KUFUATIA vitendo vya usaliti wa ndoa, uasherati, ufuska na ukiukwaji wa maadili ya Kitanzania kwa wanandoa, wiki iliyopita Ijumaa iliendelea na Operesheni Fichua Maovu kwa kuzunguka jijini Dar usiku wa manane na kunasa tukio la mke wa mtu akifanya uzinzi ndani ya gari.
Kabla ya kufanya operesheni hiyo, waandishi walitaarifiwa kwamba Wilaya ya Kinondoni jijini Dar ndiyo inayoongoza kwa wake na waume za watu kufanya vitendo vya ngono kwenye magari.
Maeneo yaliyodaiwa kwamba wazinzi hao hupenda kuyatumia ni Coco Beach, Leaders Club, Mlimani City na sehemu kubwa ya vitongoji vya Sinza na Mwenge, Dar.
Mbali na waume na wake za watu, wengine wanaotajwa kufanya vitendo vya ngono ndani ya magari ni mastaa wakubwa ambao wanaogopa kwenda kukodi vyumba mahotelini na gesti wakihofia watajulikana kutokana na umaarufu wao.
Jumatatu ya Aprili Mosi, mwaka huu, waandishi wetu walianza mchakato wa kutembelea vitongoji walivyoezwa kwamba, watu hususan wake na waume za watu hupenda kuvitumia kufanyia ufuska.
Waandishi wetu walitinga kwenye Ufukwe wa Coco uliopo Oysterbay, Dar ambako walishuhudia wasichana wengi waliokuwa wakifanya biashara ya kujiuza ‘machangudoa’ katika viunga hivyo.
Mbali na wasichana hao, pia kulikuwa na vibaka wengi waliokuwa wakiwalinda machangudoa hao ili wasipate matatizo.
Pia, wanaume wengi walikuwa wakifika na wanawake ndani ya magari yao na kupozi kwenye maegesho, wengi wao hawakuonekana kama ni watu na wake zao.
Hata hivyo, waandishi walibaini kwamba magari mengi yanayotumiwa katika eneo hilo ni yale yenye vyoo vyeusi ‘tinted’ hivyo ni vigumu kujua kinachoendelea ndani yake.
Kwa ujanja, waandishi wetu walibaini kwamba ‘pea’ nyingine zilikuwa zikifanya vitendo vya ‘kudendeka’ na wengine kufika mbali zaidi lakini walishindwa kuwavaa kutokana na usalama mdogo katika eneo hilo.
Waandishi wetu walihamishia mtego wake Leaders Club, Kinondoni mida ya saa 8:05, baada ya kupiga misele ya hapa na waandishi walifanikiwa kumbamba mmoja wa wazinzi.
Waandishi walitulia baada ya kuliona gari aina ya Toyota Land Cruiser likiwa katika eneo la maficho nje ya viwanja hivyo.
Gari hilo lilikuwa likitikisika kuonesha kwamba mchezo ulikuwa ukiendelea ndani yake.
Wakati waandishi wakijipanga kulivamia, ghafla waliokuwa ndani walishtuka na kupozi kwa muda.
Hata walipoachiwa ili waendelee, machale yaliwacheza na kuwasha gari kisha kuondoka kwa kasi.
Pamoja na kulikosakosa tukio hilo, waandishi hawakukata tamaa, kuanzia Jumatatu hadi Jumapili waliendelea na utaratibu wa kutembelea viwanja husika.
Jumapili iliyopita baada ya kutembelea viwanja vyote kusaka ‘wahalifu hao’, hatimaye mtego ulinasa.
‘Patroo’ ikiwa kazini maeneo ya Mwenge, Dar jirani kabisa na hoteli moja inayopata umaarufu mkubwa siku za hivi karibu, ghafla gari aina ya Toyota Corona likiwa limepaki kwenye eneo la giza, chini ya mti lilikuwa likitikisika kuonesha kwamba kulikuwa na watu waliokuwa wakifanya ngono.
Safari hii, bila kufanya makosa, waandishi wetu waliwasogelea ambapo na wao hawakuonekana kujali wapita njia....
Credit: GPL-Ijumaa
No comments:
Post a Comment