Friday, April 12, 2013

MZEE CHILO AWACHANA LAIVU WASANII WANAOVAA NUSU UCHI




STAA wa filamu za Kibongo, Ahmed Uloto ‘Mzee Chilo’ amewachana wasanii wa filamu wanaovaa nusu uchi huku akieleza kuwa, kufanya hivyo ni kuiabisha tasnia ya fimlamu Bongo.

Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Mzee Chilo alisema amekuwa kwenye tasnia hiyo kwa muda mrefu sana na kuwashudia wasanii kama vile Suzan Lewis ‘Natasha’ na mama Mjata wakiigiza filamu zao kiheshima lakini siku hizi anashangazwa na uvaaji unaokiuka maadili, si kwenye filamu tu bali hata kwenye maisha yao ya kila siku.

“Mbona kuna hawa wakongwe ambao wanaigiza vizuri na kufikisha ujumbe bila kuvaa nusu uchi? Kwa kweli hali sasa hivi ni mbaya na wasanii hasa wa kike wanatakiwa kujirekebisha wanapokuwa wanaigiza na hata kwenye maisha yao ya kawaida,” alisema Mzee Chilo.

No comments:

Post a Comment