Sunday, June 9, 2013

FEZA WA TANZANIA ANUSURIKA KUYAAGA MASHINDANO YA BIG BROTHER...KOKETSO NA LK4 KWAHERI


FEZA azidi kupeta mjengoni....

Mtanzania FEZA amenusurika kutoka katika jumba la biggie baada ya kuwa up for possible eviction kufuatia kuwekwa kitanzini (nominated) Jumatatu iliyopita... 
Koketso mshiriki kutoka South Africa na LK4 ambaye ni mshiriki kutoka Uganda wamekuwa washiriki wa tatu na wa nne kutoka katika jumba la Big Brother Africa baada ya Denzel na Huddah kuyaaga mashindano  wiki  iliyopita..
Hivi ndivyo walivyopigiwa kura na nchi tofauti :
Total: Hakeem = 6; Feza = 3; Dillish =3, Koketso = 2, LK4 = 1. (Total: 15 Votes)

LADY JAYDEE AMTUKANA MWANA FA KWA KUMUITA " MWANA FAtuma" HUKU AKIMTANDIKA VIJEMBE KWA KUUZA SURA JUZI


Lady Jaydee amemshambulia vibaya MwanaFA. Chanzo cha kuanza kumpa makavu Live ni pale MwanaFA alipo-Retweet post ya shabiki yake mmoja ambaye aliikejeli Show ya Jide kuwa ni Fundraising, ambapo MwanaFA aliongezea neno ‘Daaaamnnn’ kwenye Post hiyo.
 
Mambo yalizidi kuwa mabaya baada ya MwanaFA ku-Retweet post ya shabiki wake mwingine aliyedai kwamba Lady Jaydee anawalipa watu buku buku ili wamponde MwanaFA.

 Hapo ndipo mwanadada Lady Jaydee uzalendo ukamshinda baada ya kutoa warning iliyopuuziwa, akaanza kumchana MwanaFA bila woga lakini MwanaFA hakuweza kujibu kitu zaidi ya ku-Retweet posts za mashabiki wake wanaomponda Lady Jaydee na team yake. 
ILI  kuepuka kusumbuliwa na mahakama , Jide alitumia ‘MwanaFAtuma’ akimlenga MwanaFA.