Saturday, May 11, 2013

" HAKUNA KANISA LILILOSHAMBULIWA KWA BOMU JIJINI DAR LEO "...HII NI KAULI YA KAMANDA KOVA




Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kova amesema Taarifa zilizoenea kwamba Bomu limelipuka katika Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania (KKKT), Kunduchi jijini Dar es Salaam zimeenea ndivyo sivyo na kwamba askari walikuwa wanapambana na majambazi.

Wakati taarifa zikiwa zimesambaa katika mitandao ya kijamii na mitaani kwamba kuna kanisa la KKKT limeshambuliwa na bomu hivi punde, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kova amesema kwamba taarifa hizo sio za kweli na kwamba askari wa jeshi la polisi walikuwa wanapambana na majambazi karibu na eneo la kanisa hilo. 


Katika mapambano hayo polisi waliwarushia majambazi hayo bomu ili kuyakamata.

"Wakati askari wetu wanapambana na majambazi hayo- waumini wa kanisa hilo wamejitokeza kuwasaidia askari wetu. Naomba unisaidie kukanusha siyo kweli, nitazungumza na vyombo vingine vya habari kuweka sawa," amesema Kamanda Kova hivi Punde. 

MIKE TEE, PROFESA JAY, JAY MOE NA JUMA NATURE WATUMIA VIFARU VYA KI VITA KTK KUSHOOT VIDEO YAO?





Wasanii wakongwe wa Bongo Flava kutoka kushoto waliovaa kiraia ni Jay mo, mike tee, Juma Nature na profesa Jay wakiwa na wanajeshi
Picha hizi unazoziona ni post ya facebook ya Rapper and CEO wa kampuni ya Show BIZ Mike Tee Mnyalu na amezipost jana na kuandika  namnukuu "Wanaume Kazini Today tumeanza kushoot video yetu mpya soon tittle ntawajulisha its Under ShowBiz Defined Media" Swali je story line ya video hiyo itakuaje kuaje?
punguza kiraru raru, tusubiri tyme itafika.....
Mike Tee, Jay Moe , Profesa Jay na Juma Nature

YOU HEARD : PREZOO NA DIVA LOVENESS LOVE WAPO KWENYE MAPENZI MOTO MOTO




PREZZO
                                                                   IN LOVE WITH
DIVA LOVENESS LOVE
 Taarifa za siri ambazo zimefika mezani kwa muhariri zina nong'oneza kwamba Rapper tajiri nchini Kenya kwa sasa hivi yuko katika mahaba mazito na Mtangazaji wa kituo cha radio kikubwa nchini Tanzania, namzungumzia Diva Loveness Love wa Ala za Roho, inasemekana mahusiano yao yalianza wiki za karibuni baada ya Prezoo kudondoka bongo na alialikwa kwenye kipindi cha Ala za roho ndipo picha zima lilipo anzia, kama utani wakaanza kutania taniana, sasa usiku wa tukio hawakufanikiwa kwenda out lakini namba zilibadilishwa pale, kilichofata baada ya hapo sasa Prezzo akataka kwenda mpaka kwa kina binti lakini akazuiliwa wataalamu wa mambo wanasema penye nia pana njia, basi huenda time navyozungumza japo Prezzo hayuko bongo narudia tena huenda mambo yao yako bam bam kwa njia ya simu.
Muhariri alipojaribu kucheki na Diva, mwanadada akapangua shuti kuleeeeee, na kudai kuwa yuko na boyfriend wake wa kitanzania na PREZZO ni mshkaji tu.
alipovutiwa wire PREZZO jamaa akajaa mzima mzimaaaa, na kutiririka ya moyoni kuwa ni kweli anampenda Diva na mipango mengine inafata.
Skiza YOU HEARD HAPO CHINI:

VIGOGO WA DUBAI WAMGOMBANIA LULU MICHAEL ....




HABARI zilizonaswa na mwandishi  wetu  zinaeleza kuwa nyota wa sinema Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, ameitwa katika Jiji la Dubai, Falme za Kiarabu kwa ajili ya kula  bata ikiwa ni pole yake kwa kusota Gereza la Segerea kwa karibu mwaka mmoja.

Chanzo kimoja  kilipenyeza habari kuwa mapedeshee hao wamemualika staa huyo huku ikinyetishwa kwamba, vigogo wa sanaa hiyo Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ ndiyo watakaomsindikiza.
 

“Mapedeshee wamemtumia mamilioni ya fedha Lulu, wanataka kufanya naye pati ya pamoja kwa vile ni miongoni mwa mastaa wa Bongo wanaokubalika nchini humo na pia kumpa pole kwa kukaa gerezani muda mrefu.
 

“Mbali na sherehe hiyo, watakapokuwa nchini humo wanatarajia kuendeleza filamu ambayo wameanza kuirekodi hapa Bongo,” kilisema chanzo hicho.
 

Hata hivyo, chanzo kiliweka wazi kwamba kwa sasa, Lulu si rahisi kusafiri nje ya Bongo kwa vile kesi aliyonayo ina mipaka ya sehemu za kwenda. 
Alipotafutwa Dk. Cheni juu ya ishu hiyo, alisema waliomuita Lulu si mapedeshee bali ni Wabongo waishio kule, lakini masharti ya kesi yake hawezi kusafiri nje ya Tanzania.
Dk. Cheni akaulizwa kuhusu yeye na Steve Nyerere kuwepo kwenye safari hiyo ambapo alisema hana ufafanuzi zaidi, akakata simu.

