HUDDAH TOKA KENYA AYAAGA MASHINDANO YA BIG BROTHER..... MWAKILISHI WA TANZANIA ALIA NA WAVUTA BANGI
Maneno huumba....!!! Huddah ameliaga shindano hilo...
------------------------
Huddah ambaye ni mshiriki kutoka Kenya alijikuta akibubujikwa na machozi jana wakati akimuelezea Angelo (SA) kuhusiana na uhusiano wake wa kimapenzi ambao ni wa ku-beep yani vuta nikuvute ambao amekuwa nao nchini kwao.
Mrembo huyo hakutaja jina la mpenzi wake lakini inahisiwa alimaanisha kuwa katika mahusiano na Rapper Prezzo wa Kenya. Kwa muda sasa kumekuwa na umbea mtaani kuhusiana na uhusiano wa kimapenzi kati ya wawili hao lakini haijafahamika kinaga ubaga kama Huddah alimaanisha kum-miss Mr. President. ..
Mrembo huyo akizidi kufunguka, alielezea jinsia anavyo-miss mabusu motomoto, anavyo-miss kung'atwa shingoni n.k. “I miss the way that he kisses me. I miss him biting my neck”..
LEO MACHOZI YAKE YAMELIPWA BAADA YA MREMBO HUYO KUONDOLEWA NDANI YA JUMBA HILO....Mashabiki wamepiga kura ya kumwondoa ili asiendelee kumlilia mpenzi wake.....
Mshiriki mwingine aliyeaga mashindano hayo ni Denzel wa Uganda....
KWA UPANDE MWINGINE, mrembo wa Tanzania ,Feza anayeiwakilisha Tanzania alijikuta katika simanzi kali wakati alipoelezea kuhusu jinsi ambavyo kaka yake aliteseka kutokana na kujihusisha na madawa ya kulevya .. 'drugs'.
Feza alitumia fursa hiyo kuwasihi watu hasa vijana kujiepusha kabisa na madawa ya kulevya kwani ni hatari sana katika jamii inayotuzunguka..
No comments:
Post a Comment