Friday, April 19, 2013

SPIKA WA BUNGE AWAKAANGA TENA WALE WABUNGE WALIOTIMULIWA BUNGENI.....







Leo asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu Mh Spika ametoa uamuzi kuhusu muongozo ulioombwa na Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kuhusu uhalali wa kutolewa nje na kisha kufungiwa vikao vitano kwa wabunge sita (6) wa Chadema uliotolewa juzi na Naibu Spika.
 Mh Spika anasema kwa kuwa kwa sasa hakuna kanuni kuhusu jambo hilo uamuzi wa Naibu spika utabaki halali na utaingizwa kwenye kumbukumbu za bunge kwa ajili ya kutumika huko mbele kwa ajili ya maamuzi pale itakapotokea tukio kama hilo.

Kwa uamuzi huo Wabunge hao watakosekana bunge bunge kwa siku tano ambazo ni Alhamisi (jana), Ijumaa (leo) pamoja na Jumatatu, Jumanne na Jumatano wiki ijayo.


Uamuzi wa Naibu Spika Mh. Job Ndugai, wa kumtoa nje Mh. Lissu na wengine  watano na kupewa adhabu ya kutoshiriki vikao vitano vya Bunge umebarikiwa na Mheshimiwa Spika..
 Hivyo Basi, Maamuzi ya Mh. Ndugai, yatakua Kanuni Rasmi kwa Tukio kama Hilo Na adhabu iliyotolewa.
Photo
Taswira ya vurugu zilizotokea bungeni dodom

No comments:

Post a Comment