Friday, May 17, 2013

MLINZI WA BAR ACHINJWA KIKATILI NA MAJAMBAZI USIKU WA KUAMKIA LEO





Mlinzi wa baa ya Darajani Stop Over iliyo kando kando ya barabara kuu ya Morogoro Dar es salaam jirani na daraja la Mzambarauni  Bw Mika Athumani amechinjwa na majambazi usiku wa kuamkia leo.


Habari zilizopatikana eneo la tukio zilidai kwamba majambazi hayo yalivamia baa hiyo iliyojitenga usiku wa manane na kumvamia mlinzi huyo na kumchinka kama kuku na baadae kuvunja baa hiyo na kuimba vitu mbali mbali.

Mwili wa marehemu ukiwa ndani ya gari, la polisi kufuatia mwili huo kutenganiswa vibande viwili..



Sehemu aliyochinjiwa mlinzi huyo aliyefahamika kwa jina Mika Athumani.


Akihojiwa na mwandishi wetu,  mmiliki wa baa hiyo Bw Salvatory Mushi alidai kwamba majambazi hao walimvamia mlinzi wake na kumchinja na baadae walivunja Counter ya baa hiyo pamoja na duka ililipojirani na baa hiyo na kuiba vitu mbali mbali.
  

Alipoulizwa kwamba kuna taarifa zinadai kwamba mlinzi huyo alikutwa akiwa amelala Bw Mushi alisema"  inawezekana lakini hakuna mtu mwenye uhakika na jambo hilo kwani sote hatukuwepo,wakti tukio hilo linatokea"
Mwananachi akishuhudia damu ya mlinzi huyo kwa hudhuni


Baskeli ya Mlizni huyo ikiwa imetapakaa damu ambapo inadaiwa mlinzi huyo alikuwa amelala kwenye eneo hilo


Redio ambayo majambazi hayo waliiangusha nje ya baa hiyo


Majaira ya saa 12 asubuhi ya leo wananchi walishuhudia maduka mawili ya baa hiyo yakiwa wazi huku mwili wa mlizni huyo umekutwa upande wa baa ukiwa umechinjwa na kutenganishwa kichwa na mwili


Umati wa watu ukishuhudia tukio hilo muda mfupi uliopita




Gali la polisi likiondoka eneo la tukio na mwili wa marehemu



Wananchi nao waliondoka eneo hilo la tukio


Mmiliki wa baa hiyo Bw Salvatory Mushi akihojiwa na waandishi wa habari eneo la tukio


Majirani wa eneo hilo wakihojiwa na waandishi wa habari


Baadhi ya watu waliokuwepo eneo hilo la tukio walidai kwamba mlinzi huyo alikuwa amelala hivyo majambazi hayo yalimvamia na kumpora siraha zake na kishi kumchinja shingoni..

Mwandishi wetu alishuhudia mtoto wa marehemu pamoja na mjukuu wa marehemu wakiangua vilio eneo la tuko baada ya kuuona mwili wa mazazi wao aliyeuwawa kikatili baadae wote wawili walipanda gari la polisi na kuondoka nao.

No comments:

Post a Comment