Sunday, March 31, 2013

BREAKING NEWSSSS!! RAIS KIKWETE AMFUTA KAZI MKUU WA MKO WA DAR ES SALAAM BAADA YA JENGO LA GOROFA KUMI NA SITA KUANGUKA.



Rais Jakaya Kikwete

Habari zilizotufikia hivi punde kutoka vyanzo vyetu vya habari, Rais Kikwete amemfukuza kazi Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar es salaam Said Meck Sadick kutokana na uzembe wa kutosimamia kikamilifu ujenzi holela ambao unafanywa na wakandarasi ambao hawana sifa jijini Dar es salaam. Uamuzi huo Rais ameutangaza usiku huu muda wa saa 6.15 leo tarehe 1/04/2013 na kuiacha nafasi yake ya ukuu wa mkoa ikikaimiwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi mpaka hapo atakapo mtangaza Mkuu wa mkoa mwingine.

Sambamba na Mkuu wa Mkoa, Rais amemsimamisha kazi Msimamizi wa Mkoa katika Idara ya Ujenzi sanifu, pamoja na maafisa wawili ambao ni wakaguzi wa majengo wakati yanapokuwa yanajengwa.

Hatua hiyo ya Rais imekuja kutokana na Jengo lenye Gorofa 16 kuanguka na kuonekana uongozi wa juu kuto kuwa na taarifa zozote juu ya ujenzi wa jengo hilo ambalo halikuzingatia vigezo ambavyo vimewekwa kwa ajili ya ujenzi huo, kimoja wapo ni kile ambacho kilitaka ujenzi huo kuishia gorofa 12 na mkandarasi kujenga mpaka gorofa 16. Mheshimiwa Rais ameagiza wale wote ambao wamehusika katika kufanya uzembe wa ujenzi huu wachukuliwe hatua stahiki kulingana na kosa husika. Mpaka hivi sasa ni maafisa kadhaa wameshakamatwa akiwemo mkandarasi ambaye alikuwa analijenga jengo hili.

Kwa kutambua leo ni Tarehe 1 mwezi wa nne tunaamini unaweza ukatambua Rais amechukua maamuzi ambayo ni sahihi ili kuweza kujenga heshima kwa watendaki wake na iwe mfano kwa wengine.
Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

1/04/ 2013

No comments:

Post a Comment