Friday, May 17, 2013

"SIJAWAHI MVULIA NGUO MWANA FA"...HUSNA





MISS Sinza 2011, Husna Maulid, juzikati ameibuka na kudai kwamba katika maisha yake hajawahi kutoa penzi kwa msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Hamis Mwijuma ‘Mwana FA’.

Husna aliyasema hayo Mei 15 mwaka huu baada ya kuvumishiwa kuwa anatoka kimapenzi na staa huyo na kwamba, kwa sasa hakuna kificho chochote kwani hadi picha zinazowaonyesha ukaribu wao zimezagaa kwenye mtandao.

“Sijawahi kutoka na Mwana FA, zaidi ya kufanya naye tangazo ambalo niliombwa na dada’ngu, Mboni Masimba nikafanye naye kwa ajili ya shoo ambayo anaiandaa hivi karibuni, wanaonihusisha na mapenzi na Mwana FA hawanitendei haki hata kidogo maana sijawahi hata kuwa na wazo naye,” alisema Husna Maulid.

No comments:

Post a Comment