Monday, April 29, 2013

JB ATANGAZA NIA YAKE YA KUGOMBEA UBUNGE MWAKA 2015........HIKI NDO ALICHOKISEMA




HATIMAYE nguli wa sanaa za maigizo Bongo, Jacob Stephen Mbura ‘JB’ amelianika jimbo atakalogombea ubunge mwaka 2015.


JB aliyaongea hayo mwanzoni mwa wiki hii, jijini Dar es Salaam ambapo alisema macho yake yote yapo Mkoa wa Dar es Salaam ambao una majimbo nane.


JB: Niliposema natangaza kugombea ubunge mwaka 2015 wengi waliamini ni maneno tu, lakini nia yangu ni sahihi. Nitagombea na leo nasema jimbo langu lipo Mkoa wa Dar es Salaam.


Aliongeza kuwa, jimbo atakalogombea litaendelea kubaki kuwa siri ya moyo wake na meneja wake wa kampeni ambaye hakupenda kumtaja jina.


Majimbo yanaounda mkoa wa Dar es Salaam katika uwakilishi bungeni ni Ukonga, Ilala, Kinondoni, Segerea, Kawe, Kigamboni, Ubungo na Temeke.

No comments:

Post a Comment