Thursday, May 30, 2013

AIBU YA BIG BROTHER: VIDEO ZA MAPENZI ZAANZA KUONEKANA KATIKA NYUMBA ANAYOIONGOZA FEZA KESSY WA TANZANIA



Ikiwa ni usiku wa pili (usiku wa kuamkia leo)katika reality show ndani ya jumba la Big Brother Africa mwaka huu lilipewa jina la ‘The chace’ mambo mengi mapya yameanza kuonekana kwa washiriki ambao wameanza kufahamiana.
 
Katika hali ambayo mara nyingi haikwepeki hasa wanapokutana wanawake warembo na wanaume watanashati, scene za mapenzi zimeanza kuonekana katika Diamond house inayoongozwa na mtanzania Fezza Kessy (Head of house) ....

‘Bolt’ , mshiriki kutoka Sierra Leone na Betty ambae ni mshiriki kutoka Ethiopia walipata nafasi ya kufahamiana zaidi na kuvuka mstari wa urafiki wa kawaida wakati washiriki wengine wakiwa wamelala  ndani ya jumba la Kessy
Betty na Bolt..

Betty ambae yuko nominated pasipo yeye kufahamu, sasa yeye na Bolt ndio waliothibitishwa kuwa couple ya kwanza, japo hatima ya mahusiano yao huenda ikawa hatarini kwa kuwa jumapili hii kura za watazamaji zitaamua hatima ya Betty kuendelea kuwa katika jumba hilo au kurudi Ethiopia. 

No comments:

Post a Comment