Friday, May 3, 2013

UPDATE: MATOKEO YOTE YA KIDATO CHA NNE 2012 YAMEFUTWA NA YATASAHIHISHWA UPYA




Habari kutoka bungeni ni kwamba matokeo yote ya  kidato  cha  nne yamefutwa na yatasahihishwa upya ( Re -grading ) haraka iwezekanavyo..
  
Taarifa ya tume iliyoundwa na waziri mkuu kuchunguza sababu za kufeli vibaya kwa watahiniwa wa kidato  cha nne  imesomwa  bungeni  leo  na  mh.LUKUVI. 

LUKUVI amesema sababu zilizosababisha  wanafunzi  wafeli   ni upungufu wa waalimu, mazingira magumu a kufundishia, idadi kubwa ya shule za sekondari iliyopelekea idadi kubwa ya watahiniwa  na  utaratibu  mbovu  wa  baraza  la  mitihani  uliotumika  bila  kuwashirikisha  wadau  wa  elimu


Mh.  LUKUVI amesema kuwa NECTA haikufuata vigezo vya kuwafaulisha wanafunzi kwa kufuata STANDARDIZATIONS na CONTINOUS ASSESSMENTS. ...

Hivyo  basi, matokeo  hayo  YAMEFUTWA  na  YATAFANYIWARE-GRADING 

BAADHI YA WASHUKIWA WA UJAMBAZI NYUMBANI KWA FINA MANGO WAKAMATWA



Baadhi ya washukiwa ujambazi nyumbani kwa mtangazaji wa kipindi cha Makutano cha Magic FM, Fina Mango wamekamatwa.Kwa mujibu wa Fina, majambazi hao wapo kwenye mtandao mkubwa unaofanya vitendo hivyo jijini Dar es Salaam.


Fina Mambo akiwa na familia yake
Kupitia Twitter ameeleza:
Lile kundi la majambazi lilokua likifanya uvamizi wa nyumba zipatazo 7 (kwangu ilikua ya 4) maeneo ya Kawe hadi Mbezi, ilisemekana ni kundi la watu 40 waliosambaa kuanzia Kawe (makao makuu) Mikocheni, Kinondoni mpaka Mbagala, Wameanza kukamatwa.


Polisi Kawe inashikilia watu 7 ambao walikutwa na baadhi ya vitu pamoja na bastola 1 na Gobole 1 matching risasi zilizokutwa maeneo ya tukio.


Waliokamatwa wanaongea na kusema kote walikopeleka mali kuviuza. Ni juhudi za kusifiwa za mmoja wa wahanga maana aliamua kulifatilia swala.


Hili mpaka mwisho wake baada ya kuvamiwa na risasi kupigwa ndani kwake. Kwa ushirikiano na wasamaria wema waliotoa info pamoja na Kawe Police wamekamatwa. Kidogo twaweza lala kwa Amani sasa.


Fina Mambo alivamiwa na majambazi wafikao wanane nyumbani kwake na kupora mali na fedha.
Screenshot 2013-03-25 at 06.49.53
Screenshot 2013-03-25 at 06.50.00

AIBU: MREMBO ATUPWA JELA MIEZI 6 BAADA YA KUNASWA AKIJIUZA.....MCHUMBA WAKE AMWAGA MACHOZI HADHARANI





MREMBO Brandina Barthon (24), Jumatatu iliyopita alihukumiwa kwenda jela miezi 6 baada ya kupatikana na hatia kwenye kesi ya ukahaba iliyokuwa ikimkabili katika Mahakama ya Sokoine Drive (Jiji) jijini Dar.

Brandina alisomewa hukumu hiyo na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, William Mutaki ambaye alisema kutokana na ushahidi uliothibitika, mahakama hiyo inamhukumu kwenda jela miezi 6, ili liwe fundisho kwa wengine.

Hukumu hiyo ilimfanya mrembo huyo kuchanganyikiwa na kuangua kilio lakini mheshimiwa hakimu aliamua kukazia hukumu yake bila ya kupepesa macho.
 
