Sunday, May 5, 2013

ANGALIA PICHA ZA MLIPUKO WA BOMU KANISANI KATOLIKI ARUSHA



Polisi wakijaribu kuchunguza eneo bomu lilipolipukia leo asubuhi wakati wa misa ya kuzindua kigango hicho.iliyo katika kata ya olasiti na parokia ya burka
Majeruhi wa tukio hilo wakiwa katika hali mbaya..
endelea kupitia audifacejackson blog kwa  picha zaidi 


Read more: http://audifacejackson.blogspot.com/2013/05/angalia-picha-za-mlipuko-wa-bomu.html#ixzz2SQ6WXFlk

SABABU ZA KIUCHUNGUZI -'KWANINI WANAUME WENGI WANA MATATIZO KWENYE TENDO LA NDOA



ASILIMIA 60 ya wanaume wasioweza kufanya tendo la ndoa inatokana na matatizo ya kisaikolojia. Takwimu hizo zimetolewa jijini Dar es Salaam na Meneja wa Mradi wa Chama Cha Elimu ya Afya ya Uzazi cha Sweden (RFSU), Dk. Cathbert Maendaenda wakati wa semina ya siku moja ya waandishi wa habari iliyokuwa na lengo la kuzungumzia sheria ya masuala ya uzazi na ushiriki wa wananume.

Dk. Maendaenda alisema wanaume wanaopata tatizo hilo kutokana na magonjwa, umri na maumbilie ni asilimia 40 tu.

“Kundi kubwa la wananume wanaopata tatizo hili si kwamba ni wagonjwa bali wanakabiliwa na matatizo ya kisaikolojia, ukiwaweka chini na kuwapatia elimu wanarudi katika hali yao ya kawaida.

“Lakini changamoto kubwa inayopata wanaume hawa ni kwamba hospitali zetu ninyi zimejengwa kwa mfumo wa kutoa tiba na si ushauri nasaha kwahiyo mwanaume anaweza kwenda kule ili kuelezea tatizo lake lakini kutokana na mazingira ya hizo OPD  anashindwa kujielezea. 

“Matokeo yake anarudi nyumbani na kukaa na tatizo, kundi kubwa la wananume wa aina hiii wanakimbilia kwa waganga wa kienyeji au kujitibu wenyewe kwa mitishamba wakiamini watapona lakini mwisho wa siku hakuna unafuu unaopatikana,” alisema Dk. Maendaenda.

Akizungumzia tatizo la usihiriki wa wanaume katika suala la uzazi alisema bado jamii ina changamoto kubwa kwasababu wanaume wanapewa haki za kufanya ngono zaidi kuliko wanawake.

“Kwenye jamii tunayoishi bado kuna tatizo kubwa, wanaume wamepewa uhuru wa kufanya ngono kuliko wanawake, mwanamke akimfumania mke wake jamii na familia inachukulia jambo hilo ni la kawaida.

“Lakini mwanaume anapokwenda kushitakiwa kwao au ukweni akisema nimemfumania mke wangu na mwanaume mwingine mwanamke huyo ataonekana nuksi na jamii itamtenge
“Sasa wote huu ni ukatili na kuminya haki za wanawake, ndiyo maana unaona mwanamke hata akijua mume wake anatoka nje ya ndoa ataishia kulalamika mwenyewe lakini hajui hatua za kuchukua,”alisema Dk. Maendaenda.

Alisema kutokana na hali hiyo ya kukandamizwa kwa haki zao, wanawake wengi waliko ndani ya ndoa wanashindwa kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango kutokana na kuwaogopa waume zao.

HIZI NDIZO SABABU ZINAZO MFANYA MWANAMKE KUCHELEWA KUFIKA KILE***I WAKATI WA KUFANYA TENDO LA NDOA





Kukeketwa (Female Genital Mutilation).
Kukeketwa ni kitendo cha kukata sehemu ya uke hasa kisimi kwa wanawake. Katika Afrika kuna nchi 28 ambazo hufanya hicho kitendo cha kikatili, na pia nchi kama Yemen na Indonesia bado wanafanya. 

