Thursday, April 25, 2013

"WANAUME NI TAPELI NA WAMENIPOTEZEA MUDA WANGU"...QUEEN SUZY




MNENGUAJI wa Bendi ya FM Academia, Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’ amesema hahitaji mwanaume yoyote kwa sasa kwani wanampotezea muda kwa kipindi kirefu.

Akizungumza na mwandishi wetu,Queen alisema wanaume wamekuwa wakimsumbua mara kwa mara kutaka kampani ya kimapenzi lakini wengi wao wanakuwa hawana mapenzi ya kweli hivyo anaona bora kuwapiga chini.

“Bora niwe singo natafuta pesa kuwazawaza hawa wanaume nitaishia kuumia tu na kushindwa kufanya shughuli zang, tena waache kunifuatafuata kwa sasa,’’alisema Queen Suzy.


Mnenguaji huyo alishawahi kuwa na uhusiano na mwimbaji wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Kalala Junior ambaye alizaa naye mtoto mmoja baadaye akatembea na rapa wa FM Academia, G 7 ambao wote ameshamwagana nao. 

ORODHA NZIMA YA WASANII WALIOTAJWA KUWANIA TUZO ZA "KILI MUSIC AWARDS" MWAKA 2013



Majina ya wasanii watakaowania tuzo za Kili mwaka 2013 yametajwa leo. 
WIMBO BORA WA MWAKA 
Dear God - Kala Jeremiah
Leka dutigite - Kigoma all star
Mapito - Mwasiti Feat Ally Nipishe
Me n U - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee
Pete- Ben pol

MSANII BORA WA KIUME 
Ben Pol
Diamond
Linex
Mzee Yusuf
Ommy Dimpoz

MSANII BORA WA KIKE 
Isha Mashauzi
Khadija Kopa
Lady Jaydee
Mwasiti
Recho

MSANII BORA WA KIKE - TAARAB 
Isha Mashauzi
Khadija Kopa
Khadija Yusuph
Leila Rashid

MSANII BORA WA KIUME - TAARAB
Ahmed Mgeni
Hashim Said
Mzee Yusuf

MSANII BORA WA KIUME - BONGO FLAVA 
Ally Kiba
Ben Pol
Diamond
Linex
Ommy Dimpoz

MSANII BORA WA KIKE - BONGO FLAVA 
Linah
Mwasiti
Recho
Shaa

MSANII BORA WA HIP HOP 
Fid Q
Joh Makini
Kala Jeremiah
Profesa J
Stamina

9. Msanii Bora wa Kiume - Bendi 
Chalz Baba
Dogo Rama
Greyson Semsekwa
Jose Mara
Khaleed Chokoraa

Msanii Bora wa Kike - Bendi 
Anneth Kushaba
Luiza Mbutu
Mary Lucos
Vumilia

Msanii Bora anayechipukia
Ali Nipishe
Angel
Bonge la Nyau
Mirror
Vanessa Mdee

Video Bora ya Wimbo ya Mwaka 
Baadae - Ommy Dimpoz
Kamili gado - Professor J Feat Marco Chali
Marry Me - Rich Mavoko
Nichum - Bob Junior
Party Zone - AY Feat Marco Chali

Mtunzi Bora wa Mashahiri - Taarab
Ahmed Mgeni
Hemed Omary
Khadija Kopa
Mzee Yusuf
Thabit Abdul

Mtunzi Bora wa Mashahiri - Bongo Flava
Ally Kiba
Barnaba
Ben Pol
Linex
Ommy Dimpoz

Mtunzi Bora wa Mashahiri - Hip Hop
Fid Q
Joh Makini
Kala Jeremiah
Mwana Fa
Stamina

Mtunzi Bora wa Mashahiri - Bendi
Chalz Baba
Grayson Semsekwa
Jonico Flower
Jose Mara
Khaleed Chokoraa

Mtayarishaji Bora wa Mwaka - Muziki wa Kizazi Kipya
Bob Junior
Ima the boy
Man Water
Maneke
Marco chali
Mensen Selecta

Mtayarishaji wa Wimbo wa Mwaka - Taarab
Bakunde
Enrico

Mtayarishaji wa Wimbo wa Mwaka - Bendi
Allan Mapigo
Amoroso

Mtayarishaji Chipukizi wa Mwaka
Imma the Boy
Mensen Selecta
Mr T Touch
Sheddy Clever

Rappa Bora wa Bendi 
Fagasoni
Greyson Semsekwa
J4
Jonico Flower
Sauti ya Radi

Wimbo wenye vionjo vya asili
Aambiwe - offside trick
Atatamani - AT
Boma la utete - Young D
Chocheeni kuni - Mrisho Mpoto Feat Ditto
Mdundiko - Momba Feat Juma Nature

Wimbo Bora wa Bendi 
Chanzo ni sisi - Mapacha watatu
Jinamizi la Talaka - Mlimani Park Orchestra
Risasi kidole - Mashujaa band
Shamba la twanga - African Stars band

Wimbo Bora wa Reggae 
Hii si ya waoga - Yuzzo
Kilimanjaro - Warriors from The East
NATAFUTA PARADISE - Mac Malick Simba
Salvation - Delayla Princess
Tunda - Hardmad

Wimbo Bora wa Africa Mashariki 
Fresh All Day - Camp Mulla
Make you dance - Keko Feat Madtrax
Maswali ya polisi - DNA
Still a Liar - Wahu
Valu Valu - Jose Chameleone

Wimbo Bora wa - Bongo Pop 
Aifola - Linex Feat fundi Samweli
Baadae - Ommy Dimpoz Feat Angel
Chuki Bure - Sharo Milionea Feat Dully Sykes
Marry Me - Rich Mavoko
Me and you - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee

Wimbo Bora wa Kushirikiana/kushirikishwa
Chuki Bure - Sharo Millionea Feat Dully Sykes
Mapito - Mwasiti Feat Ally Nipishe
Me and U - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee
Sihitaji marafiki - Fid Q Feat Yvonne
Single Boy - Alikiba Feat Lady Jaydee


Wimbo Bora wa Hip Hop
Alisema - Stamina Feat Jux
Bum kubam - Nikki wa Pili Feat G Nako
Dear God - Kala Jeremiah
Nasema Nao - Nay wa Mitego
Sihitaji Marafiki - FID Q Feat Yvonne

Wimbo Bora wa RnB
Amerudi - Belle 9
Kuwa na Subira - Rama Dee Feat Mapacha
Maneno maneno - Ben Pol
Pete - Ben Pol

Wimbo Bora wa Ragga/ Dancehall 
Je ni nani - Ras Six
Muda upite - Susu Man
Predator - Dabo
Push Dem - Dr Jahson
Take it down - Chibwa and Tanah

Wimbo Bora wa Taarab
Mjini chuo kikuu - Khadija Kopa
Mpenzi chocolate - Jahazi [Mzee Yusuph]
Si bure una mapungufu - Isha Mashauzi [Mashauzi Classic]
Sina muda huo - Jahazi [Leila Rashid]
Siwasujudii Viwavi jeshi -Isha Mashauzi [Mashauzi Classic]

Wimbo Bora wa Zouk/Rhumba 
Gubegube -Barnaba
Mapito - Mwasiti Feat Ally Nipishe
Nashukuru umerudi - Recho
Ni wewe - Amini
Sorry - Barnaba

Bendi Bora ya Mwaka CD1 African Stars Band
Mapacha wa tatu
Mashujaa Band
Mlimani Park Orchestra [Sikinde]
Msondo Ngoma Music band

Kikundi Bora cha Taarab
Dar modern Taarab
Five stars modern Taarab
Jahazi Modern Taarab
Kings modern Taarab
Mashauzi Classic

Kikundi Bora cha Muziki wa Kizazi Kipya 
Jambo squad
Makomando
Tip Top Connection
Tmk wanaume family
Weusi

" HAKUNA WANAUME TZ....WENGI WAO WANA F** L"....HILI NI TUSI LA JINI KABULA BAADA YA KUSALITIWA



 Kinachoonekana  ni  kwamba  Jini  kabura  amesalitiwa  na  mpenzi  wake  na  hivi  ameamua  kuhamishia  hasira  zake  kwa  wanaume  wote.....

Jini  kabura  amefikia   hatua  ya  kuunga  mkono  vitendo  vichafu  vya  mapenzi  ya  jinsia  moja  kwa  madai  kuwa  hakuna  wanaume  tz  na  hao  wachache  waliopo  eti wanaf***lwa....!!!!

Kupitia  mtandao  wa  BBM,  Jini  kabula  alipost  ujumbe  huu:

 "Hivi Boy Friend Akikusaliti kwa Marafiki zako na Ndugu zako Ukilipiza kuna Ubaya?

"Naombeni Jibu maana nina mpango wa kutoka mpaka na baba zake kama mbwai acha iwe Minina wanaume Bongo....Griiii... 

"Mnao Sag*na Sag**neni tu nawasaport wote Peaneni raha wanaume hakuna maana wengi wanaf*lwa"...

WABUNGE WAUNGANA KUKATAA BAJETI WIZARA YA MAJI





Bajeti ya Wizara ya Maji ya mwaka wa fedha 2013/14, iliyokuwa ipitishwe na Bunge jana, imekwama na kuahirishwa hadi Jumatatu.

Hatua hiyo ilifikiwa, baada ya wabunge kutoridhika na kiwango cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya wizara hiyo.
 
 Wakati wabunge hao wakichangia hoja zao katika mjadala wa bajeti hiyo, iliyowasilishwa na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe juzi, walionesha msisitizo kuwa hali ya upatikanaji wa maji ni mbaya nchini.
 
 Mbali na kuelezea hali mbaya ya maji majimboni, wabunge wengine walitoa ushahidi kuwa wanakotoka hulazimika kuoga kwa zamu na wakati mwingine hawaogi kwa siku kadhaa.
 
 Spika wa Bunge, Anne Makinda ndiye aliyeahirisha kupitishwa kwa bajeti hiyo, wakati akitoa majibu ya Mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba (CCM).
 
 Nchemba katika hoja yake aliyoombea Mwongozo, alitaka mjadala wa Bajeti hiyo usitishwe, ili kutoa nafasi kwa Serikali kukutana na Kamati ya Bajeti na kuangalia namna ya kutatua ufinyu wa fedha zilizotengwa.
 
 “Naona sasa mahitaji ya wabunge wote na wananchi kwa jumla ni Bajeti hii, kwa kweli iboreshwe, ili ifikie malengo stahiki katika maeneo yetu.
 
 “Ni kweli suala la maji hatuwezi kulifanyia utani, sasa naitaka Wizara ya Maji, Kamati ya Bajeti na Wizara ya Fedha, zikafanyie kazi suala hili, walete majibu ya uhakika hapa Jumatatu,” alisema Makinda.
 
 Alisema amefuatilia na kubaini kuwa idadi kubwa ya wabunge waliochangia mjadala huo wa maji, wamekataa kuiunga mkono Bajeti hiyo, huku akisisitiza umuhimu wa kushughulikia suala hilo kwa utaratibu wa majadiliano ambao Bunge hilo limeridhia.
 
 “Tangu jana (juzi) hadi leo (jana), hakuna anayeunga mkono suala hili, mkumbuke utaratibu tuliojianzishia wenyewe wa majadiliano, ni vyema tuliwasilishe kwa Kamati ya Bajeti ili lipatiwe ufumbuzi,” alisisitiza.
 
 Wakati kikao cha Bunge kikianza jana, pamoja na Mwigulu, pia Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema), walitaka mjadala huo usitishwe, ili kutoa fursa kwa Serikali kuboresha kiwango cha fedha za Bajeti hiyo.
 
  Juzi na jana wakati wabunge wakichangia mjadala huo, walikataa kuunga mkono Bajeti hiyo huku wakitaka kiwango cha fedha kilichotengwa kwa Wizara hiyo Sh bilioni 398, kiongezwe angalau Sh bilioni 185, ili miradi mingi ya maji hasa vijijini itekelezwe.
 
 Pia katika mjadala huo, baadhi ya wabunge walijikuta wakilumbana kuhusu mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe, uliotengewa Sh bilioni 56 ambapo wengine walidai Waziri wa Maji, amejipendelea huku wengine wakitetea hoja hiyo.
 
 Michael Laizer, Mbunge wa Longido (CCM), katika mchango wake, alisema katika jimbo lake wananchi hasa wazazi wanalazimika kuoga kwa zamu, kutokana na shida ya maji na kuiomba Serikali kufuta safari za nje, ili fedha zipelekwe katika miradi ya maji.
 
 Mbunge wa Viti Maalumu Agnes Hokororo (CCM), aliishauri Serikali kuangalia mbinu mpya kwa ajili ya kuboresha miradi ya maji kwa kuwa inaathiri  wananchi hususan wanawake.
 
 Alitolea mfano Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, kuwa kutokana na ukosefu wa maji, wanawake hufanyiwa vitendo vya udhalilishaji wanapotafuta maji hayo.
 
 “Nasema wazi hapa, wanawake wa mikoa ya Kusini wanapata shida. Mfano kijiji cha Nanjota, Wilaya ya Masasi, wanawake wanashindwa kushiriki shughuli za maendeleo kwa kuwa wanatumia saa 24 kutafuta maji na wakati mwingine wanarudi bila kuyapata,” alisema.
 
 Mbunge wa Viti Maalumu, Rose Kamili (Chadema), alitaka fedha zilizotengwa katika mradi wa maji wa Mwanga, zigawanywe katika maeneo mengine, ili nako miradi ya maji itekelezwe na wananchi wa maeneo hayo nao wapate maji.
 
 Si kwamba hatupendi maji yaende Mwanga, lakini utaratibu uliotumika si mzuri, haiwezekani Sh bilioni 56 zote ziende Mwanga wakati maeneo mengine kuna shida ya maji,” alisisitiza.
 
 Alieleza kushtushwa na kitendo cha Wizara ya Maji kutoa tangazo la zabuni kwenye baadhi ya vyombo vya habari, kuhusu mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe, wakati Bajeti hiyo haijapita jambo ambalo alidai ni dharau kwa wabunge.
 
 Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema), kama alivyofanya Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugora (CCM) kwa kuja na mchoro aliouita nyoka wa shaba, naye aliwasilisha picha halisi zinazoonesha wanawake wanavyopata shida kutafuta maji.
 
 “Namwunga mkono Kangi na mimi naleta picha hii inayoonesha mazingira halisi ya tatizo hili. Mbunge yeyote atakayeunga mkono Bajeti hii, hafai kurudi
bungeni mwaka 2015, naomba mjadala huo uahirishwe ili Bajeti iboreshwe zaidi,” alisisitiza.

TRAFIKI AKABWA KOO....!!! POLISI WALAANI NA KUDAI WAMEDHALILISHWA




Siku moja baada ya kituo cha ITV kuonesha mzozo uliosababisha askari wa usalama barabarani kuwa katika wakati mgumu kutokana na kukunjwa na raia wakati akiamua ugomvi baina ya madereva wawili baada ya kutokea ajali , jeshi la polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni limelaani na kutoa onyo kali na kuongeza kuwa tukio hilo limelidhalilisha jeshi la polisi na kwamba halivumiliki.

GODBLESS LEMA AHUSISHWA NA MAUAJI YA MWANAFUNZI WA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA



MKUU wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo ameamuru polisi kumkamata Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema pamoja na wanafunzi walioshiriki kurusha mawe baada ya kutokea vurugu zilizotokana na kifo cha mwanafunzi wa mwaka wa pili, Chuo cha Uhasibu Arusha, Henry Kago (22).
 
Naibu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Faraji Kasidi jana alitangaza kufunga chuo hicho kwa muda usiojulikana kutokana na vurugu zilizotokea chuoni hapo, ikiwemo ukiukwaji wa nidhamu na urushwaji wa mawe uliofanywa na wanafunzi hao kwa Mkuu wa Mkoa na kamati ya ulinzi na usalama.
 
Mulongo alitoa amri hiyo baada ya Lema kudaiwa kuingia chuoni hapo jana asubuhi na kufanya siasa bila kufuata utaratibu.
 
“Si jambo jema kwa Mbunge kuingia chuoni na kuhamasisha siasa kwenye jambo hilo la kifo badala ya kuwatuliza wanafunzi ili tujue kiini cha tatizo hili," alisema mkuu wa mkoa na kushutumu kwamba jambo hilo linabadilika badala ya msiba linawekwa chuki za siasa na wanafunzi nao kuingia kwenye mkumbo.
 
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa, upo utata wa kifo cha Kago kutokana na wengine kudai ameuliwa na bodaboda eneo la Esami na Kanisa la Waadventista Wasabato karibu na chuo huku wengine wakidai alitoka eneo la Bugaluu.
 
Alisema polisi inachunguza utata wa kifo hicho cha mwanafunzi huyo aliyekutwa na simu yake ya mkononi.
 
"Naagiza polisi kumkamata Lema popote alipo na wanafunzi wengine pamoja na wakili wake,” alisema Mkuu wa Mkoa bila kutaja jina la wakili.

Kwa  mujibu  pia wa  RADIO FIVE ya  jijini  Arusha, Mkuu  huyo  wa mkoa wa Arusha bwana Mulongo amenukuliwa kwa nyakati  tofauti tangu  jana  akitaja uwezekano wa Lema kusababisha kifo cha mwanafunzi ili apate nafasi ya kufanya siasa chuoni hapo.

FFU WAACHA LINDO NA KUINGIA DISCO KUKATA MAUNO



ASKARI Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Kilimanjaro wanaolinda mipaka kukabiliana na biashara za magendo zisiende Kenya, wanadaiwa kuacha lindo na kutinga ukumbi wa disko wakiwa na silaha nzito za kivita aina ya SMG.
  
Tukio hilo lilitokea usiku wa Aprili 20 mwaka huu, ambapo askari hao zaidi ya watano waliingia katika ukumbi wa disko wa High Way uliopo njia panda ya Himo na hivyo kutoa mwanya kwa magari sita aina ya Fuso yaliyokuwa yamesheheni sukari ya magendo kupita kirahisi kwenda nchini Kenya.
  
Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima umebaini kuwa baada ya askari hao kutinga katika ukumbi huo, ilichukua muda wa dakika 20 magari yakaanza kupita eneo hilo ambako askari hao walikuwa wameweka doria katika barabara ya Mwika.
  
Mbali na askari hao, pia maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) nao huweka doria katika barabara hiyo ya Mwika, lakini siku hiyo waliungana na askari wale katika ukumbi wa disko na kuacha magari hayo yakienda Kenya bila kukaguliwa.
  
Hata hivyo, raia wema waliwasiliana na waandishi wa habari za uchunguzi ambapo magari mawili yalijikuta mikononi mwa wananchi huku moja likiwaponyoka baada ya dereva wake kukimbia na kwenda kulificha katika mji mdogo wa Himo.
  
Gari lililobaki mikononi mwa wananchi wakiwamo pia waandishi wa habari za uchunguzi lilikuwa na namba za usajili T 695 BXH aina ya Fuso mali ya Susan Bahati Paul wa Moshi Mjini ambalo lilibainika kusheheni sukari kutoka nchini Thailand.
  
Gari hilo ambalo lilikuwa mita chache kuingia nchini Kenya kupitia eneo la machimbo ya mchanga aina ya pozolana, lilikabidhiwa kwa maofisa wa TRA katika kituo cha forodha cha Holili likiwa na mifuko 250 ya sukari yenye ujazo wa kilo 50 kia moja.
  
 Alipoulizwa jana juu ya askari wake kwenda kustarehe disko na kuacha sukari ikienda Kenya, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Koka Moita pamoja na kudai hana taarifa, aliahidi kulishughulikia suala hilo.
  
Wakati Moita akidai hana taarifa, habari za ndani ya Jeshi la Polisi zimedokeza kuwa askari wote waliokuwa zamu mpakani hapo usiku wa kuamkia Aprili 20 mwaka huu, wamehojiwa juu ya tuhuma za kuachia magari hayo yaliyosheheni sukari ya magendo.
  
Taarifa hizo zimedokeza kuwa askari hao waliokuwa kwenye magari mawili ya FFU, waliitwa na kuhojiwa ofisini kwa mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Kilimanjaro (RCO), Ramadhan Ng’anzi.
  
Zaidi ya magari kumi aina ya Fuso yaliyosheheni sukari ya magendo yamekuwa yakivuka mpaka kwenda nchini Kenya kila siku kutoka katika mji mdogo wa Himo kupitia njia ya Kwa Hussein hadi yalipo machimbo ya mchanga aina ya pozolana mita chache kutoka kituo cha forodha cha Holili na kuingia nchini Kenya kirahisi.