Wednesday, June 19, 2013

KAHABA APEWA KICHAPO KIKALI BAADA YA KUNASWA AKIJUZA JIRANI NA MSIKITI



Kahaba  mmoja   alijikuta akiambulia kichapo kikali toka kwa vijana wa kiislamu baada ya kunaswa akijiuza karibu na msikiti wao.....
  
Tukio hilo lilishuhudiwa na wanahabari wetu majira ya usiku jirani na msikiti huo uliopo nyuma ya Corner Bar, Kijitonyama jijini Dar ambapo mwanamke huyo na wenzake walikamatwa na baadhi ya vijana waumini wa Kiislamu waliokerwa na kitendo cha wao kutoa huduma haramu ya ngono maeneo hayo.


Baada ya wenzake kufanikiwa kutoka nduki mwanamke huyo alishuhudiwa akila bakora kisha akapelekwa katika Kituo cha Polisi Kijitonyama, Dar akaunganishwa na wengine waliokamatwa usiku huo.

Ilielezwa kuwa wanawake hao wamekuwa wakiuza miili kwa wanaume karibu na msikiti huo na pembezoni mwa baa hiyo.

Ilisemekana kuwa kumekuwa na kawaida ya wanawake hao kusimama maeneo ya nyumba hiyo ya ibada na kufanya biashara hiyohuku wakichafua mazingira kwa kutupa ovyo kondomu na kujisaidia maeneo hayo.
 Wakati mwanamke huyo akicharazwa bakora, nguo ya ndani ilimvuka huku akipiga kelele kuwa hatarudia kufanya hivyo na kama akirudia basi akatwe kichwa.

Kutokana na kukerwa na vitendo hivyo, vijana hao wanaofanya ibada katika msikiti huo, waliamua  kuwatafuta vijana wa ulinzi shirikishi na kuwapa kazi hiyo ya kuwakamata na kuwacharaza bakora kisha kuwapeleka katika kituo hicho cha polisi.
 

“Tumeamua kuwakamata na kuwacharaza bakora, hawana ustaarabu wala busara hawa, wanakojoa na kutupa kondomu  hovyo, “ alisikika mmoja wa vijana hao.
  
Mmoja wa vijana hao aliyekuwa akisimamia kwa karibu zoezi hilo, aliwaambia waandishi wetu kuwa wameamua kufanya hivyo na litakuwa zoezi endelevu kutokana na wanawake hao kutokuwa wasikivu kwani kila wanapoambiwa juu ya kukaa mbali na nyumba hiyo ya ibada hawasikii.

Alisema kuwa siku moja wanawake hao walimtoa udhu muumini mmoja ambaye alikuwa akienda kuswali alfajiri baada ya kumshika na kusababisha akose kuhudhuria swala siku hiyo.



Hata hivyo, wakati mahojiano yanaendelea, mmoja wa askari waliokuwa zamu aliamuru mwanamke huyo aingizwe lokapu kusubiri kesho yake aunganishwe na wenzake kisha wapelekwe mahakamani.

Habari zilizotufikia  ni kwamba baada ya kufikishwa mahakamani na kukutwa na kosa la uzururaji, wakahukumiwa kifungo cha miezi sita jela au faini ya shilingi elfu hamsini ambapo walilipa kiasi hicho na bado wanaendelea na biashara hiyo maeneo hayo.

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA



Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetuma salamu za rambi mbali kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Magesa Muhongo kutokana na vifo vya wananchi watatu wa Mkoa huo vilivyotokea kufuatia mripuko wa bomu uliotokea juzi katika viwanja vya Soweto Jijini Arusha.

Watu wasiopungua 70 waliripotiwa kujeruhiwa wakati wa mripuko huo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi katika Kata ya Soweto wa Chama cha Demokrasia ya Maendeleo { Chadema }.

Katika Taarifa ya rambi rambi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyotumwa kwa Mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha na kutiwa saini na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alielezea kupokea kwa masikitiko na huzuni taarifa ya shambulio la kigaidi la bomu lililotokea tarehe 15 Juni mwaka 2013.

Balozi Seif alisema Taifa kwa mara nyengine tena limekumbwa na msiba wa njama za kigaidi zilizoua na kujeruhi rMkuu wa Koa wa Arusha aia wema wasio na hatia sambamba na tukio jengine linalofanana na hilo lililogharimu roho za wananchi wengine wakati wakiwa katika ibada Kanisani.

Balozi Seif alisema kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wananchi na yeye binafsi anatuma salamu hizo za rambi rambi kutokana na maafa hayo na kuwaombea marehemu malazi pema na majeruhi wapone haraka ili waungane na wenzao katika ujenzi wa Taifa.


Halkadhalika Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaiunga mkono Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika jitihada zake za kupambana na ugaidi wa aina yoyote hapa Nchini.

Alieleza kwamba SMZ na Wananchi wa Zanzibar wako pamoja na wenzao katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na maombolezo na kuwaomba wafiwa wawe na moyo wa ustahamilivu, uvumilivu na subra katika kipindi hichi.

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kutenga shilingi Milioni Mia Moja { 100,000,000/-} kama zawadi kwa kwa mtu ye yote atakayetoa Taarifa zitakazofanikisha kunaswa kwa mhalifu au watu wenye mtandao wa ulipuaji wa mabomu hapa Nchini.