Thursday, March 28, 2013

HONGERA DINA KWA KUPATA TUZO YA WOMEN OF THE YEAR



Leo hii kupitia tuzo za Tanzania Women Of Achievement Award (TWAA), mtangazaji wa Clouds Fm, kupitia kipindi cha Leo tena, Dina Marios, amejichukulia tuzo ya "Women of the year" , katika sherehe zilizofanyika katika hoteli ya Serena, iliyoko jijini Dar es salaam.
"sikutegemea kama nitapata tuzo hii, maana kila mmoja aliekuwa karibu yangu nilimuona kama mtu mzima sana, nikasema hawa ni watu wazima sana mimi hapa sidhani kama kuna changu, ila nikajipa moyo nikasema, hawa akina mama waliopata tuzo wamefanya kazi nzuri sana mpaka kufikia hapa, lakini kabla sijamaliza nikasikia wanataja jina langu ikiwa ni tuzo ya mwisho kutolewa. huwezi kuamini hata sikumbuki nilitoa speech gani pale ila kila mtu alisifia, nimeshukuru sana" amesema Dina
all the best to you, na mungu akuzidishie


No comments:

Post a Comment