Ingawa wanawake waliokeketwa huweza kurudia hali ya kuweza kufika kileleni, walio wengi huathiriwa sana na hiki kitendo na kuwasababishia kushindwa kufika kieleleni.

 Dini, jadi na utamaduni:
Kuna baadhi ya mitazamo na malezi ya dini, jadi au tamaduni huwapa wanawake mtazamo mbaya, finyu na usio na maana kuhusiana na tendo la ndoa.

Katika dini, jadi, na tamaduni nyingi ukiacha jando na unyago, elimu ya mwanamke kuhusu mwili na uzazi havifundishwa wala kutamkwa matokeo yake wanawake wengi hawaijui miili yao, kiasi ambacho unakuta kijana wa kiume anamuoa binti hajui chochote kuhusu mwili wa huyo mwanamke na mwanamke mwenyewe hajui chochote kuhusu mwili wake mwenyewe, akiguswa chuchu anakataa kwani ni kwa ajili ya mtoto, hapo utategemea afikishwa kileleni kweli?

 Kisaikolojia.
Hili huchangia kwa asilimia 95 kwa matatizo yote yanayosababisha mwanamke asifike kileleni.

Adui mkubwa anayetisha sana wa mwanamke kutofika kileleni ni akili (mind.) 

Hofu labda ya kuachwa, mashaka, kutojiamini, kukasirika, donge moyoni, kisirani au mahusiano kutokuwa mazuri huweza kusababisha mwanamke kutofika kileleni, Kushindwa ku- concentrate kwenye tendo lenyewe na kupata hisia halisi (sensations). 

Kuwa na mawazo ya kitu kingine wakati wa tendo la ndoa Mawazo hasi (Negative) kuhusu tendo la ndoa, pia Kuwa mchomvu  kutamfanya mwanamke asifike kileleni.

 Kibailojia
Kama vile kuwa na mfumo ovyo wa mzunguko wa damu kwenye maeneo ya viungo vya uzazi pia huchangia. Anaweza kuwa na uvimbe au kisukari pia huchangia. pia hitilafu za viungo baada ya kufanyiwa upasuaji hasa sehemu ya uke.

 Umri (Menopause)
Kuna wakati mwanamke kuanzia miaka 48 – 52 hupata mabadiliko ya upungufu wa homoni na huo upungufu husababisha sehemu ya uke kuwa kavu wakati wa tendo la ndoa. 

Kuwa na uke mkavu huchangia katika ufanisi wa tendo la ndoa kuwa mdogo na hatimaye kushindwa kufika kileleni.

 Si kweli kwamba mwanamke akizeeka uwezo wa tendo la ndoa unakuwa mdogo, muhimu ni kutumia vilainisho kama gel au KY jelly na libeneke linaendelea kama kawaida.

 Kutumia madawa (Medicaments).
kama unatumia dawa za kuzuia msongo wa mawazo pia huchangia ile hamu ya tendo la ndoa (libido) na matokeo yake kukosa kufika kileleni. 
Pia kuna dawa za uzazi wa mpango hupunguza hamu ya tendo la ndoa hasa zile ambazo huingizwa mwilini (sindano). Pia dawa za kupunguza pressure hupunguza uwezekano wa kufika kileleni.

 Pombe, madawa ya kulevya na sigara, Alkoholi na madawa ya kulevya hupunguza sana hamu ya tendo la ndoa. Huathiri mfumo wa Fahamu unaohusika na mzunguko wa hisia za mapenzi kati ya ubongo na uke.

 Kama inavyoathiri (alkoholi) mwanaume kudindis*a vilevile huathiri mwanamke kufika kileleni. Mwonekano, urembo na umaridadi:

Kwa mwanamke jinsi anavyoonekana na jinsi mwanaume anavyoonekana kuna sehemu katika hisia za mapenzi (emotions na feelings).

