Wednesday, April 3, 2013

WAZIRI MKUU AHUDHURIA MISA YA PAMOJA JIJINI ARUSHA YA KUAGA MAREHEMU WALIOFUKIWA NA KIFUSI



Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitia saini kitabu cha maombolezo alipofika mkoani Arusha leo Kuwapa pole ndugu na jamaa ambao ndugu zao wamefariki katika machimbo ya Moramu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha. Maporomoko hayo yametokea jana na kusababisha vifo vya watu13 na majeruhi wawili ambao mmoja ameruhusiwa na mwingine amelazwa katika Hospitali ya Mount Meru
Waziri Mkuu akiwa na wabunge wa Arusha na Meya pamoja na mkuu wa mkoa kwenye msiba huo mzito. Toka Kushoto ni Mbunge wa Arusha Mjini Mhe Godbless Lema, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Magessa Mulongo, Meya wa jiji la Arusha Mstahiki Gaudence Lyimo, Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari na Mbunge wa kuteuliwa Catherine Magige
Sehemu ya majeneza ya marehemu katika ibada hiyo maalumu leo
Waziri mkuu Mizengo pindaakiongea na familia, ndugu na jamaa wa marehemu walioporomokewa na moramu.
kwa picha zaidi bofya read more
Kiongozi wa dini akiombea marehemu waliofariki kwa kuporomokewa na Moramu

Waziri Mkuu akipeana mkono na Askari wa Jeshi la Wananchi (jwtz) alipotembelea eneo la tukio. 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipowasili mkoani Arusha leo Kuwapa pole ndugu na jamaa ambao ndugu zao wamefariki katika machimbo ya Moramu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha, maporomoko hayo yametokea jana nakusababisha vifo vya watu 13 na majeruhi wawili ambao mmoja ameruhusiwa na mwingine amelazwa katika Hospitali ya Maunti meru.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoka eneo la tukio katika machimbo ya Moramu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha, maporomoko hayo yametokea jana nakusababisha vifo vya watu 13 na majeruhi wawili.

" FILAMU ZA NUSU UCHI ZINATUHARIBIA SOKO"...JENGUA




NGULI wa filamu za Kibongo, Mohammed Fungafunga ‘Jengua’ amewafungukia baadhi ya wasanii wa kike wanaofanya filamu za nusu uchi kuwa zinawaharibia soko la tasnia hiyo kwani wakati mwingine wazazi hushindwa kununua kuhofia kuangaliwa na watoto wao.

Akizungumza na Risasi , Jengua alisema kuna baadhi ya wasanii wameshazoeleka kwa filamu hizo kiasi kwamba wazazi wanachenga kuzinunua ili kutowaharibu watoto wao.

“Hivi jamani hutuwezi kutengeneza filamu bila kuweka hayo mambo ya utupu? Mbona sisi wazee tunacheza filamu bila kuwa na huo utupu lakini bado tunaendelea kuwa na mashabiki wengi na filamu zetu zinanunuliwa? Tukiendelea hivi tusishangae pale ambapo filamu zetu zitadunda sokoni,’’ alisema Jengua.

PICHA 5 ZA LAANA YA "KANGA MOJA" KATIKA SHOW YA MSANII DIAMOND- BUKOBA



Mambo yanayofanywa na kundi la kanga moja ni ya aibu sana  kwa  sababu  ni  uchafu  unaotendeka  mbele  ya  watoto......

Mwanamke  hujifunga  kanga  moja  tu  bila  chupi  wala  chochote  ndani.Baada  ya  hapo  humwagiwa  maji  kitu ambacho  huanika  kila  kitu  hadharani......

Kama haitoshi, akimwagiwa  maji, wenzie  huanza  kumtia  chupa  matakoni  hali  inayoashiria  VITENDO  VYA  ULAWITI......

Tunawafundisha  nini  watoto???..Tunaifundisha  nini  jamii  na  kizazi  cha  kesho????




KAJALA MASANJA AJICHORA TATTOO YA WEMA SEPETU MGONGONI KAMA ISHARA YA KUMSHUKURU KWA ZILE MILIONI 13




Kajala ameamua kuchora Tattoo yenye jina la WEMA mgongoni mwake  baada ya kutolewa faini ya Shilingi Milioni 13 na msanii mwenzake Wema Sepetu,
 
hii ikiwa kama ishara ya shukrani kwa rafiki yake kipenzi Wema Sepetu.

Kupitia ukurusa wake wa instagram Wema nae ameandika hivi: