Tuesday, May 28, 2013

CHANZO CHA KIFO CHA MSANII ALBERT MANGWEA



Ngwea akiwa na msanii M to the P jana south africa.

Hussein Original ambaye yupo Pretoria amesema Ngwear  na   M to the P  ambaye walikuwa room moja walitakiwa kurudi Tanzania leo  wakitokea  Afrika kusini..

Walipowapitia,  waliwakuta wamezima kwenye room wote wawili baada ya kuji overdose madawa ya kulevya...
 
Mpaka sasa M to the P yupo hoi  katika  hospitali ya St. Hellen  huku  msanii Ngwair  akiwa  tayari  amekwishaaga  dunia.....

Tunaendelea  kufuatilia  undani wa  tukio  hili

R.I.P NGWAIR 

Mke wa Mshikaji Wangu Aniduwaza!



Jana nimeduwazwa sana baada ya mke wa rafiki yangu kunitamkia wazi kuwa ananipenda na anataka kutoka na mimi.
Tangu nifahamiane naye miaka takribani mitano sasa tumekuwa tukiheshimiana naye sana kama mashemeji. mwaka huu akaniambia kuwa mumewe ameanza kubadilika kwa kuzidisha ulevi, kuchelewa kurudi nyumbani na wakati mwingine kulala nje na pia alizifuma meseji za mapenzi kwenye simu ya mumewe kutoka kwa mtu aliyemsave kwa jina la kiume, hivyo nimsaidie kumshauri ili abadilke ila akanionya nisimwambie kama ni yeye ndiye kaniambia.

Nilimtia moyo kuhusu hali hiyo na kumwomba awe mvumilivu na asichoke kuongea na mumewe kuhusu hali hiyo ili abadilike. Binafsi nilipata wakati mgumu wa namna gani nitamshauri jamaa bila kumtajia makosa yake na wapi nimeyapata hivyo nikashindwa hiyo kazi.
 

Mke wa jamaa akaanza kunipigia simu usiku kulalamika kila mumewe anapochelewa kurudi na wakati mwingine akinipigia alfajiri kuniambia kuwa mumewe hajarudi hadi muda huo. Niliendelea kumtia moyo ingawa mambo hayo yalikuwa ni ya kweli.
 

Cha ajabu kuanzia wiki jana amekuwa akinitumia meseji za mapenzi, nikajua ni hizi meseji ambazo watu hutumiana hivyo sikujali sana hadi pale aliponiandikia akiniambia kuwa yuko serious anataka kutoka na mimi. Sikuamini nikampigia simu kusikia sauti yake kama ni yeye kweli, ndipo aliponithibitishia kuwa yuko serious na atatunza siri na kunitunzia heshima yangu kwa jamaa kwani tayari moyo wake umeangukia kwangu.
 

Sikuweza kumjibu kitu kwa namna nilivyopatwa na mshangao. hadi sasa anaendelea kunibembeleza na kunipa mbinu nyingi za kutimiza lengo lake bila kujulikana na watu.
 

Binafsi sina lengo la kumsaliti mshikaji wangu ila nimelileta kwenu ili mnishauri nimjibu vipi huyu mwanamke ili heshima yangu kwa familia hii iendelee kuwapo na pia kusitokee chuki yoyote kutokana na kadhia hii itakayopelekea urafiki wangu na familia hii kuyumba au kupotea.

AIBU: KIJANA ANASWA AKIUZA UUJME WA MTU....POLISI WATIA MBARONI



Jeshi la polisi nchini malawi wanamshikilia kijana mmoja baada ya kumkuta akiuza sehemu ya siri ya mwanaume.

Kijana huyo mwenye miaka 24 alikamatwa baada ya wananchi kutoa ripoti kituo cha polisi kuwa kunamzee kalala relini huku akiwa anatokwa damu nyingi 
 Polisi walifika eneo la tukio na kumkuta mzee huyo akiwa hoi na kuamua kumkimbiza hosipitali.

Baada ya kufikishwa hosipitali, madaktari  gundua kuwa mzee huyo alikuwa amejeruhiwa kwa kukatwa sehemu zake za siri...