Kama yeye mwenyewe anajijua kwamba hayupo vizuri kimwonekano (urembo, usafi, harufu) na pia kama mwanaume hayupo sawasawa basi anakuwa ameathirika sana kiasi ambacho hawezi kufika kileleni.

Pia wanawake wana uwezo mkubwa kunusa harufu kuliko mwanaume hivyo harufu yoyote mbaya kwake huwezi kumpeleka nje kabisa ya njia ya kwenda kileleni.

 Mazingira
Kama eneo au chumba mlichopo hakina usalama kama vile anahisi mtu anachungulia au anaweza kuingia, kwa mwanamke hiyo ni issue kwani hawezi kufika kileleni kwa sababu ya usalama wake.

Je kuna jinsi ya kuondoa tatizo la kutofika kileleni?
Kujiruhusu mwenyewe kupenda tendo la ndoa na zaidi kupenda kufika kileleni kwa hamu kubwa.

Kuwa responsible kwa mambo yote yanayohusu ufanisi wa tendo la ndoa.

Kujipa elimu na maarifa kuhusu elimu ya mapenzi kwa mwanaume na mwanamke,viungo vinavyohusika na kila kitu kinachiweza kukupa tofauti katika ufanisi uimarishaji wa tendo la ndoa kama unavyosoma hapa sasa hivi.
Kuwa na mawasiliano wakati wa tendo la ndoa hasa kuhusiana na maeneo yote ambayo unasisimka pale ukiguswa au kuchezewa.

Kufanyia kazi kila tatizo lolote la kisaikolojia na kupata solution kabla ya tendo la ndoa.

Umebadilika---K.Zungu ft Shevy Mapesa{Official HD Video}

MWALIMU WA MADRASAT ALIYEMLAWITI MWANAFUNZI AFUNGWA JELA MIAKA 15 HUKO ZANZIBAR



BAADA ya mahakama ya mkoa Vuga kumwachilia huru mwalimu wa madrasat Qadiria iliyopo Amani wilaya ya Mjini Unguja, aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kumlawiti mwanafunzi wake wa kiume wa miaka 11, hatimae mahakama kuu ya Zanzibar imemfunga jela miaka 15.

 Uamuzi huo wa mahakama umekuja kufuatia rufaa iliyowasilishwa mahakamani hapo na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP),  kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama ya Mkoa.

 Pamoja na adhabu hiyo, mahakama imemtaka kulipa fidia ya shilingi 500,000 dhidi ya mtoto huyo mdogo aliyemfanyia kitendo hicho.

 Mahakama hiyo, chini ya Jaji Abdulhakim Ameir Issa imelazimika kutoa adhabu hiyo baada ya kuridhika na sababu za rufaa zilizowasilishwa na DPP, ambazo zilidai kuwa mahakama ya mkoa Vuga imekosea kisheria katika utoaji wa hukumu.

Hivyo, baada ya kusikiliza kwa kina hoja za pande mbili hizo juu ya rufaa hiyo pamoja na kuangalia vielelezo vya ushahidi vilivyotolewa katika mahakama ya mkoa wakati wa usikilizwaji wa kesi ya msingi, Jaji Abdulhakim alisema mahakama ya mkoa ilikosea kisheria katika utoaji wa hukumu.

Jaji huyo alilazimika kutengua uamuzi wa mahakama ya Mkoa na kumtia hatiani Ustadh huyo dhidi ya shitaka hilo la kumuingilia mtoto wa kiume kinyume cha maumbile lililokuwa likimkabili.

 "Mahakama inatengua uamuzi wa mahakama ya mkoa kwa sababu ilikosea kisheria katika utoaji wake wa hukumu, hivyo mahakama hii inaamuru kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka 15, haki ya rufaa ipo wazi kwa upande ambao haukuridhika na uamuzi huu,"alisema Jaji Abdulhakim.