Wakati mwanamke huyo akiangua kilio, afande wa Jeshi la Magereza alimfikia na kumchukua  kwa ajili ya kumpeleka kwenye Karandinga kuelekea Gereza la Segerea kuanza maisha ya jela.

Mbali na Brandina, mwanaume aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wa mtuhumiwa huyo aliyekuwa akifuatilia kesi hiyo naye alimwaga machozi baada ya kutolewa hukumu hiyo.

"BILA CONDOM HUWEZI KULIFAIDI PENZI LANGU HATA UKINIHONGA MABILIONI"...SHILOLE



Mwigizaji na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Zena Mohamed, maarufu kwa  jina  la   shilole amedai kuwa anaweza kufanya ujinga wowote humu duniani lakini linapokuja suala la mapenzi kamwe hawezi kwenda pekupeku ( bila  condom )  ....

Akiongea kwa  kujiamini ,Shilole  alisema kuwa hata mtu awe vipi, au awe wa dini gani au awe na pesa kiasi gani kamwe hawezi kumvulia nguo kama  hana  kondom  mkononi.....

Msanii  huyo  alienda  mbali  zaidi  na  kuzilaani   kauli   za  baadhi  ya  watu zinazosema eti ukitumia "CONDOM"  ladha ya mapenzi inapungua.Yeye  anadai  kuwa  ni  mdau  wa  "GEMU"  hilo  na  huwa  anatumia  NDOM  kama  kawa  na  hufurahia  kama  kawaida...

" Hata niwe nimelewa kiasi gani huwa nipo makini sana maana najua vijana wengi wa mjini wananimezea  mate....Waje  tu , lakini  bila  KINGA wataambulia  PATUPU!!” Alisisitiza Shilole

MFANYABIASHARA KARIAKOO AJIRUSHA TOKA GHOROFA YA TISA NA KUANGUKIA GARI MCHANA HUU


KUANGUKIA GARI MCHANA HUU



Muda mfupi uliopita,Mtu mmoja alietambulika kwa jina la Shirimaambaye ni Mfanyabiashara katika moja ya Maduka ya Kariakoo jijini Dar es Salaam,amejirusha toka ghorofa ya 9 ya Hoteli ya Concord iliopo Maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam na amekimbizwa hospitali kwa uangalizi zaidi maana haijafahamika kama kapoteza Maisha au bado yu hai.

Mfanyabiashara huyo alijirusha toka ghorofani na kuangukia Gari aina ya Toyota Corolla ambayo ni taxi iliyokuwa imepaki nje ya hoteli hiyo....chanzo cha kujirusha kwa mfanyabiashara huyo bado hakijafahamika mpaka sasa.

Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea muda mfupi uliopita,wanaeleza kuwa walipatwa na mshuko baada ya kusikika kishindo cha kitu kilichokuwa kimeangukia gari hilo na waliposogea kushuhudia ndipo walipobaini kuwa alikuwa ni mtu huyo alietambulika kwa jina moja la Shirima.

" MAKALIO YANGU BADO YANALIPA..."AGNESS MASOGANGE




Mrembo  asiyeishiwa  na  vituko  maarufu  kwa  jina  na  Masogange  ameamua  kuvunja  ukimya   wa  muda  mrefu  kwa  kuyanadi  makalio  yake.......
  

Kumbukumbu  zetu  zinaonesha  kwamba Masogange  ni  miongoni  mwa  wasanii  waliopata  umaarufu  nchini  Tanzania  kwa  kupiga  picha  za  uchi  na  kucheza  movie  za  Uchi  mithili  ya  wacheza  XXXXX....

Ni  matumaini  ya  wengi  kuwa  Masogange  hutatuvulia  nguo  tena  na  badala  yake  utaishia  kujinadi  kwa HESHIMA..

Nasema  hivi  kwa  sababu  hata  mwaka  jana  ulianza  hivi  hivi.Ulivyoona  watu  wamekupotezea   uliamua  kuvua  nguo  zote  na  kujianika  mtupu,tena  katika  VIDEO  ambazo  zipo  mtandao  hadi  leo....