Tuesday, May 28, 2013

AIBU: KIJANA ANASWA AKIUZA UUJME WA MTU....POLISI WATIA MBARONI



Jeshi la polisi nchini malawi wanamshikilia kijana mmoja baada ya kumkuta akiuza sehemu ya siri ya mwanaume.

Kijana huyo mwenye miaka 24 alikamatwa baada ya wananchi kutoa ripoti kituo cha polisi kuwa kunamzee kalala relini huku akiwa anatokwa damu nyingi 
 Polisi walifika eneo la tukio na kumkuta mzee huyo akiwa hoi na kuamua kumkimbiza hosipitali.

Baada ya kufikishwa hosipitali, madaktari  gundua kuwa mzee huyo alikuwa amejeruhiwa kwa kukatwa sehemu zake za siri...

Madaktari hao walilipoti kwa maofisa hao wa polisi na ndipo msako mkali ulipo pita katika wilaya ya Lakeshore mjini Salima na polisi hao kufanikiwa kumtia mbaroni kijana huyo baada ya kumkuta  akiwa katika gesti bubu akijaribu kuuza uume huo kwa dola za kimarekani 360.
  Mtuhumiwa Samuel Banda

Polisi walisema mtuhumiwa Samuel Banda alikamatwa na kiungo hicho ambacho alikuwa amekifunga katika karatasi nyeupe.

Mtuhumiwa alikiri kuwa huwa anauza viungo mbalimbali vya binadamu kwa wafanya biashara maarufu nchini humo ambao wanaamini wakivipata viungo hivyo huwasaidia katika biashara zao na huwaongezea utajiri.

No comments:

Post a Comment