri huyo ambaye alikuwa akihudumu katika Parokia ya Korongoni, Moshi Vijijini kabla ya kuhamishwa na kupelekwa Parokia ya Makomu, Marangu ambako inadaiwa ameshushwa cheo.


Inadaiwa kuwa baada ya tukio hilo, Father Ngowi alikana kukutwa na mke wa mtu chumbani kwake lakini alipobanwa sana na mabosi wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Moshi, alikiri na kudai ibilisi alimpitia na kuomba kanisa limsamehe na kutompa adhabu kali ambayo itamuathiri kisaikolojia.


Hili ni tukio kubwa na la aina yake kuwahi kulikumba Kanisa Katoliki nchini kwa padri wake kudaiwa kukutwa na mke wa mtu chumbani kwake!

Father Ngowi na Mama P wakiwa na nyuso za aibu baada ya tukio hilo.

Kuna madai kwamba mwaka jana (2012), Father Ngowi, mbele ya waumini wake alisoma barua yenye kukana shutuma zote zilizoelekezwa kwake kwamba amekuwa na ukaribu wenye maswali mengi na wake za watu.


Taarifa zilidai kuwa padri huyo aliweka wazi akisema si kweli kwamba amekuwa na ukaribu unaotajwa, akawataka waumini wake wapuuze tuhuma hizo alizosema  zina mwelekeo wa kuchafua sifa yake na taswira ya Kanisa Katoliki kwa jumla.


Hayo ni madai ya vyanzo vyetu ambavyo viliambatanisha na picha mbalimbali za tukio hilo lenye kushtua waumini sambamba na namba za simu za padri huyo kwa ajili ya mawasiliano ili kujiridhisha.

 Father Ngowi akipatiwa suruali yake.

KITENDO CHA WANAWAKE KUNYONYANA NDIMI HUKU WAKIWA NUSU UCHI KIMEMFANYA PREZZO AIPITIE UPYA VIDEO YAKE




Inaonekana baadhi ya vituo vya runinga nchini Afrika Kusini, zikiwemo Channel O na Soundcity zimetaka video mpya ya Prezzo, Liqher ifanyiwe marekebisho kadhaa ili vianze kuicheza.
Prezzo 5

Hiyo ni kwa mujibu wa mawasiliano kwenye mtandao wa Twitter kati ya msichana aitwaye Tricia Stever anayetumia jina GOLDIE 4EVER GOLDEN aliyetaka kufahamu kwanini video hiyo haioni ikichezwa kwenye vituo hivyo.

“Pls y is d video for #liqher not being shown on soundcity, channel o n other music channels @amb_prezzo #justcurious,” aliuliza msichana huyo jana.
Prezzo akiwa kwenye jacuzzi
Prezzo akiwa kwenye jacuzzi
Wanawake wakionesha vitendo vya usagaji
Wanawake wakionesha vitendo vya usagaji
Wanawake wakinyonyana ndimi kwenye video hiyo
Wanawake wakinyonyana ndimi kwenye video hiyo
Prezzo 5
Prezzo alijibu, “Working on it, had 2 make sme changes……if u know wht I mean.”

“Yeah i understand but pls try n hasten it up, cos dat video is dope n d whole of africa need to watch it,” alitweet Tricia.
prezzo 2
prezzo 3
Prezzo 4
Video ya Liqher inamuonesha Prezzo katika baadhi ya scenes akiwa kwenye Jacuzzi na wasichana walio nusu utupu na wengine wakinyonyana ndimi.

 Katika sehemu zingine anaonekana msichana mrembo akijig’ata vidole vyake kimahaba na hivyo kuamsha hisia kali .