Mfanyakazi wa ndani aliyejiua kisa mapenzi aitwaye Devotha Sanga leo ameagwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Marehemu Devotha alijinyonga Juni 4 mwaka huu akiwa nyumbani kwa bosi wake eneo la Kitunda jijini Dar kwa wivu wa mapenzi.
Devotha alikuwa katika penzi na kijana mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Christopher anayedaiwa kuwa na wapenzi wengi kiasi cha kusababisha marehemu kuchukua uamuzi huo.
Baada ya kuagwa mwili wa Devotha umesafirishwa kuelekea Njombe kwa mazishi.
No comments:
Post a Comment