Friday, March 29, 2013

Diamond Platinum akiwa na judges katika music video audition ya kumtafuta model ambaye ataweza kufanya video mpya ya Diamond Platinum.Zoezi ili lilifanyika katika maeneo ya Nyumbani lounge Jijini Dar es Salaam

.

Diamond hapo akielezea sababu na dhumuni zilizomfanya mpaka afanye hivyo huyu hapa anafunguka kwa dzain hii "kusema kweli nimeona umuhimu kwasababu unakuta pale msanii anapoamua labda kufanya video mpaka aanze kutafuta watu lakini mimi nikaona kwanini ni si ajili watu wa kunifanyia video zangu kama models na ndiyo maana leo hii ni siku maalum ya kumtafuta yule ambaye ataweza kufanya video mpya ya kwangu na pia kumuajili katika kazi zangu za muziki kwa hiyo pale ninapoamua kufanya video ninakuwa ninajua kabisa nina watu kadhaa wa kufanya nao video".Hayo ndiyo maneno ya Diamond wa wasafi akielezea sababu na dhumuni la kufanya Music Video Audition leo maeneo ya Nyumbani lounge jijini Dar es Salaam.
 

No comments:

Post a Comment