Madaktari hao walilipoti kwa maofisa hao wa polisi na ndipo msako mkali ulipo pita katika wilaya ya Lakeshore mjini Salima na polisi hao kufanikiwa kumtia mbaroni kijana huyo baada ya kumkuta  akiwa katika gesti bubu akijaribu kuuza uume huo kwa dola za kimarekani 360.
  Mtuhumiwa Samuel Banda

Polisi walisema mtuhumiwa Samuel Banda alikamatwa na kiungo hicho ambacho alikuwa amekifunga katika karatasi nyeupe.

Mtuhumiwa alikiri kuwa huwa anauza viungo mbalimbali vya binadamu kwa wafanya biashara maarufu nchini humo ambao wanaamini wakivipata viungo hivyo huwasaidia katika biashara zao na huwaongezea utajiri.

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA KOSA LA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA WA MIAKA 7


MKAZI wa kijiji cha Turiani, Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, Athuman Rashid (25) amehukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela na adhabu ya kuchapwa viboko sita baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka saba. 
Hukumu hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Korogwe, Arnold Kirekiano.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyosomwa na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Janson Zakaria alidai Athuman alitenda kosa hilo Juni 21 mwaka jana, saa 11.00 jioni katika kijiji cha Turiani wilayani hapo. 
 
Hati hiyo ya mashitaka inadai Athuman alimuita mtoto huyo ambaye alikuwa akiishi na bibi yake kijijini hapo kwa lengo la kumtuma dukani ndipo alipomtendea unyama huo. 
 
“Alipokuwa akifanyiwa tendo hilo mtoto huyo alipiga kelele na baadhi ya majirani kujitokeza kufika eneo hilo huku, mtoto huyo akilalamika kwa maumivu sehemu ya siri na akimtaja mtuhumiwa,” alidai Zakaria. 
 
Kabla ya Hakimu Kirekiano kutoa hukumu alimtaka mshitakiwa kama ana chochote cha kujitetea aeleze mahakamani; naye akasema hana cha kujitetea, Mahakama iamue. 
 
Hakimu alisema kifungo hicho cha maisha jela na viboko sita, iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

DIVA WA CLOUDS FM AMPA SUPPORT "MKE MWENZA WA KENYA " ANAYEIWAKILISHA NCHI HIYO KWENYE BIG BROTHER AFRICA


juzi (May 26) ndio ulifanyika ufunguzi rasmi wa shindano kubwa Africa la Big Brother ambalo mwaka huu limepewa jina la “The Chase”, na tayari washiriki wa nchi zote ikiwemo Tanzania wamekwisha fahamika.

Huddah Monroe a.k.a The boss lady ambaye ni model mwaka huu ndio amebeba imani za wakenya za kurudi na kitita cha $300,000 zinazoshindaniwa katika msimu wa 8 wa shindano la Big Brother “The Chase” baada ya kuchaguliwa kuiwakilisha nchi hiyo ya jirani. 
 
Siku chache zilizopita jina la Huddah limeonekana kupata umaarufu zaidi Tanzania hasa kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, baada ya binti huyo mwenye historia ya matukio mengi ya utata huko Kenya (pamoja na kujihusisha na upigaji wa picha za utupu) kujikuta anaingia katika ugomvi wa maneno na mtangazaji maarufu hapa Tanzania Loveness Love a.k.a Diva kutokana na kinachoaminika kuwa sababu ni Prezzo. 
 
Diva a.k.a mimi Kupitia akaunti yake ya twitter, juzi (May 26) aliandika tweet inayoonesha kuweka kando tofauti alizokuwa nazo na Huddah na kuahidi kumsupport kwa kutokumwandikia “shit” kama njia ya kumuunga mkono “wifi” katika BBA.

Diva amekuwa akidai kuwa na mahusiano ya kimapenzi na rapper kutoka Kenya CMB Prezzo, kitendo kilichopokelewa tofauti na mrembo Huddah ambaye pia kulikuwa na tetesi aliwahi kudate na “Liq Her” hit maker, Rapcellency, Prezzo.