Thursday, February 28, 2013

MAMA KANUMBA AJA NA ' WITHOUT DADDY'




FLORA Mtegoa ambaye ni mama mzazi wa aliyekuwa mwigizaji wa filamu za Bongo, Steven Kanumba (marehemu sasa), ameigiza filamu ya Without Daddy akiwa na watoto na wasanii walioshiriki katika filamu ya Bigg Daddy ya marehemu Kanumba. 
Mama Kanumba ambaye amedai kuwa filamu hiyo ni mwendelezo wa filamu ya mwanaye na kwamba baada ya filamu hiyo hataigiza tena. 

Nimeigiza katika filamu ya Without Daddy katika kuonyesha uwezo katika uigizaji, lakini sidhani kama naweza kuigiza filamu nyingine tena, ni kazi ngumu na inahitaji muda sana. Pia nisingependa kuwa mwigizaji wa moja kwa moja, anasema Mama Kanumba. 
Katika filamu hiyo nyota walioshiriki ni Cathy Rupia, Ben Blanco, Muhogo Mchungu, Bi. Mwenda, Patcho Mwamba Tajiri Othuman Njaidi Patrick,Wastara Juma na wengineo.

No comments:

Post a Comment