 Sambamba na adhabu hiyo, Jaji Abdulhakim alimtaka Ustadhi huyo kulipa fidia ya shilingi 500,000 kwa mtoto huyo aliyemfanyia kitendo hicho.

 Katika rufaa hiyo upande wa DPP uliongozwa na Mwanasheria wa serikali Maulid Ame Mohammed, kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka.

 Ustadh Hamadi Bakari Mohammed, miaka 48, alikuwa akikabiliwa na kesi ya kumuingilia kinyume cha maumbile mwanafunzi wake wa kiume wa miaka 11, kesi ambayo ilikua chini ya hakimu Makame Mshamba Simgeni wa mahakama ya mkoa Vuga.

 Kesi hiyo ilifunguliwa kwa mara ya kwanza Julai 7, 2011 ambapo alikana shitaka hilo baada ya kusomewa na Mwanasheria wa serikali Juma Msafiri Karibona, kutoka ofisi ya DPP.

 Pamoja na kukana huko, upande wa mashitaka uliwasilisha mashahidi sita mahakamani hapo, lakini walishindwa kuthibitisha kosa hilo kwa mujibu wa hakimu Makame Mshamba Simgeni kwa maelezo kuwa ushahidi wao ulijaa shaka ya maana.

 Hivyo, Januari 18 mwaka jana, mahakama hiyo ya mkoa ilimuona hana hatia dhidi ya kesi hiyo na kumuachilia huru chini ya kifungu cha 219 cha sheria za mwenendo wa jinai (CPA) namba 7/2004 sheria za Zanzibar.

 Wakati mahakama hiyo ya mkoa ikitoa hukumu hiyo, mshitakiwa huyo alikuwa nje kwa dhamana ya fedha taslimu shilingi 150,000 kwa wadhamini wawili pamoja bondi ya shilingi 300,000 kwa upande wake.

 Kwa upande wa mahakama kuu, Jaji Abdulhakim alimwachilia kwa dhamana ya wadhamini wawili wenye vitambulisho, mmoja kwa fedha taslimu shilingi 1,000,000 na mwengine kwa bondi ya shilingi 300,000.

 Ilifahamishwa, kinyume na kifungu cha 132 (1) sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar, Januari 13, 2011 majira ya saa 2:30 za asubuhi, huko Amani alimuingilia kinyume cha maumbile mtoto huyo wa kiume (jina tunamuhifadhi).

 Pamoja na adhabu hiyo aliyopewa na mahakama, Ustadh Hamad aliwahi kukaa rumande kwa muda wa siku 16, baada ya upande wa mashitaka kupinga kupatiwa dhamana kwa mara ya kwanza alipofikishwa mahakama ya mkoa, kwa madai anaweza kuingilia kati upelelezi ambao kwa wakati huo ulikuwa bado haujakamilika.

Zanzinews

BREAKING NEWS: KANISA KATOLIKI LALIPULIWA NA BOMU JIJINI ARUSHA WAKATI MISA IKIENDELEA



Kanisa katoliki parokia  ya Olasiti ambalo leo hii lilikuwa linapandishwa hadhi na kuwa Parokia limelipuliwa na  kitu  kinachosemekana  kuwa  ni  bomu, watu wengi wamejeruhiwa  na  mtu  mmoja  inasemekana  amefariki  dunia.... ....

Tukio  hilo  limetokea  wakati  Misa ikiwa ndio inaanza .Ilikuwa ni saa 5 kamili...Kabla Askofu hajaanzisha sala , mlipuko mkubwa  ulitokea  ndani  ya  kanisa  hilo...... 


Mgeni rasmi   katika  hafla  hiyo  alikuwa  ni   balozi wa Vatican nchini Tanzania. ...

Habari zaidi   zinakuja