NAIBU WAZIRI AINGILIA KATI UGOMVI WA LADY JAYDEE NA CLOUDS FM....RUGE AKIMBILIA MAHAKAMANI




IKIWA ni siku moja tu tangu Naibu Waziri wa Habari  Michezo Vijana na Utamaduni Amos Makala kutangaza hadharani kulivalia njuga suala la mzozo kati ya Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Clouds Media Group Ruge Mutahaba  na msanii nyota wa kike wa Bongo Fleva Judith ‘Wambura Lady Jaydee’  Ruge ametoa ya moyoni.
Tanzania Daima ambayo ilimpigia simu Ruge na kumuuliza ana lipi la kusema baada ya Makala kutamka kwamba atawaita wawili hao na kuzungumza nao sambamba na kuleta suluhu.
“Mimi kana nilivyosema katika tamko langu wiki iliyopita kwamba niko tayari tuitwe na watu watusikilize  pande zote mbili  hasa mlalamikaji na ukweli uweze kuwa wazi zaidi kwa sababu hadi sasa Lady Jaydee amekuwa akisema mambo mengi kiasi kwamba hata nashindwa kumuelewa”
Na siyo Waziri Makalla tu pia ikiwezekana hata kama kuna watu wengine wanataka kujitokeza ili kutuweka katika kiti moto watuulize maswali na kila mmoja wetu aote majibu mbele ya hao watu mimi niko radhi kufanya hivyo” anasema Ruge.
Wakati huohuo Ruge ameongeza kwamba  tayari ameshafuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungulia jalada la malalamiko ya kutukanwa na Lady Jaydee na taarifa hiyo amepelekewa  msanii huyo akiitwa katika vyombo vya sheria.
Lakini ninaweza kusema jambo hili linaweza kuzungumzika nje ya vyombo vya sheria kwani sisi tunaliona ni jambo dogo na la mzaha lakini lina athari kubwa katika jamii inayotuzunguka  anasema Ruge.
Mwanzoni mwa mwezi huu Lady Jaydee aliamua kuibuka na kuituhumu Clouds Media Group  kwa kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, twitter nab log yake kwamba wana muhujumu kimuziki , kuzuia matangazo ya mgahawa wake wa Nyumbani Lounge   na kipaji chake kwa ujumba tuhuma ambazo Ruge na Clouds wanazikanusha vikali.
Mwandishi wa habari hii alijaribu kumtafuta Lady Jaydee azungumzie kuhusu kauli ya Waziri kwa kupitia simu ya mumewake Gadner Habash simu iliita bila kupokelewa.

JESHI LA TANZANIA LATAMBA TENA.....LINASEMA KAZI YAKE NI MOJA TU AMBAYO NI KUWAFUMUA WAASI WA M23 HUKO KONGO




JESHI la Wananchi Tanzania (JWTZ), limesema limeanza kuwapeleka askari wake nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) kulinda amani na kuhakikisha wananyang’anywa silaha zote waasi wa kundi la M23 ili nchi hiyo itawalike.

Kutokana na hatua hiyo, JWTZ limesema halitishwi na vitisho vya M23 kutokana na kujiandaa vizuri kila idara, ikiwa ni lengo la kutaka kuona wananchi wa DRC wanaishi kwa amani, tofauti na sasa ambako kumekuwa na vitendo vya kinyama dhidi ya wanawake na watoto wadogo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, wakati wa kutoa tamko la jeshi hilo, Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, alisema kamwe hawatishwi na kundi la M23.

Alisema wanashangazwa na kitendo M23 kutoa vitisho, wakati askari wanaokwenda huko wanatoka nchi za Afrika Kusini, Malawi na Tanzania.

“Kwa nini iwe Tanzania pekee, sisi hatuwezi kutishwa na kikundi cha wanamgambo 1,000, tunasema tunakwenda kutimiza jukumu la Umoja wa Mataifa (UN) kuhakikisha DRC inatawalika na silaha zote wananyang’anywa,

“Tanzania tuna historia kubwa ya kuleta ukombozi na amani ndani ya nchi za Afrika, zikiwamo Commoro, Afrika Kusini, Liberia, Sudan na Lebanon, ndiyo maana vikosi vyote vitatu vinaongozwa na Mtanzania, Brigedia Jenerali James Mwakibolwa.

“Tulipokwenda Commoro, tulihisi kama damu itamwagika lakini hali ilikuwa tofauti kabisa na isitoshe ni askari mmoja tu aliteleza na kuanguka majini, sasa hawa M23 wao wamepata wapi mafunzo.

“Itakumbukwa Idd Amin Dada, alikuwa anajigamba na kusema anataka kuja kunywa chai Dar es Salaam, lakini aliishia kuchungulia visiwa vya Ukerewe… majigambo ya M23 ni ishara ya kuanza kuwa na wasiwasi,” alisema Kanali Mgawe.

Alisema kikosi kilichoanza kwenda DRC,kinajulikana kama Tanzania Bataria One –DRC (TANZBATT-1 DRC) na kuongeza kwamba kila baada ya miezi sita kutafanyika mabadiliko kadri itakavyohitajika.

Alisema kutokana na vitisho hivyo, bado Tanzania ni salama na itakuwa kuwa salama na kuwataka Watanzania kuondoa hofu juu ya matukio yanayotokea hivi sasa.

Alisema vifaa vya askari, wanaokwenda Kongo vimekamilika na tayari UN imevifanyia ukaguzi na kuridhia vinakidhi mahitaji katika kuimarisha ulinzi na usalama.

Kuhusu mzozo wa Tanzania na Malawi, alisema nchi hizo bado zina uhusiano mzuri wa kidiplomasia.

Mapema wiki hii, Rais Jakaya Kikwete aliwakabidhi askari wa JWTZ bendera mkoani Pwani, ikiwa ni ishara ya kuanza safari ya kuelekea DRC.