Monday, May 27, 2013

JACK WOLPER ALIA NA MATAPELI YANAYOTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KWA JINA LAKE KUOMBA HELA WATU



Katika kile kinachoonekana ni mwendelezo wa matapeli wa mjini kutumia majina ya waigizaji maarufu nchini kutapeli watu kwa njia ya mtandao, dhahama hii sasa imemkuta mwanadada Jacqueline wolper baada ya watu wanaoaminika kuwa ni matapeli kutumia jina lake kujipatia fedha na vitu vingine kiudanganyifu.

Akizungumza kwa simu na tovuti ya bongomovies, mwanadada Jacqueline wolper  alisema matapeli hawa sasa wameamua kutumia mtandao wa instagram na mtandao mwingine wa kijamii uitwao badoo kwa jina la “wolper gambe25” katika kutapeli watu kwa kuwaomba hela au michango mbalimbali kupitia account hizo feki

“Leo nilikuwa naenda saluni, baada ya kufika tuu, yule dada wa saluni akaanza kunilalamikia kuwa mbona sijaenda kuchukua viatu nilivyomuagiza pamoja na hela? 

  
Nikawa sijui cha kumwambia maana sikumuagiza viatu na wala sijampigia simu kumwambia anitumie hela, ndipo aliponionesha huo ujumbe kwenye simu yake na ndio nikagundua hizo account feki za hao watu wanaoutumia jina langu kutapeli watu” Alisema Jack.

“Mimi sipo facebook na wala sitarajii kujiunga, nawaomba sana mashabiki wangu wajue hilo. Natumia mtandao wa instagram kwa jina la wolpergambe au jacklinewolperjacklinewolper.”
 Alisisitza Wolper

Pia alisema kuwa amegundua leo kuna mtu mwingine anayetumia jina lake kuomba watu wamchangie kuhusu kampeni inayoitwa“Zinduka” na amewataka sana mashabiki wake wasije wakafanya hivyo kwani mtu huyo ni mwizi na analengo la kumchafulia jina lake.

HII NI NEEMA KWA WALIOFELI KIDATO CHA NNE....UFAULU WAONGEZEKA, MATOKEO NI MUDA WOWOTE


Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu, Mwananchi limebaini.

Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.

Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.

Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.

Msemaji wa Necta, John Nchimbi alisema upangaji wa matokeo hayo ulikuwa bado unaendelea. “Ninachojua kwa sasa ni kuwa mchakato unaendelea na matokeo yatatangazwa mapema tu ili watoto waweze kujiunga na shule mapema,” alisema Nchimbi.

Pia alisema usahihishaji wa mitihani ya kidato cha sita umekamilika.

Matokeo ya awali

Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1.

Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.

Hata hivyo, habari kutoka Necta zinasema kuwa licha ya kuwezesha kuongezeka kwa waliofaulu, matumizi ya kanuni mpya ya kukokotoa matokeo hayo yalisababisha zaidi ya wanafunzi 2,500 kushuka ufaulu ikilinganishwa na awali.

Maofisa mbalimbali wa Necta pamoja na wale wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na taasisi zake, walikutana mwishoni mwa wiki iliyopita kukubaliana masuala mbalimbali juu ya matokeo hayo pamoja na suala la matokeo ya wanafunzi hao 2,500 kabla ya kutangazwa wiki hii.

“Baada ya wajumbe kujadili suala lile, busara ilibidi itumike kwa hiyo hakuna mwanafunzi ambaye alama yake itashuka, kwa kawaida isingewezekana mtoto ambaye matokeo yalitoka akiwa amefaulu leo umwambie ameshuka,” kilieleza chanzo chetu.
Matokeo ya awali ndiyo chimbuko la kupitiwa upya baada ya wadau kuyalalamikia na kumlazimisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuunda tume ya kuyachunguza Februari 23, mwaka huu.
Kabla ya tume hiyo kuhitimisha shughuli zake, ilitoa taarifa ya awali ambayo ilipendekeza kufutwa kwa matokeo hayo kwa maelezo kwamba Necta ilitumia kanuni mpya ya kukokotoa matokeo bila kushauriana na wadau.
Serikali ilitoa taarifa bungeni kwamba imeamua kufuta matokeo ya 2012 na kuamuru yapangwe upya kwa kufuata madaraja yaliyotumika mwaka 2011.

