Thursday, May 30, 2013

K' LYNE AWEKA WAZI UHUSIANO WAKE NA REGINALD MENGI



Kumekuwepo na Minong'ono mingi lakini hapakuwa na ushahidi wa hili mpaka mwanadada huyo alipoamua kuanika hadharani kuwa mheshimiwa Reginald Mengi ndiye baba halali wa mapacha wake wawili. 

Hongera Mmiliki  wa makampuni ya IPP bwana REGINALD mengi kwa kumiliki mtoto mkali  Jackline Ntuyabaliwe(K'lyne)  ....

Hiyo ndo Tweet ya K'lyne kwa mpenzi wake Mh. MENGI

MBINU ZA KIMAHABA ALIZOZITUMIA KARRUECHE TRAN KUUTEKA TENA MOYO WA CHRIS BROWN




Kwa kawaida mapenzi hutawaliwa na hisia za kimahaba alizonazo mtu kwa mwenziwe ama mtu anaetamani kuwa nae kama boyfriend/girlfriend wake ama mke/wake. Lakini hakukosea aliyesema mapenzi ni kama mmea unaweza kutunzwa na kustawi na ukiachwa bila matunzo unaweza kunyauka. 


Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa mrembo Karrueche Tran aliyetoswa vibaya na Chris Brown lakini kwa kuweka mikakati ya dhati na kuumwagilizia vyema mmea wa penzi kati yake na na Chris hata wakati akiwa hana muda nae na anahang out na Rihanna kumemsaidia kurudisha kwa kasi na nguvu mpya penzi alilopoteza.
 
Moja kati ya mikakati ya kimahaba aliyoitumia Karrueche huku moyoni mwake akiuamini msemo wa ‘mvumilivu hula mbivu’, ni kujiweka karibu na Chris kama rafiki hata wakati akiwa bado yuko na Rihanna na hakuonesha chuki ya wazi kwake japokuwa alikuwa anaumia sana. 


Mkakati mwingine ni kuhakikisha anaonesha moyo wa upendo wa dhati na nia ya kuwa na Chris Brown kwa kuwa alijua kabisa kuwa mwisho wa siku ataangalia zaidi anakooneshwa kupendwa na kuvumiliwa, akijua mwisho wa siku akiumizwa na kulizwa huko aliko atahitaji kufutwa machozi na kutulizwa, na Karrueche atakuwa karibu zaidi, na kweli ndicho kilichotokea.



Chanzo cha karibu na KT kimesema, “Karrueche hakuwahi kuacha kumpenda Chris, hakuwa kulazimisha kitu chochote kwake kwa upande wa mahusiano, na hakuwahi kulazimisha kupewa kitu mkononi au kuomba chochote kwake.”



Mkakati huo pia ulimuongezea alama za ushindi kwa jamaa, lakini pia alijua kabisa ya Rihanna yatapita tena, kwa imani yamepita kweli. “Alijua alikuwa bado anafanya vyote na Rihanna na alitegemea hilo na muda wote alikuwa rafiki kwa Chris Breezy hata wakati akiwa na Rihanna.” Kiliendelea kufunguka chanzo hicho.



Kwa sasa KT amehamia nyumbani kwa Chris na ripoti zinasema ni takribani nusu mwezi hivi na wanaishi kama mke na mume.

AIBU YA BIG BROTHER: VIDEO ZA MAPENZI ZAANZA KUONEKANA KATIKA NYUMBA ANAYOIONGOZA FEZA KESSY WA TANZANIA



Ikiwa ni usiku wa pili (usiku wa kuamkia leo)katika reality show ndani ya jumba la Big Brother Africa mwaka huu lilipewa jina la ‘The chace’ mambo mengi mapya yameanza kuonekana kwa washiriki ambao wameanza kufahamiana.
 
Katika hali ambayo mara nyingi haikwepeki hasa wanapokutana wanawake warembo na wanaume watanashati, scene za mapenzi zimeanza kuonekana katika Diamond house inayoongozwa na mtanzania Fezza Kessy (Head of house) ....

‘Bolt’ , mshiriki kutoka Sierra Leone na Betty ambae ni mshiriki kutoka Ethiopia walipata nafasi ya kufahamiana zaidi na kuvuka mstari wa urafiki wa kawaida wakati washiriki wengine wakiwa wamelala  ndani ya jumba la Kessy
Betty na Bolt..

Betty ambae yuko nominated pasipo yeye kufahamu, sasa yeye na Bolt ndio waliothibitishwa kuwa couple ya kwanza, japo hatima ya mahusiano yao huenda ikawa hatarini kwa kuwa jumapili hii kura za watazamaji zitaamua hatima ya Betty kuendelea kuwa katika jumba hilo au kurudi Ethiopia. 

"SITAKI KUSIKIA NYIMBO ZA NGWEA ZIKIPIGWA CLOUDS FM..WAO NDO WALIOMFANYA AANZE KUVUTA BANGI ILI KUONDOA MAWAZO"...P FUNK




Muda mfupi uliopita djchoka amepokea simu kutoka kwa Producer mkongwe hapa bongo anayejulikana kwa jina la P Fuck Majani na kumuuomba aipokee msg hii hapa chini na kuwaomba watanzania walijue hili na baadae atatoa barua rasmi.