Saturday, June 8, 2013

NAIBU WAZIRI WA JINSIA NA WATOTO AIBUA KASHIFA YA RUSHWA YA NGONO KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA


Suala la uwepo wa rushwa ya ngono kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) limetinga bungeni.

Suala  hilo Lilijitokeza jana wakati Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM), alipomaliza kujieleza bungeni akiomba kura kwa wabunge wamchague awe mjumbe kwenye taasisi hiyo.


Baada ya Mbunge huyo kumaliza kujieleza, alisimama Mbunge wa Viti Maalumu, Naibu Waziri wa Jinsia na Watoto, Ummy Ally Mwalimu aliyemhoji atatoa mchango gani katika kupambana na changamoto kwenye chuo hicho, ikiwamo rushwa ya ngono na ukatili wa kijinsia, ili kusaidia watoto wa kike wasome vizuri.


Kabla ya Mangungu kujibu swali hilo, Mbunge wa Chakechake, Mussa Haji Kombo (CUF), aliomba Mwongozo wa Spika kutaka muuliza swali afute kauli yake kwani ni ya udhalilishaji na inaweza kuleta matatizo.


 Hata hivyo, Spika Anne Makinda aliingilia kati na kusema hakuna haja ya kufuta kauli hiyo kwa vile ndiyo hali halisi iliyopo.

Akijibu swali hilo, Mangungu alisema atasaidiana na wenzake kuhakikisha wanakomesha suala hilo.

Katika uchaguzi huo, Mbunge wa Kisarawe, Suleiman Jaffo (CCM) alichaguliwa kuwa mjumbe kwenye Jukwaa la Kibunge la Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC-PF) katika uchaguzi uliofanyika bungeni.

Akitangaza matokeo, Spika Makinda alisema Jaffo aliibuka kidedea baada ya kupata kura 74 na kuwashinda wapinzani wake, Mbunge wa Viti Maalumu, Leticia Nyerere (Chadema) aliyepata kura 56 na Mbunge wa Busanda, Lorensia Bukwimba (CCM) aliyepata kura 51.  Kura 182 zilipigwa na moja kuharibika.
 

Pia Spika Makinda alimtangaza Mangungu mshindi na kuwa mjumbe wa Baraza la Udom kwa kupata kura 137 dhidi ya 38 za mpinzani wake, Mbunge wa Viti Maalumu, Pudenciana Kikwembe (CCM). Kura 177 zilipigwa na mbili kuharibika.
 

Upande wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) aliyeibuka mshindi ni Mbunge wa Babati Vijijini, Jitu Soni (CCM) ambaye hakuwa na mpinzani baada ya Mbunge wa Igunga, Dk Dalaly Kafumu (CCM) kujitoa.
 


Pia Mbunge wa Viti Maalumu, Pindi Chana (CCM) aliibuka kidedea kwa ujumbe wa Baraza la Chuo  Kikuu cha Sayansi na Teknolojia, Mbeya, baada ya kukosa mpinzani.

SAKATA LA HOUSE GIRL ALIYEJINYONGA KISA PENZI LA CHRISTOPHER


 





Mfanyakazi wa ndani aliyejiua kisa mapenzi aitwaye Devotha Sanga leo ameagwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam. 

Marehemu Devotha alijinyonga Juni 4 mwaka huu akiwa nyumbani kwa bosi wake eneo la Kitunda jijini Dar kwa wivu wa mapenzi. 


Devotha alikuwa katika penzi na kijana mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Christopher anayedaiwa kuwa na wapenzi wengi kiasi cha kusababisha marehemu kuchukua uamuzi huo. 

Baada ya kuagwa mwili wa Devotha umesafirishwa kuelekea Njombe kwa mazishi.

MFULULIZO WA VIFO VYA WASANII WAMFANYA DOKII AFUNGUKE KUWA NI MUNGU ANAWAADHIBU


MWIGIZAJI Bongo, Ummy Wenslaus ‘Dokii’ ameibuka na kusema kuwa vifo vya wasanii vimetokea kutokana na kujisahau hivyo Mungu ameamua kuwaadhibu. 

Akiongea na mwandishi wetu katika Viwanja vya Leaders Club, Juni 5, mwaka huu ambapo mwili wa Mangwea ulikuwa ukiagwa, Dokii alisema matukio ya vifo vya wasanii mbalimbali yaliyotokea miaka miwili mfululizo ni pigo kubwa kwani wengi ni vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa kitu ambacho anakiona ni ishara kuwa Mungu anataka kujidhihirisha kwa wasanii.
“Wasanii tulijisahau sana na kuona Mungu hayupo kwani kipindi bado hatujatoka na tunatafuta kutoka kisanaa, tulikuwa tunamuomba kila wakati lakini baada ya kutoka na kuwa mastaa tumemsahau kabisa.

“Hatukumbuki kwenda ibadani tunabaki kuendekeza starehe za dunia tu, hivyo tubadilike kwani Mungu ameanza kujionesha kwetu kwamba yupo,” alisema Dokii.

Tizama Picha ya Diamond enzi hizo kabla hajawa star.

Maisha siku zote nikupambana na mpambanaji hodari siku zote lazima shinde unaweza jua ulipotoka ila usijue uendako. Hivi ndivyoilivyokuwa kwa msanii Diamon.Nani alijua leo Diamond atakuwa hivi.
TIZAMA PICHA HII..hapani Diamond kabla hajawa supasta



SASA TIZAMA PICHA ZA DIAMOND BAADA YA KUWA SUPASTAA 


Kweli pesa sabuni ya roho..all da best Diamond

MTAMBUE KIJANA HANDSOME ZAIDI DUNIANI NA BINTI MZURI ZAIDI DUNIANI.

naitwa Queen Fatima Zohar-Godabari wa Saudi Arabia inasemekana yeye ndiye mwanamke mzuri zaidi duniani kwa mwaka huu wa 2013. Fatima Zohar-Godabari ambaye kwasasa ni malkia wa Saudi Arabia alikuwa akivaa hijabu muda wote kama wafanyavyo wanawake wakiislamu kiasi cha kufunika uso wake masaa yote lakini siku moja alipigwa picha akiwa hajajifunikana usoni napicha hiyo ilipostiwa katika mitandao na magazeti ndipo watu walipodai hakika ni mwanamke mzuri zaidi na kumpelekeakuwahuru kupiga picha pasipo kujifunika usoni.
 Tizama picha zake hapa












Upande mwingine inasemekana kwamba kijana Omar Borkan Al Gala ndiye kijana handsome zaidi kuliko wote duniani kwa mwaka huu wa 2013..Omar Borkan Al Gala ambaye ni mwigizaji napi ni mwanamitindo alifukuzwa huko Saudi Arabia kutokana na mvuto aliokuwa nao.
Tizama Picha zake hapa.






Je Unadhani watu hawa wawili wanastahili sifa hizo???