Tuesday, May 28, 2013

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA KOSA LA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA WA MIAKA 7


MKAZI wa kijiji cha Turiani, Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, Athuman Rashid (25) amehukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela na adhabu ya kuchapwa viboko sita baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka saba. 
Hukumu hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Korogwe, Arnold Kirekiano.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyosomwa na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Janson Zakaria alidai Athuman alitenda kosa hilo Juni 21 mwaka jana, saa 11.00 jioni katika kijiji cha Turiani wilayani hapo. 
 
Hati hiyo ya mashitaka inadai Athuman alimuita mtoto huyo ambaye alikuwa akiishi na bibi yake kijijini hapo kwa lengo la kumtuma dukani ndipo alipomtendea unyama huo. 
 
“Alipokuwa akifanyiwa tendo hilo mtoto huyo alipiga kelele na baadhi ya majirani kujitokeza kufika eneo hilo huku, mtoto huyo akilalamika kwa maumivu sehemu ya siri na akimtaja mtuhumiwa,” alidai Zakaria. 
 
Kabla ya Hakimu Kirekiano kutoa hukumu alimtaka mshitakiwa kama ana chochote cha kujitetea aeleze mahakamani; naye akasema hana cha kujitetea, Mahakama iamue. 
 
Hakimu alisema kifungo hicho cha maisha jela na viboko sita, iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

No comments:

Post a Comment