IMEBAINIKA kuwa baadhi ya wasanii wa kike nchini hawavai nguo za ndani kwa madai kwamba joto linawaumiza na kuwasababishia michubuko katika baadhi ya sehemu za mwili wao
Hali hiyo ya kutovaa nguo za ndani inasababishwa na wasanii hao kutaka kupata hewa na kuepuka kubanwa kwa madai kuwa wanahitaji kuwa huru zaidi na mavazi wanayovaa huku baadhi ya sehemu zao za mwili kuonekana vizuri
Hayo yalibainishwa jijini Dar es Salaam juzi na msanii wa filamu pamoja na muziki wa miondoko ya miduala Zuwena Mohamed 'Shilole' alipokuwa akizungumza na jarida hili ....Shilole alisema kuwa kutovaa nguo za ndani hususani kwa mtoto wa kike ni kujiaibisha na kujishushia heshima katika jamii
Alisema kuwa wapo wasanii ambao hawavai nguo za ndani kwa madai kuwa wanaogopa kuchubuka jambo ambalo yeye aliliona si sahihi hivyo na kudai kuwa tabia ya kujirahisisha katika maswala ya ngono ndiyo inayopelekea kuvaa bila nguo yoyote ndani
"Unajua kiukweli ni kujishusha thamani hauwezi kukaa bila ya kuvaa nguo ya ndani tena mtoto wa kike ni kujidharilisha hata kama ni kuiga tusifikie huko jamani"alisema Shilole
Pamoja na hayo aliongezea kuwa sababu nyingine inayosababisha wasanii hao kubaki utupu ni kuonyesha viungo vya mwili wao jinsi walivyoumbika jambo ambalo yeye aliliita ni njia moja wapo ya kujidharilisha na kuutangaza uhuni kwa jamiii
"Kama hauna makalio makubwa huna tuu hata usivae nini hayaonekani hivyo ni bora ujistili kama mtoto wa kike"alisema Shilole
Alipoulizwa kuwa na yeye ni miongoni mwa wasanii wanaokaa utupu Shilole alisema kuwa amelelewa katika mazingira ya kuvaa nguo mbili kabla haujavaa ile inayoonekana na jamii hivyo hawezi kutoka nyumbani bila ya kuvaa nguo ya ndani
Kwa upande wake mwanamitindo Joketi Mwegelo alisema kuwa wasanii hao wanaovaa nguo bila ya kuvaa za ndani wanatakiwa kujistiri na kwenda na mazingira ili waendelee kulinda heshima yao kwa jamii
Alisema kuwa kama mtoto wa kike ni vyema ukafuata maadili na mazingira ya nchi hivyo basi kukaa utupu ni moja ya kujidharilisha na kushusha soko lako katika sehemu yako ya kazi na kuchangia kupunguza mashabiki ambao kwa namna moja au nyingine unaweza kuwapoteza kutokana na tabia
No comments:
Post a Comment