Wednesday, July 3, 2013

MAHAKAMA YAWAACHIA HURU VIONGOZI WA CHADEMA BAADA YA MWIGULU NCHEMBA KUSHINDWA KUTHIBITISHA AINA YA TUSI ALILOTUKANWA


Mwita  Waitara
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mjini Singida  jana imetupilia mbali kesi iliyokuwa inawakabali viongozi wawili wa CHADEMA NduguMwita Waitara ambaye ni afisa sera na utafiti makao makuu na mshauri wa chama hicho Dk Kitila Mkumbo. 
  
Katika hukumu yake aliyeiyosoma mbele ya wakili wa washtakiwa hao Tundu Lissu, hakimu wa Mahakama hiyo Masham alisema kuwa washatakiwa hawana kesi ya kujibu kwa kuwa mashahidi wa serikali walishindwa kuthibitisha aina ya matusi yaliyodaiwa kutolewa na washtakiwa. 

Aidha, hakimu huyo alisema kwamba upande wa serikali walishindwa kumleta shahidi muhimu katika kesi hiyo Mwigulu Nchembaaliyedaiwa kutukanwa ili athibitishe kwamba yeye ndiye aliyetukanwa na namna ambavyo matusi hayo yamemuathiri. 

"Kushindwa kwa Mwigulu Nchemba kufika mahakamani ni kuonyesha kwamba ama hajui kwamba alitukanwa au hakuona kosa lolote alilotendewa na mahakama haiwezi kutoa uamuzi kwa mambo ya kuhisiwa".. alisema hakimu huyo.  

Washtakiwa walidaiwa kutenda kosa hilo tarehe 14 Julai mwaka jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ndago wilayani Iramba ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo kilikuwa na mkutano wa hadhara. 

Kesi hiyo imekuwa ikisuasua mara nyingi kwa upande wa serikali kushindwa kuleta mashahidi mahakamani na kusababisha kesi hiyo kuahirishwa mara kwa mara, jambo ambalo lilikuwa likimkera hakimu wa kesi hiyo.

MACHANGUDOA WAULAANI UJIO WA OBAMA....WANADAI HAUKUWA NA PESA IKILINGANISHWA NA ULE WA BUSH



Katika hali ilisiyokuwa ya kawaida,  machangudoa wameulalamikia ujio wa Rais Barack Obama kwa kile kinachodaiwa  kuwa  haukuwa na faida yoyote kwa kukosa dili za pesa.



" Tumesikitishwa sana na ujio wa Obama kwani tulikuwa tumejipanga kupiga hela ndefu sana .

"Bahati mbaya watu  wake tuliokuwa tunategemea kuwanasa walikuwa busy na wale  wa  mikoani  walizuiwa"Walisema akina dada hao.
 
Machungudoa hao wanadai  kuwa  kipindi cha Bush alipokuwa Rais ambaye alikaa nchini karibu wiki moja walinufaika sana ambapo wengi wao walijenga majumba kwa pesa za ziara ya Bush .

MAMA WA MIAKA 52 AKAMATWA KWENYE CHUMBA CHA MTIHANI AKIMFANYIA MTIHANI BINTI YAKE



Mwanamke mmoja mfaransa (52) amejikuta mikononi mwa polisi wa jiji la Paris katikati ya mwezi june, baada ya kukamatwa kwenye chumba cha mtihani akimfanyia mtihani wa Kiingereza mwanae mwenye umri wa miaka 19, huku akijiweka kisichana zaidi wasimshutukie.

Ripoti kutoka nchini humo zinasema mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Caroline D aliingia kwenye chumba cha mtihani akiwa amevaa skin jeans na viatu aina ya Converse ili aonekane kama mwanae.

Lakini jicho makini la msimamizi wa mtihani lilimnasa mama huyo kwa kuwa msimamizi alikua tayari alishamuona mwanae wakati anafanya mtihani wa Philosophy, kwa hiyo akamshtukia mama huyo kwa muonekano wake na sura yake ya kiutu uzima.

Msemaji wa Polisi wa Paris alisema mwanamke huyo alikiri makosa yake ya udanganyifu na kusema kuwa kiukweli yeye alikuwa anaweza zaidi Kiingereza zaidi ya mwanae.

