Ni muda mrefu sasa kumekuwa na wimbi la watangazaji au maripota wa television na radio wasiomudu kutamka maneno ya kiswahili wanapokuwa wakiripoti/wakitangaza au wakisoma hasa taarifa ya habari.Hii imekuwa kero unapomsikia ripota anatamka maneno mfano bizaa(bidhaa),feza(fedha)saman i(thamani)taalifa(taarifa)n.k. Kifupi matumizi ya r/l,th/s na dh/z ni kero iliyopitiliza kwa hawa watu kwani huondoa ladha ya matamshi ya kiswahili.Sasa swali ninalojiuliza ni vp watu hawa walifaulu usaili(interview)ktk vituo husika na zaidi wanaendelea kuharibu tu.Walifaulu vp mitihani yao tangu shule za msingi mpaka kupata kufikia elimu ya juu? Je maboss hawawasikizi wakawarekebisha? on job trainning hakuna?hata daily briefing pia hakuna?Enyi waandishi nguli mlioko humu jamvini tusaidieni kujadili.
Friday, May 17, 2013
Watangazaji/Maripota Hawa Walipataje Kazi?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment