WASANII wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ na Jacqueline Wolper Massawe ‘Wolper’ wamemaliza bifu lao lililokuwa likifukuta kama moto wa kifuu mwishoni mwa wiki mbili zilizopita.
Akizungumza na mwandishi wetu katikati ya wiki hii, Baby alisema alikuwa Mkoani Geita kwa ziara ya kikazi lakini alipigiwa simu na Wolper akimuomba msamaha kutokana na tofauti zao zilizosababishwa na nyumba ya kupanga.
“Nimeona bora yaishe kwa sababu Wolper amekubali kosa na mimi siwezi kuendeleza bifu lakini kama asingeniomba msamaha tungefikishana mbali,’’ alisema Baby Madaha na kuongeza:
“Nimemalizana na Wolper ila kesi itabaki kwa mwenye nyumba, nitapambana naye hadi atakaporejesha mkwanja wangu japokuwa nimepata nyumba nyingine maeneo ya Mikocheni.”
Wolper na Madaha waliingia kwenye bifu zito baada ya Madaha kukuta nyumba aliyoilipia shilingi milioni 3.6 kama kodi maeneo ya Kinondoni jijini Dar imechukuliwa na Wolper kabla yeye hajahamia.
No comments:
Post a Comment