Mwanamke huyo anakabiriwa na mashtaka ya udanganyifu na anaweza kulipa fine isiyopungua £7,000.

Lakini pia binti yake anaweza kupata msala wa kuzuiwa kufanya mtihani wowote wa kitaifa kwa muda wa miaka mitano. 

"GEREZANI KUMENIFANYA NIMJUE MUNGU VIZURI SANA"....HII NI INTERVIEW YA LULU MICHAEL



Kwa mara ya kwanza muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael aka Lulu jana alifanya interview ya kwanza tangu atoke gerezani January mwaka huu. 

Lulu aliye na muonekano wa ‘udada’ zaidi alihojiwa jana kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV kinachoendeshwa na Zamaradi Mketema.
 Katia interview hiyo, Lulu aliongea masuala mengi kuhusu maisha yake ya sasa, mipango yake na mengine lakini akidai kuwa hatopenda kuongelea suala la uhusiano wake na Kanumba kwakuwa anahisi bado hajawa tayari ila muda ukifika atafunguka mengi. Haya ni baadhi ya masuala aliyoyazungumza.

Kuhusu uzinduzi wa filamu yake mpya Foolish Age


Ninaplan kufanya uzinduzi kwaajili ya movie yangu, lengo kubwa la kufanya uzinduzi ni kwamba kwanza nitajiskia vizuri kukutana na ‘okay these are my fans’ kukutana nao sehemu moja. Kuna vitu sitaweza kuongea kwenye interview ntahitaji kuviongea mwenyewe kama mwenyewe. 



Nitahitaji watu waone baadhi ya vitu vilivyopo kwenye movie. Movie inaitwa Foolish Age. Nitaizindua chini ya kampuni ya Proen (????) Promotions Ltd na ni kampuni ambayo ndio inanimanage kwa sasa.

Kuhusu kama ana boyfriend aliyemnunulia vitu vya thamani

Watanzania wengi tulishajiwekea ile dhana kwamba ‘ukiona mwanamke amefanya kitu basi there is a man behind, yaani ni ile dhani ipo tayari ndani yetu kwahiyo hata kama mtu atastruggle kutafuta kitu chake mwenyewe lakini hiyo itakuwa ni ukweli wako na unaujua mwenyewe . 



Kiukweli ni kwamba hakuna mwanaume yeyote ambaye amenifanyia chochote till now. Nachoshukuru tu ni menejimenti yangu, kampuni ambayo nafanya nayo kazi.


 Ni kampuni ambayo inanijali, inajali kazi zangu, inajali msanii wao kwahiyo whatever I’m having, whatever I’m doing ni mimi mwenyewe, ni kazi zangu ni biashara yangu.

Uhusiano wake na Mama Kanumba na jinsi alivyompata kufanya naye movie ‘Mapenzi ya Mungu’

Kwa sasa hivi tupo kama familia kwa hiyo it wasn’t hard mimi kumpata na nilijisikia vizuri kama ntaweza kufanya naye kazi. Kuna spirit ambayo ilinivuta zaidi nifanya kazi na Mama Kanumba kuliko labda mama mwingine.

Anachomiss kwa Kanumba

Busara zake, he was a person ambaye akikuona unaenda hivi he takes you in the right way.

Kuhusu kwanini mapenzi yake na Kanumba yalikuwa siri
Ni makubaliano tu and there was no need like to let people know yaani kumfanya kila mtu ajue nadhani haikuwa na maana kwetu.

Kuhusu kwanini alinenepa alipokuwa gerezani


Labda kwasababu nilimwachia Mungu kila kitu, nilimkabidhi Mungu kila kitu so I had this peace of mind. Niliacha kwamba yeye ni msimamizi wa kila kitu. Let me confess kwamba gerezani kumenifanya nimjue Mungu vizuri sana,. 



Kumenifanya nimjue na nimwamini na kumjua na kumwamini kumetokana kwamba kuna vitu vingi vimekuwa vinafanyika like naviona hivi kwa macho na naona kabisa kwamba hapa ingekuwa mimi kama mimi ama binadamu yeyote haiwezekani...