RIHANNA IMEKULA KWAKE..!!!!! ...KARRUECHE TRANS SASA AHAMIMIA NYUMBANI KWA CHRIS BROWN




Siku zote mwenye kiu iliyopitiliza akipewa maji ya kunywa hutamani atumie jagi zaidi ya kikombe anachowekewa maji, ndivyo ilivyomtokea mrembo Karrueche Tran aliyetoswa mwaka jana na Chris Brown aliyemchagua Rihanna dhidi yake wakati mrembo huyo akiwa na moyo uliojaa mapenzi na maumivu ya kulikosa penzi la ‘turn up the music singer’..
Sasa alipopewa nafasi tena ameamua kuitumia vyema na katika kupunguza zaidi umbali ameamua kuhamia kabisa nyumbani kwa mwimbaji huyo. 


Kwa mujibu wa TMZ Chris na Karrueche wamekua wakiishi pamoja nyumbani kwa muimbaji huyo Los Angeles tangu walipoonekana pamoja kwenye sherehe ya kuzaliwa Chris Brown alipotimiza miaka 24. 
Ripoti zinasema mrembo huyo amehamishia nguo zake na vitu vyake takribani vyote kutoka kwake na kuvipeleka nyumbani kwa Chris Brown lengo ni kuwa karibu zaidi na mwimbaji huyo. 

Rafiki wa karibu wa KT ameuambia mtandao wa Hollywoodlife kuwa karrueche anajaribu kuweka commitment katika mahusiano yake na Chris ambayo mwimbaji huyo hawezi kuitunza lakini ameamua kujiweka kwenye mstari huo kwa ajili ya mahusiano yao. 

Chanzo hicho kiliongeza kuwa Karrueche anampenda Chris kwa sababu wanaendana na anapenda upande mwema wa Chris Brown. 

Inawezekana Karrueche hamhofii tena Rihanna kwa kuwa mwaka jana alilazimika kuisomba mizigo yake kutoka kwenye nyumba ya mwimbaji huyo baada ya kumwagwa na himaya yake kuchukuliwa na RiRi bila sababu za msingi isipokuwa Chris kuamua tu kumrudisha RiRi. 


Kwa sasa Chris na Rihanna hawako pamoja tena na Karrueche anaonekana kukaba nafasi yake vizuri. Swali, je hii pembe tatu ya mapenzi yaliyojaa drama itaishia hapo au baadae itambidi KT aondoe tena mizigo yake kumpisha Rihanna?

PENZI LA WASTARA LAGOMBANIWA.....



TAKRIBAN  wiki moja baada ya kumaliza eda tangu alipofariki mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Januari 2, mwaka huu, staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma anagombewa na midume ikitaka kumuoa.


Akizungumza na mwandishi wetu  akiwa nchini Oman, Wastara alifunguka kuwa tangu amalize eda yake hiyo amekuwa akipata usumbufu mkubwa kutoka kwa wanaume mitandaoni na wanaomtamkia mwenyewe.

“Jamani mpaka nahisi kuchanganyikiwa kabisa, wanaume zaidi ya mia tano hata sijui walipotokea wanataka kunioa, hadi nahisi majanga,” alisema Wastara.

Wastara alisema kuwa wanaume hao wamekuwa wakihangaika bure kwa sababu kwa sasa hafikirii kabisa kuolewa kwani anapotembea bado anasikia harufu ya mumewe Sajuki.
 
“Bado harufu ya Sajuki ipo mwilini mwangu, wanaume wanaonitolea macho mtoto wa mwenzao wanakosea sana, sifikirii kabisa suala hilo kwa sasa,” alisema Wastara mwenye mtoto mdogo aliyezaa na Sajuki.

LWAKATARE AKWAMA TENA KUPATA DHAMANA, KESI YA JAYDEE YARUSHWA MPAKA JUNE 13.

LWAKATARE AKWAMA TENA KUPATA DHAMANA, KESI YA JAYDEE YARUSHWA MPAKA JUNE 13.

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfred Lwakatare na mwenziye Ludovick Joseph wamekwama tena leo Jumatatu, Mei 27 kupata dhamana baada ya Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Kisutu, Sundi Fimbo kueleza kuwa Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Aloyce Katemana, bado yupo likizo tangu wiki tatu zilizopita.
  
Watuhumiwa wanakabiliwa na shitaka la kupanga njama za kumnywesha sumu Mhariri wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky.

Lady Jay Dee akiwa na mumewe Gardner Habash wakisuburi kesi kutajwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kindondoni leo asubuhi saa tatu. 
------------------
Mwanamuziki Judith Wambura-Habash --Lady Jay Dee-- alifika katika mahakama ya Kinondoni leo kama ilivyotakiwa kwa mashitaka aliyofunguliwa hapo. Baadaye amefahamisha kuwa ameambiwa ardui tarehe 13 Juni 2013.
Kesi imetajwa tena tar 13 June 2013. Saa 5 asub.