Friday, June 7, 2013

PICHA ZA MAANDALIZI YA JUKWAA LA KILL MUSIC AWARDS......TUKIO LITARUSHWA LIVE MTANDAONI



Kesho ndio siku yenyewe ambayo wasanii waliotajwa kuwania tuzo za mwaka huu za muziki wa Tanzania, Kilimanjaro Tanzania Music Awards, KTMA watajua hatma yao.

 Tuzo za Kili zitatolewa kesho June 8 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. 

Hizi ni picha za jinsi maandalizi ya jukwaa na ukumbi yalipofikia.
IMG_0728
Mafundi wa TV itakayorusha matangazo live wakiweka sawa mitambo yao
IMG_0730
Sound check
IMG_0734
Hivi ndivyo maandalizi yanavyoendelea
IMG_0739
IMG_0750
Muonekano wa nje ya ukumbi
IMG_0718
Mafundi wakiziweka sawa cranes za camera

MPENZI WA ALBERT NGWEA AKILIA KWA UCHUNGU WAKATI WA MAZISHI



MAJONZI na vilio vilitawala juzi katika zoezi la kuuaga mwili wa marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’ kwenye Viwanja vya Leaders lakini mmoja wa waliotia fora katika kuangua kilio alikuwa dada mmoja mzungu anayedaiwa kuwa alikuwa Mpenzi wa Ngwea aitwaye Misheily. 


Mzungu huyo alionekana akilia kwa uchungu huku akitoa maneno yaliyoashiria kuwa ameumia sana kuondokewa na ‘mtu’ wake huyo ambaye huenda walikuwa na malengo mazuri ya baadaye.

Aidha, kilio alichokuwa akiporomosha binti huyo kiliwafanya watu waliokuwa karibu naye kumsikitikia na kuzidishiwa majonzi kwani ilifika wakati akaishiwa nguvu.


Mwandishi wetu alijaribu kumfuata na kumuomba kuzungumzia juu ya kifo cha Ngwea lakini alikataa na kusema asingeweza kufanya hivyo kufuatia majonzi aliyokuwanayo huku akionekana kutoamini kama jamaa yake huyo ametutoka

MTANGAZAJI WA TIMES FM ( KHADIJA SHAIBU) AJIANIKA "AKIKATA GOGO " CHOONI



MTANGAZAJI wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amewashangaza watu baada ya kutundika mtandaoni picha zinazomuonesha akioga bafuni huku nyingine akiwa chooni  akikata  gogo. 


Picha hizo zinapatikana kwenye mtandao wake na hakueleza ilikuwa wapi ila akasema ilikuwa ni siku alipoamua kuitumia wikiendi yake ipasavyo katika hoteli ambayo hakuitaja jina.
 
Baadhi ya watu waliyoziona picha hizo walimponda wakidai eti ni ulimbukeni lakini wapo waliomtetea kwa kusema, ni staili tu ya maisha aliyoamua kuishi.



“Ushamba tu, ndo nini sasa?  alisema mmoja wa wadau huku mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Dick akisema: “Msimuonee wivu mwenzenu, anakula bata zake na nyie hamjakatazwa.”
 
Dida alipoulizwa kuhusu kujianika hivyo alisema, hizo ni ishu zake binafsi na wapenzi wake wanapenda kuona kila anachokifanya, ndiyo maana anawawekea kwenye blogu yake.

BAADHI  YA  MAONI  YA  WATU  KATIKA  BLOG  YAKE 

BABA YAKE DIAMOND YUPO HOI ANAUMWA......DIAMOND HAJAWAHI KANYAGA KUMJULIA HALI


BABA wa msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’, Abdul Juma yupo hoi akisumbuliwa na ugonjwa wa miguu.

Kwa mujibu wa chanzo makini, Baba Diamond anasumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba hali ambayo imemfanya ashindwe kutembea lakini cha kushangaza mwanaye, Diamond hajaenda kumjulia hali.

“Baba Diamond ni mgonjwa kwa muda mrefu sana lakini Diamond hajawahi kuja kumuona hata siku moja,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, waandishi  wetu walifunga safari mpaka nyumbani kwa mzee huyo, Magomeni-Kagera, jijini Dar ambapo alikiri kuugua kwa muda mrefu na kukosa msaada kutoka kwa Diamond.

“Nasumbuliwa na miguu kwa muda mrefu sana na ninatibiwa katika Hospitali ya Saint Monica, Manzese-Darajani. Diamond ana taarifa za kuumwa kwangu lakini hajawahi kuja kuniona.

“Namshukuru mwanangu Queen Doreen kwa kunijali kwa kila kitu,” alisema baba Diamond.