Monday, May 6, 2013

LADY JAYDEE AWAFANYA CLOUDS FM WAGOME KUPIGA NYIMBO YOYOTE YA BONGO FLEVA.....TIMES FM WASHANGILIA




 Akizungumza  katika kipindi cha Power Breakfast, Meneja wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ameelezea kuwa Lady Jaydee  amekosea  kuelekeza  vita  kwao...


Amedai  kuwa kama tatizo ni Bendi ya SkyLight basi apambane kuipiku bendi hiyo na si kugombana na watu wengine.....

Akiongea  kwa  mbwembwe, Ruge  ameamuru  kutopugwa  wimbo  wowote  wa  bongo  fleva  leo.....

Amesema kuwa Clouds  fm ni chombo binafsi kina maamuzi ya kufanya chochote pasipo kuvunja sheria...

Baada  ya  kauli  hiyo  Times Fm  wamewajibu  clouds  fm  na  kudai  kuwa  WAO  LEO  WATAPIGA  BONGO  FLEVA  MPAKA  MAJOGOOOO...!!!   

Nadhani  Times  fm  wamefikia  uamuzi  huo  ili  kuwajulisha  clouds  kuwa  kuna  vituo  vingine  vingi vya  radio  zaidi  yao  na  kwamba  hawako  peke  yao 

Hii  ndo  tweet  yao...

 
"Kwa Kutumia Kilicho chetu , Asili yetu na Muziki wetu leo katika vipindi vyote utaskikia muziki wa nyumbani wa BONGO FLEVA kwa asilimia Kubwa."

JANUARY MAKAMBA NAYE AWAPONDA CLOUDS FM KWA VITISHO VYAO VYA KUGOMA KUPIGA "BONGO FLEVA " LEO




Huenda mjadala kuhusu uamuzi wa kituo cha radio cha Clouds FM, leo kutopiga Bongo Flava siku nzima haujalikuna sikio la naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.


Kupitia Twitter, Makamba ameandika kuwa Tanzania ina matatizo matatizo mengi ya kujadili kuliko nyimbo za kuchagua kucheza redioni. “We’ve got much bigger problems than radio playlists, ” ametweet.

Katika mahojiano maalum leo kwenye kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, mmoja wa wakurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba alidai kuwa ametoa amri leo kituo chake kisicheze Bongo Flava.

Uamuzi huo leo umekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

NAY WA MITEGO AFANANISHWA NA DEM....CHID BENZ AMTUNGIA JINA NA KUMUITA " NEEMA WA MITEGO"




Ugomvi  wa  chini chini kati   ya Chid benz  na  Ney wa  mitego  sasa  umefikia  pabaya.....

Juzi  Ney wa mitego  alionja  kichapo  toka  kwa  mashabiki  katika  show  yake  mbagala....Inadaiwa  kwamba Varangati hilo   lilitokana  na  madai  yake  kwamba   Chid  benz  ni  shoga  na  ametoboa  pua  kama  dem.... 

Mapema mchana huu Chidi Benz amefunguka kupitia ukurasa wake ya Facebook   na  kumtaka  NEEMA  WA  MITEGO(Neema ni jina la  kike )  aache  kumtukana  wala  kumwandika  message  zozote.....Vinginevyo  ataendelea  kuambulia  kichapo

Hii ni post yake
 

MWANAMKE AUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI NA MAJAMBAZI JIJINI DAR





Majambazi yamempora mama mmoja kiasi cha shilingi milioni kumi na kutokomea kusikojulikana....
Tukio hilo limetokea leo saa 5:16 jioni  na inavyosemekana  ni  kuwa mwanamke  huyo  alikuwa akitoka benki ya CRDB tawi la Uhuru ambapo majambazi yakiwa na pikipiki yalikuwa yakimfuatilia..
Alipotoka ,majambazi  hayo  yalimfuata na kuligonga gari lake makusudi   na ndipo dada huyo aliposimama ili angaalie nani kagonga gari yake ambapo jambazi mmoja alishuka na kumpiga risasi ya kifuani na kutokomea na kiasi hicho cha pesa. ..