28 March 2013- By Admin
Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP Suleiman Kova akiwa maeshikilia baadhi ya vipande vya meno ya Tembo vilivyokamatwa hivi karibuni katika eneo la Kimara Wilaya ya Kinondoni.
Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP Suleiman Kova akifafanua kuwa Jeshi la polisi limeweka mikakati ya mpango kazi ikiwa ni pamoja na kushirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama pamoja na kikosi cha zimamoto ili kuhakikisha kuna udhibiti wa matukio ya uhalifu au fujo.
Aidha amesema jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata bunduki mbili aina tofauti, moja ikiwa ni Shotgun yenye namba AB 44736 na ya pili ni Greener yenye namba 10883 pamoja na risasi 17.
Na.INaMoTO Blog Team
Jeshi la polisi kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kukamata vipande vya meno ya Tembo vipatavyo 13 ambavyo thamani yake haikufahamika mara moja. Tukio hilo limetokea katika eneo la Kimara wilaya ya Kinondoni ambapo askari walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.
Pamoja na kukamatwa kwa vipande hivyo pia amekamatwa mtuhumiwa Christopher Julius mwenye umri wa miaka 18, mwanafunzi wa Kidato cha Nne – Kibaha sekondari.
Katika hatua nyingine kupitia misako mikali inayoendelea Jeshi la polisi limefanikiwa kukamata noti bandia 32 za shilingi elfu 10,000/= zenye thamani ya shilingi 320,000/= za kitanzania.
Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP Suleiman Kova ametoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini hasa katika kuelekea siku kuu ambapo watu wasio na nia njema wanapenyeza pesa bandia kwa nia ya kujiongezea kipato binafsi.
No comments:
Post a Comment